Nani anafahamu jinsi ya kusali Novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia anisaidie?

Nani anafahamu jinsi ya kusali Novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia anisaidie?

Habari zenu watu wa Mungu,

Naomba mwenye kufahamu namna ya kusali/kufunga novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia anipe maelezo yake jinsi ya kufanya.

Natanguliza shukrani.
Nenda youtube marehemu mosinyori Mbiku kaifundisha vizuri mno. Ukikosea hupati matokeo
 
Tumsifu Yesu Kristoo...

Nawatakia kila la heri wote mtakaoweza kufunga..kuna group huko Telegram nimeungwa watu ni wengiiiii...

Mtakatifu Ritha wa Akashia utuombee
Naomba link ya ilo group kama hautojali.
 
Ndugu yangu mtoa mada, itoshe kusema umeuliza swali lako sehemu ya barini kuna maji ya chumvi, takataka, samaki na wadudu wa kila aina wanaojua, na wasiojua na wadhani wanajua nakadhalika. Hivyo tegemea kupata majawabu ya aina zote.

Tambua kuwa humu kuna imani na madhehebu tofauti ambayo yanavyo amini wanaona ni sawa kwao na wangetaka kila mtu aamini vile wanavyo amini. Wengine hawajui unalolitaka na hawajawahi sikia lakini watakujibu km vile wanalijua.
Hivyo naweza sema umeuliza swali kwenye wrong destination. Tafuta forums zenye mlengo sawa ili upate kusaidiwa, labda kama uliuliza kupima watu wana opinion gani na kitu unachotaka kufanya vinginevyo hutaweza pata substantial information you want.
 
Haya mambo niliona ni upuuzi nikaacha nakwenda kanisani kabisa, yaani unakaa unategemea binadamu mwenzako akusaidie ufanikishe mambo Yako ilihali yeye mwenyewe ameozea aridhini, Dini hizi zililetwa kutupumbaza akili tu na kutuongezea umasikini, ulaya watu wanachangishana pesa wanajenga shule full equipped, watoto wao wanapata maarifa ya kupambana na maisha, sisi tunachangishana pesa kujenga mikanisa mikubwa tunaenda kuimba litania ya Lita na Maria, na kunywa maji ya upako Ili tupate maisha mazuri
Wasiwasi ndiyo akili, Mungu hakusema tukae tu bila kufanya kazi hapana. Vilevile wapumbavu hujisemea hakuna Mungu! (Zab 14:1). Hutapoteza chochote ukaamini kuwa Mungu yupo na ukamuabudu na ikafika mwisho ukaona hayupo, ila is very acute kujiaminisha kuwa kumwabudu Mungu ni upuuzi na ukafika mwisho ukuta yupo!
Kama uchawi upo na unafanya kazi basi tambua tu kuwa Mungu yupo na anafanya kazi. Utatafuta kila aina ya mali lakini atakapo kuhitaji utaenda tu. Tusijidanyanye jamani Mungu yupo!!
 
Habari zenu watu wa Mungu,

Naomba mwenye kufahamu namna ya kusali/kufunga novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia anipe maelezo yake jinsi ya kufanya.

Natanguliza shukrani.
Asante kwa kumalizia kwa shukurani.
Kama ukiweza kuweka huu uzi basi ungeweza pia kuGoogle na ukapata jawabu! Jiongeze.
 
Halafu jamani kwanini kama kitu mtu hukijui au huna jibu usikae tu kimya?matusi, kejeli, dharau kwa imani za watu wengine ni ya nini?Kama imani yako haiko kwenye imani za wengine kwanini uone wanakosea?
Kila mtu ana namna yake ya kumuomba Mungu ili afanikishiwe mambo yake au amshukuru Mungu.
Tusiwe hivi jamani tujitahidi kuwa wavumilivu wa imani za wenzetu na huo ndo ukomavu wa kiroho.
 
Back
Top Bottom