Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Nani aliyetulaani wana wa mkoa wa Mara?

Shida watu wa Mkoa wa Mara ni wabinafsi hata wao kwa wao hawapendi kuona mwenzao kapata. Kingine kinachotuumiza ni UCHADEMA mwiiiiingi. Unakuta mtu yuko CCM lakini akiona anayegombea CCM sio kabila lake anakisaliti chama na kukisaidia chama cha upinzani. Naomba tusiwalaumu JK wala JPM, toka enzi za Nyerere marais wetu wamejitahidi sana kutupa nafasi lakini hatukujua kuzitumia. Matokeo yake baadhi ya wateuliwa wakishapata nafasi wanahamia Dodoma na kula maisha na Toto's. Sidhani kama Rais atakuteua then akuelekeze nini cha kufanya. Wenzetu wachaga wanajua sana kitumia fursa na ndio maana sasa hivi JPM kawabania wanaanza kutoa Nyaraka wakati walipaswa wanyamaze maana hii nchi wameila sana. Mwisho naomba tusaidiane kutaja viongozi waliotoka mkoa wa Mara ili tujue ujinga ni wetu na sio wa wale wanaotuteua. Nitakao wasahau mtanikumbusha. 1. Dr Wanyancha. N.waziri wa ujenzi/Mjumbe wa Bodi ya Tanapa. 2. Dr Mwita N.waziri Tamisemi. 3. PR Muhongo. 4. Dr. Sarungi yeye alichofanya ni kuoa Mzungu 5. Wasira. 6.Jaji Warioba 7. Dr Kebwe.8. Mama Kabaka 9. Kamanda Siro. 10. Jaji Werema. 11. Jerenerali Kyaro12. Kichele TRA na wengine wengi. Haya linganisha na wachaga kama hujaishia kumtaja msuya tu. Tena hao wa mkoa wa Mara ni wasomi tupu.
Alafu wote uliowataja ni CCM, Maendeleo hakuna..

Huyo ndiyo Mchawi wenu badirikeni nyie watu ..

Zaidi ya miaka 50 ya uhuru bado mnalialia eti sijui..Mara hakuna Maendeleo na bado mnachagua CCM..
 
Popoma kama wewe huwezi kuelewa hii ni nini maana yake

Tatizo la mkoa wa Mara ni Nyerere fullstop. Hata wakati wa vita watu wanajiandikisha wakapigane vita ya Uganda aliwapunguza idadi ili kuwe na mgawanyo nchi nzima.

Mkumbuke hata Nimrod Mkono na utajili wake wote pale Busegwe alikuwa anakaa kwa baba yake mpaka alipokufa Nyerere ndio amehama kwao amejenga kasri lake na amejenga mashule na kuikabidhi serikali, Mkono angekuwa anatoka mkoa mwingine yale mashule angeyafanya mradi wake private au angejenga mahotel Musoma mjini.

No research no right to speak



Hivi kweli wasomi kabisa tunapoteza muda kujadili ukabila! Nchi zingine wanatujua sisi ni watanzania. Ni ngumu kujua huyu Mkurya au Mzaramo. Tutajadili makabila lakini tutabaki kuwa watanzania. Na hakuna kabila zuri au lilo juu ya lingine. Wengine ni kwakuwa tu hatupendi kujadili makabila, lakini si kwamba hatujui udhaifu wa makabila mengine. Watanzania tunakoelekea siko. Kama watu mnataka kutambika si mkatambike. Kwanza Mleta mada kaongea kuhusu mkoa wa Mara si makabila watu wanaanza kujadili makabila. Mara inamakabila 24, wenyeji au waasili. Lakini bado kuna wahamiaji. Mkoa kupata maendeleo ni kwa wadau wote walioko hapo si uasilia wa kabila. Angalia Miji mikubwa kama Dar, Mwanza, Arusha na sasa hata Dodoma. Si kwamba imejengwa na makabila asili bali wadau waliopo katika mikoa hiyo. Tuache kuongelea ukabila tuangalie namna za kuendeleza maeneo yetu mbalimbali kwa fursa zilizopo.
 
