Nani anabisha kuwa kupambana hadi ushindi wa Yanga SC jana kulichangiwa na kubezwa mno na mashabiki wa Simba SC?

Kwa lugha nyingine ni kwamba badala ya kutushangaa na kututukana hadi kutudhihaki watu wa Simba SC GENTAMYCINE nikiwa kinara wao hapa JamiiForums, basi mngetupongeza! Kwani kwa 60% tumechangia kuwajaza ndimu (upepo) wachezaji wenu na wao kuamua kujitoa vile mpaka kushinda na kutinga makundi CAFCC.

Hivi mnadhani kweli GENTAMYCINE nisingekuwa nawacheka Yanga SC, nawatania hadi kuwakera huku muda mwingi nikiwasakama akina Rais Injinia Hersi Said na Msemaji Ally Kamwe wangeweza kujaa upepo na kujitoa kwa ajili ya timu?

Na kila wakikutana na wachezaji wa Yanga SC huwajaza ndimu (hasira), hali ambayo imekuwa ni kichocheo kikuu kwa wao kujituma kule na kuipambania jezi ya Yanga SC na bendera ya nchi (Tanzania).

Nasubiri sasa pongezi zenu nyingi tu kwangu kwani kuwasema kwangu nina uhakika kumechangia wachezaji wenu wote kuipambania timu hadi jana mkashinda vile, japo kwa ushindi kiduchu na wa kubahatisha kutokana na uzembe wa kipa wa Club Africaine ya nchini Tunisia.
Saa 7 mchana wa leo uende kuwapokea wananchi! Siyo unabwekabweka tu na kuweweseka humu kuhusu Yanga.
 
Mbumbumbu sisi hatushindi kwa maneno yenu hii spirit ya ushindi ipo kwa kila mwanayanga na ndio maana huku bongo hakuna anaeweza kutufunga

Hiyo spirit ilikuwa wapi hadi mkafurushwa CAFCL??acha kubwabwaja mkuu
 
Hamna kitu kama hicho, yaani mnataka mjishikize kwenye ushindi wetu. Hatutaki, nyie komaeni mtoe draw na ihefu.

Ushindi wa yanga hauihusu simba ni mipango kabambe na ya akili kubwa. Hata Al hilal walishinda kwa bahati tu ila kimchezo tuliwazidi sana.

Ko na nyie mlishinda kwa bahati??hakuna bahati kwenye soka its either umefanya kosa au umecheza chini ya kiwango..bahati ni kwenye kubet tu sio kwenye soka
 
Kama kubeti ni bahati basi na mpria ni bahati. Bahati ipo kotekote.
 
Ina maana yanga haina malengo Bali inafuata upepo unavumia wapi? Usajili mkubwa wote uliofanyika Kasi kuelekea mfumo wa mabadiliko ambao Jirani alianza na sasa kaachwa Mbali vyote hivi ni bure ila kejeli za Jirani ndiyo kichocheo hapo una potosha umma, ni mipango mikakati, malengo waliojiwekea, umoja na mshikamano, uongozi madhubuti chini ya rais hersi na bench la ufundi bora kabisa kwa sasa hapa Tz ndiyo chachu
 
Kwa lugha nyingine ni kwamba badala ya kutushangaa na kututukana hadi kutudhihaki watu wa Simba SC GENTAMYCINE nikiwa kinara wao hapa JamiiForums, basi mngetupongeza! Kwani kwa 60% tumechangia kuwajaza ndimu (upepo) wachezaji wenu na wao kuamua kujitoa vile mpaka kushinda na kutinga makundi CAFCC.

Hivi mnadhani kweli GENTAMYCINE nisingekuwa nawacheka Yanga SC, nawatania hadi kuwakera huku muda mwingi nikiwasakama akina Rais Injinia Hersi Said na Msemaji Ally Kamwe wangeweza kujaa upepo na kujitoa kwa ajili ya timu?

Na kila wakikutana na wachezaji wa Yanga SC huwajaza ndimu (hasira), hali ambayo imekuwa ni kichocheo kikuu kwa wao kujituma kule na kuipambania jezi ya Yanga SC na bendera ya nchi (Tanzania).

Nasubiri sasa pongezi zenu nyingi tu kwangu kwani kuwasema kwangu nina uhakika kumechangia wachezaji wenu wote kuipambania timu hadi jana mkashinda vile, japo kwa ushindi kiduchu na wa kubahatisha kutokana na uzembe wa kipa wa Club Africaine ya nchini Tunisia.
We miss you Genta hasa kipindi hiki Madame kamwaga mwanyanga njoo hata na ile ID yako ya Might Fighter
 
Back
Top Bottom