mwamlgallah
Member
- Sep 27, 2016
- 83
- 52
Mbunga huwa sielewiWewe ungesema watu wa Musoma vijijini hawaelewani. Maana hao wote kwao ni Musoma Vijijini.
Muhongo, Maswi, Werema na Mkono wote ni wa Musoma vijijini na mbunge wao alikua Mkono kabla hawajaligawanya jimbo hilo.
Watu wa Serengeti huna haja ya kuwalaum maana serikali mdio haikufanya mgawanyo sahihi wa rasilimali, Mbuga iko Serengeti ila makao makuu yakawa Arusha.
Watu wa Arusha wakaendelea kwa kutumia mgongo wa watu wa Serengeti.
Tatizo la mkoa wa Mara ni unequal distribution of resources. Mkoa wa Mara ni mkoa tajiri, una dhahabu na madini mengine karibu kila kijiji, una ziwa, una mbuga kubwa kuliko zote Afrika.
Cha ajabu, Dhahabu yote haiwasaidii watu aa Mara, migodi ya kihuni kama Meremeta imewaibia wana Mara, North Mara kila mtu anajua, Serikali ikaua viwanda vyote vya samaki, wao watauza wapi samaki? Wajita na wakwaya wamebakia kua na majungu tu maana hawana kazi nyingine ya kufanya.
Serengeti haiwasaidii wana serengeti, mbuga inayoingiza 80% ya mapato ya utalii Tanzania, cha ajabu wanaofaidika nayo ni watu wa Arusha na Kilimanjaro. Hata chuo kimoja cha utalii cha serikali cha ngazi ya cheti serikali haikuwajengea wakazi wa serengeti, vyote viko Arusha na Kilimanjaro.
Watu wa Mara hasa Serengeti na Tarime wana ardhi nzuri ya kulima, wanalima misimu 2 kwa mwaka lakini hawana masoko, wakitaka kuuza Kenya serikali haitaki, wanakua hawana namna zaidi ya wizi wa ng'ombe.
Serikali ndio imechangia kuua mkoa wa Mara. Watu wa Mara inabidi tuwalaum wenzetu waliotangulia kupata fursa kisha hawakuendeleza mkoa wetu.
Watu wengone wakipata uwaziri wa maji tu mikoa yao inakua na maji hadi ya kuogeshea kuku, urais ndio balaa.
Watu wa Mara tujifunze. Ukipata fursa itumie.
Sent from my HTC Desire 526G dual sim using JamiiForums mobile app