Kwa wasio fahamu Ndugai alikuwa mtu muhimu sana kwa maslai mapana ya taifa na mbunge mmoja mmoja hakika walimpenda.
Pili ukiachia yeye kama yeye kuomba msamaha kauli yake au alichoongea Ndugai hakina ubaya wowote kwa wabunge na wananchi wa kawaida hata vyama pinzani, hivyo wabunge ambao siyo mawaziri wanaweza kuwa upande wa Ndugai. Na wabunge ambao mawaziri hawa watakuwa kimya kwa sababu ya kulinda uwaziri wao.
Lingine kupata spika mpya wa awamu mpya huwa kunakuwa na mikiki mikiki mingi sasa kupata Spika wa kuokota dodo katika msufi lazima kutatokea heka heka.
Lingine karibu wabunge wote ni ngumu wakajizungumzia kufika pale bila kumtaja Magufuli, kwani kuna wabunge wengi hata awakustahili na hawakuwa na sifa ya kuingia bungeni lakini kupitia Magu waliingia na hawa bado hawana mahaba na mama kivile wenyewe wanamahaba na mzimu.
Hapa swali la kujiuliza wote ni kuwa hivi ni kweli mizimu ipo au haipo inanguvu au haina nguvu? maana kanisani na msikitini wanakataa lakini dodoma itasema.