Alafu wote uliowataja ni CCM, Maendeleo hakuna..

Huyo ndiyo Mchawi wenu badirikeni nyie watu ..

Zaidi ya miaka 50 ya uhuru bado mnalialia eti sijui..Mara hakuna Maendeleo na bado mnachagua CCM..
Hujui ulisemalo wewe, Tanzania hii ni mkoa wa Mara na Kilimanjaro tu ndio mikoa pekee iliyoonesha kwa vitendo kuikataa ccm labda unaweza kuiingiza na Kigoma humo, fuatilia historia kabla ya kubwabwaja.

Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mkoa mzima wa mara unajuwa Nccr Mageuzi ilizowa majimbo mangapi na ccm iliambulia jimbo gani?
 
Wewe ungesema watu wa Musoma vijijini hawaelewani. Maana hao wote kwao ni Musoma Vijijini.

Muhongo, Maswi, Werema na Mkono wote ni wa Musoma vijijini na mbunge wao alikua Mkono kabla hawajaligawanya jimbo hilo.

Watu wa Serengeti huna haja ya kuwalaum maana serikali mdio haikufanya mgawanyo sahihi wa rasilimali, Mbuga iko Serengeti ila makao makuu yakawa Arusha.

Watu wa Arusha wakaendelea kwa kutumia mgongo wa watu wa Serengeti.

Tatizo la mkoa wa Mara ni unequal distribution of resources. Mkoa wa Mara ni mkoa tajiri, una dhahabu na madini mengine karibu kila kijiji, una ziwa, una mbuga kubwa kuliko zote Afrika.

Cha ajabu, Dhahabu yote haiwasaidii watu aa Mara, migodi ya kihuni kama Meremeta imewaibia wana Mara, North Mara kila mtu anajua, Serikali ikaua viwanda vyote vya samaki, wao watauza wapi samaki? Wajita na wakwaya wamebakia kua na majungu tu maana hawana kazi nyingine ya kufanya.

Serengeti haiwasaidii wana serengeti, mbuga inayoingiza 80% ya mapato ya utalii Tanzania, cha ajabu wanaofaidika nayo ni watu wa Arusha na Kilimanjaro. Hata chuo kimoja cha utalii cha serikali cha ngazi ya cheti serikali haikuwajengea wakazi wa serengeti, vyote viko Arusha na Kilimanjaro.

Watu wa Mara hasa Serengeti na Tarime wana ardhi nzuri ya kulima, wanalima misimu 2 kwa mwaka lakini hawana masoko, wakitaka kuuza Kenya serikali haitaki, wanakua hawana namna zaidi ya wizi wa ng'ombe.

Serikali ndio imechangia kuua mkoa wa Mara. Watu wa Mara inabidi tuwalaum wenzetu waliotangulia kupata fursa kisha hawakuendeleza mkoa wetu.

Watu wengone wakipata uwaziri wa maji tu mikoa yao inakua na maji hadi ya kuogeshea kuku, urais ndio balaa.

Watu wa Mara tujifunze. Ukipata fursa itumie.
Hii comment yako imeniumiza sana moyo. Nimejenga chuki na watu fulani.
 
Tatizo kubwa la watu wa Musoma ni ubaguzi ulioegemea kwenye koo, na kabila, mfano Wakurya wamewagawanyika zaidi ya koo 10 na wanabaguana hasa yaani akitokea kiongozi kwenye koo fulani hapewi ushirikiano na koo nyingine, hata makabila ni hivyo hivyo. Ukweli ni kwamba watu wa Mara hawapendani kwa misingi hiyo hasa kutokana uhasama wa koo na koo au kabila na kabila.
Kuchukiana imetokana na divide and rule policy ya Nyerere baada ya jaribio la kuanzisha Jamhuri ya Chui. Aliwagawa wakurya baada kuona ni watu hatari sana kwa utawala wake. Mojawapo ni kuwachonganisha kwa kuvuruga mipaka ya vijiji. Fanya research utajionea
 
