Mtu anaenda hospital labda ana shida ya kukohoa au shida nyingine ya mfumo wa upumuaji, daktari anamuandikia Azithromycin au Azuma kama tunavyoita huku mtaani,kwa sababu ni dawa nzuri sana ya magonjwa ya mfumo wa hewa.
Mgonjwa akiona kapewa Azuma anakataa au anachukua ila akifika nyumbani hatumii,anaenda kununua dawa anayoijua mwenyewe jambo linaloathiri matibabu yake. Hii ni kwa sababu,mgonjwa anaamini daktari kampa dawa ya magonjwa ya ngono na sio dawa ya ugonjwa anaoumwa yeye. Hizi stori nimeziskia sana, imebidi nijiulize, hii imani ilitoka wapi?
Azithromycin sio dawa chaguo la kwanza la kutibu magonjwa ya ngono na kuna magonjwa mengi ya ngono ambayo Azuma haitumiki kabisa katika matibabu yake.
Ilikuwaje sisi tukahusianisha Azuma na magonjwa ya ngono kwa kiwango hicho?