Nani amesema kuwa Freeman Mbowe atagombea tena uenyekiti CHADEMA?

Endapo Mbowe atagombea, mchuano utakuwa mkali na CHADEMA haitabaki salama baada ya uchaguzi huo. Kwa kauli za Lissu juu ya uchaguzi huru na haki na endapo atashindwa, namuona (kama nilivyomuona Mchungaji Msigwa) Lissu akiondoka CHADEMA.
Mimi pia niataachana na siasa kabisa endapo Mbowe atachukuwa fomu ya kugombea uenyekiti.

Natarajia kumuona Mbowe akiwa mstari wa mbele wa mapambano kama mwanachama na kama mshauri.
 
Alipokosea Lissu ni nini? Kusema chama kina mapungufu au kuna lingine?
Lissu hanunuliki ndio dhambi kuu?
Upinzani unahitaji mapinduzi makubwa sio mazoea.

Lissu ni sahihi
Mbowe Akubali mabadiliko asilete um7 wake
Covid19 ni mbowe na mbowe ni covid19
 
Sasa asipogombea atafanya kazi gan ambayo itamkutanisha na watu wakubwa,wazito na mashuhuri najua ni tajiri ndio,.

Ila ata uwe tajir vp kuna watu huwez kua nao krb km sio mtu wa system
 
Alipokosea Lissu ni nini? Kusema chama kina mapungufu au kuna lingine?
Lissu hanunuliki ndio dhambi kuu?
Upinzani unahitaji mapinduzi makubwa sio mazoea.

Lissu ni sahihi
Mbowe Akubali mabadiliko asilete um7 wake
Covid19 ni mbowe na mbowe ni covid19
Mkuu, kuna mahali popote niliposema kuwa Lissu amekosea?
 
Mimi pia niataachana na siasa kabisa endapo Mbowe atachukuwa fomu ya kugombea uenyekiti.

Natarajia kumuona Mbowe akiwa mstari wa mbele wa mapambano kama mwanachama na kama mshauri.
Msiowe waoga, Lisu anaweza kujieleza, kujenga hoja, na anao ushawishi.

Hivyo ni vyema akagombea na Mbowe, amabaye hana ushawisi, asiyejua kujenga hoja, na dhaifu, ili kuthibitisha hayo amshinde kwa kishindo.

Huwezi kuwa mpenda haki halafu hutaki watu wagombee nafasi za uongozi.

Mbowe asipogombea Lisu atagombea na nani, au ndio atapita bila kupingwa?

Na kutakuwa na tofauti gani yeye na CCM? Mbowe agombee ili ashindwe na Lisu ndiyo italeta heshima ndani ya CHADEMA, tuache kutafuta namna za Lisu kupita bila kupingwa itakuwa haileti maana, ikiwa nafasi inapaswa kugombewa.
 
Mkuu petro ungizatia kibonzo hiki hutapata shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…