Nani ametoa Kauli ya kukubali Kujiuzulu kwa Ndugai? Hajajiuzulu!!?

Nauliza tu maana bila kuambiwa kama amekubaliwa kujiuzulu anaweza kutengua barua hiyo na hakutakuwa na la kumfanya. Unapojiuzulu mamlaka unayowajibika kwake inatakiwa iseme imekubali. Hii ndio sababu wakati mwingine mtu anaweza kukataliwa kujiuzulu (mifano ipo mingi).

Taarifa ya Katibu wa Bunge kuwa kapokda taarifa kutoka Katibu Mkuu wa CCM kuwa chama hicho kimeridhia ni potosí nq inabeba makosa ya kiutendaji. Hakujafanyika kikao chochote cha KK ya CCM kujadili tukio hilo. Haiwezekani KM akubali kujiuzulu kwa Spika.

Vipi kama Spika Ndugai ALISHIKIWA BUNDUKI na kulazimishwa kuandika barua hiyo (under duress) kutokana na sauti za kumtaka kujiuzulu? Yaani CCM haikuchukua hata dakika moja kumuuliza kana "hiari" ni "hiari" kweli.

Kujiuzulu kwa Spika hakuwezi kufanywa kiholela hivi kana kwamba aliyejiuzulu ni mpishi wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkata...

Kinyume na wengine.. sijui kama Spika amejiuzulu kweli... ndio ufyatu wenyewe huu.

Kweli aende lakini aende kiukweli...akiibuka na kusema ametishiwa maisha... ? Yaani hata kukutana na KM hakujafanyika tunakubali tu?

Acheni ufyatu!!!
Nimepenyezeqa habari kuwa alipelekewa ule mkaratasi asaini tu
 
Katibu wa bunge amekiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM. Hii maana yake CCM iko juu ya bunge ndio maana Ndugai baada ya kusutwa kule ikulu na mwenyekiti wake akaamua kujiuzulu.

Hapa naona hata kama taratibu hazikufuatwa, lakini kwasababu ya "uchama" uliotawala vichwa vyao, hili jambo kuna uwezekano mkubwa likaachwa lipite kimya kimya kwasababu ya mazoea.
Kukiri sio shida je amejibiwa?? Na nani anahusika kukubali kujiudhuru kwake
 
Vyovyote iwavyo, ama atakubaliwa au kukataliwa kujiiuzulu; hiyo haiondoi uhuru wa watanzania kuhoji suala la kukopa na kukatwa tozo kwa wakati mmoja. Na fedha zote zinatajwa kufanya maendeleo ya aina sawa. Ujenzi wa vyumba vya madarasa ni jambo jema, ila je una tija kwa pato la taifa? Fedha za kurudisha mkopo zitatoka wapi? Au tutaendeleza utaratibu wa kumkopa john ili kumlipa ally?

Lini tutaanza kujitegemea wenyewe kwa kuanzisha miradi yenye tija na kuacha kujenga masoko yasiyozalisha? Kuendelea kuwabana wananchi kwa kupandisha bei ya bidhaa na tozo zinazokatwa zaid ya mara1 kwa kipato hichohicho? Kujiuzulu kwa spika bado hakujajibu hoja ya mikopo + tozo kwa wakati mmoja!!
 
Yaani unasukumwa na kufanyiwa visa ili uondoke alafu unaamua kuwaaga kwamba basi naondoka alafu utegemee kwamba watasema hapana usiondoke ?
 
1
Screenshot_20220108-110023.jpg
 
2.
KIFUPI SIO SAMIA WALA CCM.
wote hawamtaki ndugai.
IMEISHA HYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Screenshot_20220108-110044.jpg
 
Kukiri sio shida je amejibiwa?? Na nani anahusika kukubali kujiudhuru kwake
Simple tu, chochote atakacho mwenyekiti wao wengine wote lazima wafuate hata bila kujali kama kinavunja sheria.Wao ni kuimba tu wana imani na Samia...
 
