naomba ushuhuda wa jambo moja ulilojibiwa na hiyo sala tafadhali.
Mkuu, unahitaji Ushuhuda wa Majibu ya Novena ya Mt. RITHA WA KASHIA...
Naomba, nishuhudie aliyonitendea mimi binafsi, na ingewezekana pia ungepata shuhudiwa na wale wanaonifahamu.
Kwa Ufupi.
Ipo, hivi nilikuwa na changamoto ya uvimbe ambao ulinisumbua kwa miaka kadhaa, na sio siri wengi wa wanaonizunguka/wanaonifahamu walikuwa wanauona na kwa kipindi chote ilikuwa ni changamoto kuutoa au kufanyiwa upasuaji.
Pindi, niliponuia na kuanza kusali Novena ya Mt. Ritha wa Kashia nilipata msukumo wa ajabu na kurudi Hospitali ambapo huwezi amini kwa taratibu za ile hospitali (ni moja ya Hospitali kubwa hapa nchini) ingeweza chukua zaidi ya miezi na miezi hadi upasuaji ila ndani ya mwezi 01, kwa jinsi operation ilivyokimbizwa hadi kupatiwa booking ya kwenda theater ni muujiza ambao ninaweza kuandikia story yake nyingine.
Ila kwa ufupi nimefanikiwa kufanyiwa upasuaji na sasa ninaendelea kurecover vizuri kabisa, Mimi ni ushuhuda wa majibu chanya ya Novena ya Mt. RITHA WA KASHIA, hapa nimeandika kwa kifupi ila in between huo mwezi mmoja wa Matibabu kuna mengi yalikuwa yanatokea am sure bila ya usimamizi wa huyu Mama yasingeweza kutokea na kufanyika (kuna muda hadi Matabibu walikuwa wanashangaa kwa jinsi mambo yanavyoenda kipindi wakiwa wananihudumia).
Hitimisho.
Najua katika forum hii kuna watu wa imani mbalimbali pamoja na wale wasio na imani hivyo ni vyema kushikiria kill ambacho unakiamini na unatarajia kinakupeleka katika wokovu, kwangu mimi huyu Mama amekuwa msaada kwangu na nitaendelea kumkimbilia kwa mambo yote yalishindikana.
Nb. TUSIBEZE AU KUPUUZA NGUVU YA SALA.