Nani anafaa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu baada ya Zuhura Yunus kuondolewa?

Nani anafaa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu baada ya Zuhura Yunus kuondolewa?

Nyerere alisema.
Ikulu sio mahali pakufanyia biashara!
Ikulu sio mahali pa kuuzia vitu.
Ikulu papewe heshima inayostahili.
Hatuwezi kumuweka Mwinjaku pale, wahindi watamtumia Kama daraja Kama sio mlango.
 
Umeandika vichekesho km jina lako kwa hiyo kweli hao wajinga jinga ndo wakae ikulu 😭nitaamini kweli tanzania ni stesheni ya vituko huko mbinguni...
 
Kwa maoni yangu, hulka ya huyu mama yetu kipenzi inaendana na Maulid Kitenge au Mwijaku. Amteue mmoja kati ya hawa vijana kuja kuchukua kitengo.

Haya ni maoni yangu japo sipendezwi na mambo yao lakini naona wanaendana na falsafa za mama yetu kipenzi.
wapo watu wenye taaluma hiyo na hawavumu lakini wamo wana utulivu wa akili. Sasa hawa wanavuma sana hasa kwa uchawa wao ya nini kupendekeza wapuuzi hao kwenda ikulu? Hao mavuvuzela labda yakawe simba na yanga huko yatafaa kwenda kuongoza idara za habari za timu hizo zenye utani wa jadi, sio ikulu, ikulu ni sehemu takatifu hakuna mizaha huko
 
Mwinjaku anafaa zaidi, ni msomi, mpenda maendeleo, haropoki, ana grorofa la mfano ambalo siku za nyuma alishatuonyesha,siyo chawa.
 
Kwa maoni yangu, hulka ya huyu mama yetu kipenzi inaendana na Maulid Kitenge au Mwijaku. Amteue mmoja kati ya hawa vijana kuja kuchukua kitengo.

Haya ni maoni yangu japo sipendezwi na mambo yao lakini naona wanaendana na falsafa za mama yetu kipenzi.
Huna kazi wewe.
 
Hebu acheni kuidharau serekali kiasi hicho. Au mnafikiri hamuwezi kudakwa na huu ujinga wenu
 
Habari wakuu,

Kufuatia kuondolewa kwa Zuhura Yunus kama Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, nani anaweza kuwa mrithi sahihi wa nafasi hiyo?

NB:
Hii sio mara ya kwanza kwa wana JF kufanya utabiri hapa jukwaani!

Back
Top Bottom