Sisi ndo CCM tukikutaka unakaa,tusipokutaka unatembeaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kitu usichokijua huyo hajajiuzulu Bali kafukuzwa uspika na Samia.
Na ndo maana utashangaa Kuna watu wa CCM wakaanza kujifanya wanataka ndugai ajiuzulu kumbe tayari walijua HUKUMU IMESHAPITA.
mzanzibar Hana habari nae..
Kukiri sio shida je amejibiwa?? Na nani anahusika kukubali kujiudhuru kwake
 
Wajibu hoja hebu tulieni kabisa ili kuupa ubongo nafasi ya kutafakari Kwa kina bila kusukumwa na hasira au ukada!
Ndugai ni mkuu wa mhimili mmojawapo unaounda Dola na siyo mtu mdogo kihivyo, ni mkuu wa mhimili wenye mamlaka ya kuisimamia serikali yaani rais na baraza lake la uongozi. Ndiye anayemgawia serikali pesa za matumizi na kuzifuatilia zilivyotumika!
Ndugai ana watu wengi nyuma yake na baadhi Yao wapo ndani ya serikali na Hawa ndio wanaomshauri Nini Cha kusema au kufanya kwani yeye hashtakiki ndani ya JMT, ana kinga na haijafutwa.
Watu wake ni wabobezi wa siasa za bongo na ndio walioidraft Ile barua na Kwa vile wasomaji humu wanahemkwa wanashindwa kubaini makosa ya barua Ile kuadresiwa Kwa katibu wa chama badala ya katibu wa bunge na katibu wa chama kalivaa mazima bila kuiona mtego wa kisheria ambao utaibua mgogoro wa kikatiba na hapo ndipo mtakapobaini kuwa wanaomshauri bibi wanampotosha!
Ndugai anakwenda kubaki bungeni unless wale wababe wa Nape wawe wamemkaba!
Kikatiba na Kwa mujibu wa kanuni za bunge barua Ile haikutakiwa kwenda Kwa katibu wa chama na hapo ndipo ulipo ushindi wa Ndugai! Njooni mnishambulie ndugu wahemkwaji!
 
Kitu usichokijua huyo hajajiuzulu Bali kafukuzwa uspika na Samia.
Na ndo maana utashangaa Kuna watu wa CCM wakaanza kujifanya wanataka ndugai ajiuzulu kumbe tayari walijua HUKUMU IMESHAPITA.
mzanzibar Hana habari nae..
Hapo umenena vema sasa muhimili unafukuzwaje na muhimili mwingine
 
Simple tu, chochote atakaco mwenyekiti wao wengine wote lazima wafuate hata bila kujali kama kinavunja sheria.Wao ni kuimba tu wana imani na Samia...
Katiba katiba katiba

Mpyaaaaaaaaa
 
Ndio maana wengine tuna hofu asijekuwa ametishwa! Ni muhimu sana akaondolewa kwa utaratibu kinyume na hapo siku moja tutavuna hii mbegu mbaya kabisa inayopandwa.

Ndio sikubaliani na mambo mengi ya Ndugai lakini hapa simuangilii mtu anayeitwa Ndugai bali Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

CCM mlishiriki kupigania uhuru na sasa mnaelekea kupigana vita nyingine ya kuturudisha utumwani kwa mlango mwingine.
 
Aliyemteua kuwa kiongozi wa huo muhimili ni Nani?
au umeshasahau kuwa Samia ndo kapeleka jina la ndugai bungeni?
Sasa mtu aliyekuchagua anashindwa vipi kukutoa?
Uwa mnadanganywa tu Kuna mihimili 3 Ila kiukweli upo muhimili 1unaobeba hyo 2 iliyobakia.
Rais ndo KUSEMA
Hapo umenena vema sasa muhimili unafukuzwaje na muhimili mwingine
 
Katibu wa bunge amekiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM. Hii maana yake CCM iko juu ya bunge ndio maana Ndugai baada ya kusutwa kule ikulu na mwenyekiti wake akaamua kujiuzulu.

