Nani amesema kuwa Freeman Mbowe atagombea tena uenyekiti CHADEMA?

Acha inyeshe zaidi au mnatupima imani afu mtuteke mazima..? Lakni lissu anastahili
 
Mbona hotuba yote ya Tundu Antipas Lisu iko Wazi kabisa 😀
 
Maridhiani gani hayo yakusemana, eti hela za Chama zinaishia mifukoni mwa watu!!
 
CHADEMA inahitaji Viongozi wapya wote. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Naibu Katibu both bara na visiwani. Halafu atafutwe Kijana mwenye influence awe Mkurugenzi wa sera, bunge na mawasiliano.
 
Kwamba cdm hawatakuwa wamoja kwasababu ya uchaguzi? Hii dhana ya upotoshaji huwa mnaitoa wapi? Cha muhimu ni kuwa na uchaguzi wa mfano, kura zihesabiwe kwa haki, na mshindi halali atangazwe. Huu upuuzi wa ccm wa kuingiza kura fake ubaki huko huko ccm.
 
Lisu alikwishasema kuwa yeye ana akili timamu, hawezi kuondoka CHADEMA.

Wasio na akili timamu ndio hao wanaokazania kuwa eti Lisu akishindwa kwenye ushindani wa nafasi ya Mwenyekiti anaondoka CHADEMA.

Lisu ataondoka CHADEMA kama CHADEMA itaondoka kwenye misingi yake, siyo kwa sababu ya kushindwa kwenye uchaguzi.
 
Ngoja tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…