Wakurya wana wivu na majungu sana.
Get your fact right.
Usisukumwe na chuki. Wivu na majungu hayatokani na kabila la mtu bali malezi na mazingira. Unataka kusema makabila mengine hayana wivu na majungu? Yes wapo wenye wivu na majungu but sio wote kama ilivyo makabila mengine.
Acha haste generalization.
 
Kabisaaa.... kubwa kuliko yote ni wivu!! Anaweza kukukasirikia kisa tu unamzidi kitu fulani.... yupo tayari kukopa ili anunue kitu ashindane nawewe
Mbona umekazania kuhusu wivu? Unaweza kuthibitisha kwa hoja za kisomi?watu wachache wasikupe uhalali wa kuwanjia heshima wengine. Taja mkoa wako unaotokea ndipo tufanye ulinganishi.
Kwa haraka haraka nimehisi una chuki na mmoja wa watu wa Mara so unatafuta namna ya kujifariji.
Mara ni moja ya mikoa yenye makabila mengi, je inawezekanaje wote wakawa na wivu sawa kiasi unachodai?
 
Mutatigha ubhukangi bhare bhachabhani, weito Mara itarenge igho mokogheghamba, yaani mnaongea kitu msichokijua na mnafanya analysis ya uongo, Mara tupovizur na tunaendana na jins uchumi unavyokuwa na jinsi vipato vya wanamara vinavyoruhusu, ivi ni mkoa gan ambao hauna ushirikina? Ni mkoa gan ambao hauna maeneo ya vijijin na watu maskin? Nazan hapa tujadili kwa muktaza wa uharisia wa maisha ya mtanzania na sio kusema Mara ilikuwa na viongoz BT maendeleo hakuna, kwanza uliesema Mara hakuna maendeleo labda utuambie ulimaanisha maendeleo yapi? Coz kama ni fursa za biashara, kilimo, ufugaji, zote zipo, haya miundombinu ipo main road sirari to mwanza,3airports nyamongo, musoma na mugumu, kuna bandar musoma, secondary schools A level and o level za kutosha, university IPO, vyuo vya diploma na certificate vya kila fani vipo, kama ni wasomi wapo wa kutosha. Au we mleta mada ulitaka Mara iweje ?
Waulize je Mara ni mbovu kuliko Lindi? Au Singida? Au Shinyanga? Na Kigoma je?
Waambie waingie kwenye tovuti ya NBS waangalie takwimu za umasikini watajua mkoa wa Mara hauko vibaya interms of level of povert of people
 
Nawashukuru kwa michango yenu ,ila kuna mambo nataka niyaweke sawa.Welema anatokea Kijiji kinaitwa kongoto wilaya ya Butiama,Mhongo anatokea Majita ,Mkono anatotokea Butiama na Eriakimu Maswi kwao ni tarime,Uliyeongelewa wakurya utakuwa hujafanya utafiti vzr,Hakuna kabila lenye husuda kwa mkoa wa Mara kama Wajita yego jaji, Suala la watu kujenga kwao inatengemeana ila siyo mambo ya kurongwa .Nenda kwao Jaji Warioba huwezi amini kuwa ndipo anatokea,Lkn kwao mke wake moshi mambo yako vzr,Hivyo hivyo kwao welema alijenga msonge tena baada ya wazee kukomalia kuwa huwezi kufikia kwenye nyumba mama yake mzazi,Kwahiyo suala la kujenga hata wanawake tunaoa wanaweza kuchangia mwanaume kushindwa kuwekeza nyumbani.
Kwa hilo la kusingizia wanawake litawagharimu sana,mwanamke anasababisha vp ww usijenge kwenu?,hebu kuweni serious bhana...
 
Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo imebahatika kutoa viongozi wengi katika Serikali zote za kuanzia muasisi wa taifa hili.Lakini ni kati ya mikoa ambayo maendeleo yake yako nyuma sana, ukifatilia kiundani ni kuwa hata viongozi ambao walipewa nyadhifa mbalimbali wao kwa wao hawaelewani bila kujali itikadi zao za vyama.

Kwa mfano Wasira na Jaji Warioba ni watu wasiopikika chungu kimoja japo wote wako ccm. Mwanasheria mkuu aliyestafu Jaji Welema na Mbunge Nimrod Mkono na Pro ,Mhongo ni maadui na uhasama huu unatokana na masilahi,baada ya kuchaguliwa Mhongo kuwa waziri wa nishati kwa kushirikiana na Mwanasheria mkuu Jaji Welema walikata mirija ya ulaji ambayo Nimrod mkono alikuwa analipwa kwenye kampuni yake ya uwanasheria kutokana na lile sakata la Dowas.

Mkono nae nae akaamua kuwalipua kwa kumpa documents Kafulila na kuwakomalia mbugeni na kusababisha Mhongo,Eriakim Maswe na Welema kupoteza nafasi.

Ninachomaanisha hapa ni kuwa viongozi kutoka mkoa wa Mara bila kujali itikadi zao ni watu ambao hawawezi kukakaa meza moja na kuzungumzia matatizo ya Mara kwa sababu wao kwa wao hawapendani.

Ni mji ambao hata miundombinu yake ni shida pamoja na kuwa na ziwa victoria lkn maji bado ni shida hasa kwa wakazi wa nje kidogo ya mji, Ukienda makao mkuu ya wilaya ya Serengeti mji wa Mugumu huwezi amini palivyo choka na wakati wako karibu na hifadhi.

Wakuu wa kaya nao wameususa kuanzia awamu ya Jk na sasa JPM ndio hana hbr kabisa na mkoa wa Mara.

Tupatiwe fursa hata viwanda vilivyokuwepo vifanye kazi pamoja na kuwa na chuo kikuu ,kwani chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere ni jina tu hakuna kinachoendelea.


Nafikiri laana kubwa waliyonayo ni kule kudhalilisha wanawake kwa kuwakeketa bila ridhaa yao. Mwanadamu anapokosa kiungo mwilini anakuwa si wa kawaida na anapolalamika kwa mwenyezi Mungu LAZIMA Mungu atalipizia tu. Waache kukeketa wanawake, ule ni upuuzi. Kilio cha mwanamke Mungu anakiitikia kwa kishindo.
 
Hapo Mnaongelea Musoma na vitongoji vyake, Tarime pako poa sana, ni mji ambao mgeni hata akifika hatamani kuondoka, fursa zipo kibao, na Yule aliyesema Wakurya wana husuda na fitina hawajui vizuri, labda anahisi Mkoa wote wa Mara wenyeji ni Wakurya, Musoma nature ya eneo ndio inapafanya pawe nyuma, ni peninsula, barabara ya kutoka na kuingia ni hiyo hiyo moja, hakuna shughuli yoyote ya maendeleo mbali na uvuvi ambao ni wa kusuasua ukilinganisha na maeneo mengine kama Bunda na Mwanza, hali ya hawa na ardhi sio nzuri kwa kilimo, wenyeji wake sio wafugaji, pale kupata maendeleo ni ngumu sana, ni bora hata Makao Makuu ya Mkoa wangepeleka Tarime
Hivi Tarime ni Halmashauri ya Mji mdogo au ni Mji kamili?

Vv
 
yani kama ulikuwepo kichwan mwangu...
ni selfish
wajivuni
wajuaji
kunaaringo fulani hivi../kujisikia
wanajua kila kitu....
Hizo ni tabia za baadhi ya makabila ya huko ila sio wote, kwa hiyo msipende kujumuisha
 
Back
Top Bottom