Hapa naona hata kama taratibu hazikufuatwa, lakini kwasababu ya "uchama" uliotawala vichwa vyao, hili jambo kuna uwezekano mkubwa likaachwa lipite kimya kimya kwasababu ya mazoea.
Kama hili litapita kimya nitakubali CCM imechoka kwa kiwango ambacho hatukuwahi kufikiri.
 
Ndugai mwenyewe asingeweza kujiuzulu.
Hukumu imepita kutoka JUU.
kwa kumlindia HESHIMA yake ndo wamemwambia aandike barua.
Watu wanasahau kuwa ndugai anaripoti CCM sio serikalini.
Yaani CCM Wana madaraka makubwa kushinda serikali.ndo maana barua imeenda kwa katibu mkuu wa CCM kwanza.na Mambo yamekubalika.
Baba jeni bye bye
Ndio maana wengine tuna hofu asijekuwa ametishwa! Ni muhimu sana akaondolewa kwa utaratibu kinyume na hapo siku moja tutavuna hii mbegu mbaya kabisa inayopandwa.

Ndio sikubaliani na mambo mengi ya Ndugai lakini hapa simuangilii mtu anayeitwa Ndugai bali Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

CCM mlishiriki kupigania uhuru na sasa mnaelekea kupigana vita nyingine ya kuturudisha utumwani kwa mlango mwingine.
 
Aliyemteua kuwa kiongozi wa huo muhimili ni Nani?
au umeshasahau kuwa Samia ndo kapeleka jina la ndugai bungeni?
Sasa mtu aliyekuchagua anashindwa vipi kukutoa?
Uwa mnadanganywa tu Kuna mihimili 3 Ila kiukweli upo muhimili 1unaobeba hyo 2 iliyobakia.
Rais ndo KUSEMA
"Mjingawewe" unasahau kuwa hata majaji/CAG wanateuliwa na Rais ila hana mamlaka ya kuwafukuza?
 
Nauliza tu maana bila kuambiwa kama amekubaliwa kujiuzulu anaweza kutengua barua hiyo na hakutakuwa na la kumfanya. Unapojiuzulu mamlaka unayowajibika kwake inatakiwa iseme imekubali. Hii ndio sababu wakati mwingine mtu anaweza kukataliwa kujiuzulu (mifano ipo mingi).

Taarifa ya Katibu wa Bunge kuwa kapokda taarifa kutoka Katibu Mkuu wa CCM kuwa chama hicho kimeridhia ni potosí nq inabeba makosa ya kiutendaji. Hakujafanyika kikao chochote cha KK ya CCM kujadili tukio hilo. Haiwezekani KM akubali kujiuzulu kwa Spika.

Vipi kama Spika Ndugai ALISHIKIWA BUNDUKI na kulazimishwa kuandika barua hiyo (under duress) kutokana na sauti za kumtaka kujiuzulu? Yaani CCM haikuchukua hata dakika moja kumuuliza kana "hiari" ni "hiari" kweli.

Kujiuzulu kwa Spika hakuwezi kufanywa kiholela hivi kana kwamba aliyejiuzulu ni mpishi wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkata...

Kinyume na wengine.. sijui kama Spika amejiuzulu kweli... ndio ufyatu wenyewe huu.

Kweli aende lakini aende kiukweli...akiibuka na kusema ametishiwa maisha... ? Yaani hata kukutana na KM hakujafanyika tunakubali tu?

Acheni ufyatu!!!
Ndugai hajajiuzulu , ametimuliwa
 
Hapana Sasa hivi CCM ndo imeanza kupata nguvu.
CCM ilichoka kipindi Cha magufuli.
WATU waliuliwa,walikamatwa,kuteswa, kufilisiwa n.k
Ila huyo spika wa bunge alikaa kimya

Back
Top Bottom