Sultan MackJoe Khalifa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2022
- 6,782
- 14,148
Kama ni kweli Mbowe hatagombea kwanini wachaga wameanza kumuita Lisu kirusi cha CCM?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usimuamshe aliyelalaChadema ni wajanja wajanja sana na wanajua kubakia katika headlines. Hata hii kuchelewa kufanya uchaguzi ni kuendeleza hilo ili tunapoelekea uchaguzi mkuu wanakuwa wamevuna watu wengi sana.
Nazan ww ndio una taarifa za chama hebu tupe information wana chama wenzako mana safari hy niligoma hata kujiandikisha katika daftari la wapiga kuraUsimuamshe aliyelala
Usiondoke JFNazan ww ndio una taarifa za chama hebu tupe information wana chama wenzako mana safari hy niligoma hata kujiandikisha katika daftari la wapiga kura
Hicho ndicho cha kushangaza. Lakini nadhani itakuwa busara kwa Mbowe kuweka wazi azma hiyo ya kutogombea ili joto lipoe kidogo. Mimi sidhani kama Mbowe hakujua kuwa hii ilikuwa nia ya Lissu ya muda mrefu kidogo. Matamshi na matendo yake kwa muda sasa yameashiria kuwa haridhiki na hali ilivyo ndani ya chama chake. Hatua ya mwisho ya kupuuza kikao kilichoitwa na kubakia Singida kuhudhuria mazishi ya mgombea wa CDM ilikuwa ishara kubwa.Tangu jana, mara baada ya Wakili Tundu A.M. Lissu kutangaza kugombea uenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, kumekuwa na 'kuwapambanisha' Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe na Lissu kwenye uchaguzi wa CHADEMA utakaofanyika mwakani.
Kuna siku nilimsikia Lissu akisema kuwa mtia-nia yeyote ndani ya CHADEMA huwasilisha nia yake hiyo kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA. Hadi hapo, taarifa rasmi za mtu fulani kugombea nafasi fulani ndani ya CHADEMA hutolewa na mgombea mwenyewe au Katibu Mkuu.
Sikuwahi kumsikia Mbowe au Katibu Mkuu Mnyika kutoa taarifa rasmi kuwa Mbowe atagombea tena uenyekiti wa CHADEMA Taifa kwenye uchaguzi ujao. Sasa, nani hasa anatuaminisha kuwa Mbowe na Lissu watapambania uenyekiti wa CHADEMA?
Binafsi, naona kumeshakuwa na maridhiano na makubaliano baina ya Mbowe na Lissu kuachiana nafasi hiyo ya uenyekiti. Kama Mzee Mtei alivyomwachia Hayati Bob Nyange Makani; Makani alivyomwachia Mbowe ndivyo sasa Mbowe anavyomwachia Lissu.
Endapo Mbowe atagombea, mchuano utakuwa mkali na CHADEMA haitabaki salama baada ya uchaguzi huo. Kwa kauli za Lissu juu ya uchaguzi huru na haki na endapo atashindwa, namuona (kama nilivyomuona Mchungaji Msigwa) Lissu akiondoka CHADEMA.
HahahaNi hawa akina mama wa UWT ndiyo wanashadadia mambo ya CHADEMA huku CCM hakujawahi kufanyika uchaguzi wa Mwenyekiti hata siku moja, kuhusu Lissu kuondoka CDM haiwezi kufa aliondoka Zitto, Slaa, Halima na haijafa sembuse Lissu? Lissu siyo tishio kama watu wanavyodhani isipokuwa ni tishio sababu anapata support ya CHADEMA.
Kwa sababu yanajua misumari yake ni ya moto sana. Na akimuongeza Heche, lazima vijana waende barabarani , ya Asadi yatakuja mapema sana hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025. Hicho tu ndicho ccm wanaogopa.Maccm yamehamaki sana Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema.
Swali gumu sanaKwani nyie UWT ni lini mlichagua Mwenyekiti wa CCM? waligombea na nani? mtindo wenu wa fomu ni moja
PamojaHahaha
Hivi wale vibaka ya CDM bawacha watakuwa wapo upande gani ?Ni hawa akina mama wa UWT ndiyo wanashadadia mambo ya CHADEMA huku CCM hakujawahi kufanyika uchaguzi wa Mwenyekiti hata siku moja, kuhusu Lissu kuondoka CDM haiwezi kufa aliondoka Zitto, Slaa, Halima na haijafa sembuse Lissu? Lissu siyo tishio kama watu wanavyodhani isipokuwa ni tishio sababu anapata support ya CHADEMA.
Yaani wachagga waliopo kwenye hii saccos wanasababisha matatizo aiseeKama ni kweli Mbowe hatagombea kwanini wachaga wameanza kumuita Lisu kirusi cha CCM?
Lini alikuambia kuwa atagombea?Mimi naamini Mbowe atagombea tena kwasababu kwa Mwenyekiti aliye madarakani na hana nia ya kugombea,angelisema mapema ili wanachama wengi zaidi wawe huru kugombea.
Lema naye ni CCM!!?Maccm yamehamaki sana Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema.
Niliyoandika nimeandika.Lema naye ni CCM!!?
Utajijua..🚮🚮Niliyoandika nimeandika.
Namuona pia J. Heche akiwa makamu mwenyekiti.Ni hawa akina mama wa UWT ndiyo wanashadadia mambo ya CHADEMA huku CCM hakujawahi kufanyika uchaguzi wa Mwenyekiti hata siku moja, kuhusu Lissu kuondoka CDM haiwezi kufa aliondoka Zitto, Slaa, Halima na haijafa sembuse Lissu? Lissu siyo tishio kama watu wanavyodhani isipokuwa ni tishio sababu anapata support ya CHADEMA.
Sasa hivi CCM wanamtaka Mbowe agombee tena uenyekiti😂😂😂Maccm yamehamaki sana Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema.
Utajijua wewe unaye nifuata fuata.Utajijua..🚮🚮