Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

As for me nakataa ila sikulazimishi uamini!

Hao unaoona wanakusanya watu kuna cha ziada wanachotumia siyo nguvu ya neno la Mungu,(japo neno la Mungu linatenda kwa wale wanaoihubiri kweli).

Manabii enzi za mababu wa imani walikuwa wanatumwa kuwakumbusha watu umuhimu wa kumrudia Mungu na kutenda mema ila hawa wa kisasa hawasemi hayo wao wanawaambia watu watafute hela haijalishi wataiba au wataloga na kwamba hakuna aliyezaliwa awe maskini,au kuwaahidi watu watamiliki magari nyumba nzuri etc vitu ambavyo haviwasaidii chochote kwenye ulimwengu wa kiroho.

Kila mtu amewekewa na Mungu uwezo wa kupambana kiimani na yanayomsibu kama umaskini mapepo etc siyo lazima kwenda kwa hao popoma,na mpaka watu waje kustuka kwamba jamaa ni wapigaji watakuwa wameng'atwa sana.
Shetani utenda miujiza ikiwemo uponyaji pia kwa magonjwa ya kiroho Mungu utenda miujiza pia inategemea na huyo nabii upande aliopo sisi tunawatambua kupitia maandiko.
Utoaji Kama ni wa kiibada hakuna shida.
Ndo maana unaambiwa shika Iman kwa akili ukiyachunguza maandiko,Hawa mitume na manabii wa uongo hawali pesa yako.
 
Nadhani unaongelea manabii wa uongo.Manabii wa kweli wanatenda miujiza.
Umasikini ni laana
Nimekwambiajee!hao watu hawapo hao unaowaona ni wevi na matapeli wanasukumwa na njaa zao but still sikulazimishi uamini haya as long as umeamua uwaamini!!!

Hakuna asiyependa kuona miujiza mimi nataka hao unaosema wanatenda miujiza niwapelekee mimi mlemavu ninaemjua wakanitendee muujiza kwa kumfanya atembee magongo ayatupe,wenye matatizo wapo wagonjwa wapo matajiri wapo ili kulinganiana duniani haiwezekani wote tuwe Mabahkresa au tuwe Matonya au tuwe wazima au tuwe wagonjwa tupo hivi ili kila mmoja wetu kupitia sisi wenyewe kwa matendo tutakayotendeana kama ni kwa mzima dhidi ya mgonjwa au tajiri dhidi ya maskini tuweze kumfikia Mungu.

Kila kitu duniani kinaenda kwa process anzia hatua moja,mbili tatu so on,mfano mimi nyumba ninayoishi nimeijenga miaka nane kwa jasho na damu sasa sitakuelewa leo atokee tu mwendawazimu ajiite nabii sijui mtume aniambie nitapata nyumba au gari,au mke or chochote kile kwa kwenda kuwekewa mikono na yeye huku sijafanya process yoyote eg,sijafanya kazi kwa bidii,sijatoa sadaka kwa moyo (sadaka siyo nimpe yeye,ni yeye anifundishe nikampe nani na nani,wapo walemavu na wasiojiweza mbalimbali wanahitaji kusaidiwa),unfortunately hatanifundisha haya atataka nitoe sadaka zaidi na zaidi nimpe yeye huku nje ame-park Hummer au Vogue na anaishi kwenye nyumba nzuri ishara ameshafanikiwa but still anashindwa kunifundisha nikawape na wengine ambao hawaijui kula yao ya leo.

Siku ukimuona nabii au mtume anatumia sehemu ya ibada yake kwa 75% kukukataza uache uzinzi,uache wizi,ukitoka hapo Kanisani kwake uende ukawasaidie wasiojiweza,sali kwa ajili ya wengine wanaoteseka kwa maradhi mbalimbali,akikusisitiza kafanye kazi kwa jasho ili ununue gari ujenge nyumba,jenga nidhamu na jamii upate connection upewe deal na mengineyo na siyo usubiri akuwekee yeye mikono huku akikuuzia maji ya upako ili ukafanikiwe rudi hapa uone nitaipokeaje hoja yako ila kwa hawa wa sasa,sahau hao ni wenye njaa waliojiongeza!!!
 
Unafadhiri = unafadhili. Kajifunze kwanza kuandika wewe chawa wa Kapola.
Hujielewi tu usicholewa nini hapo mpuuzi tu wewe unazani kila mtu chawa, chawa ni nyie msio kuelewa na kujitambua
 
Kwanini umuongelee Mtumishi ambaye hujui mkataba wake na Mungu? Unajua wito wake? Kama Mungu anataka awe hivyo kila mtu alisikie neno kupitia yeye! Eshimuni kazi na wito wa mtu unazani nyie mnajua zaidi yake mwenye wito?
 
Huyo pastor Tony ni mwembamba sijui hali ,ana mwili mdogo kama yule tapeli Ontario aliyekusanya Kijiji humu jf akawapiga hela kwenye forex [emoji23][emoji23]..
 
Haya makanisa kama huna msimamo familia itayumba sana. Yupo jamaa Mkatoliki mwenzangu alishawishiwa na mkewe waende kwa mzee wa yesu Boko.

Tupo masanga jamaa ananisimulia kesho yake anaenda. Nikamshauri asicheze na imani atulie. Akaamua kwenda na familia nzima ( kuna changamoto alikuwa anapitia). Alichokutana nacho kule hakuna tofauti na uganga. Hakurudi tena, mkewe aliendelea kwenda huko baadae akagundua kinachoendelea akapakimbia.

Wakiwa hawaja settle kipindi hicho "nabii" shilah amepamba moto anapewa airtime na clouds kupitia akina Jimmy na Samsasali mkewe akavutiwa na miujiza na zile shuhuda akataka kubeba mdogo wake wa kike ampeleke kwa maombi.

Jamaa kwa experience ile ya mzee wa yesu akapiga marufuku na mkwara mzito. Ugomvi ukawa mkubwa kuwa anapinga mambo ya wokovu! Muda umepita kidogo kashfa za huyo nabii zikaanza kutoka hasa ulaghai wa kingono na miujiza fake. Yule mke wa jamaa alishukuru kutokwenda huko na sasa anapambana na rozari tu amechoka misele ya makanisa [emoji1787]
 
Kwanini umuongelee Mtumishi ambaye hujui mkataba wake na Mungu? Unajua wito wake? Kama Mungu anataka awe hivyo kila mtu alisikie neno kupitia yeye! Eshimuni kazi na wito wa mtu unazani nyie mnajua zaidi yake mwenye wito?
Acha upumbavu wewe chawa wa Kapola.
 
Eti " kwanini hahubiri mavazi"?....
Na we hapo unaona umeuliza swali la msingiiiiii baada ya kutafakari sanaaa??😀
Kama husikii Mungu akisema kupitia yeye,si ajabu yeye Sie aliekusudiwa uisikie sauti ya Mungu kupitia yeye.
So nenda na zingatia kule unakoisikia sauti ya Mungu na kuielewa.
 
Sasa mkuu kwenye bio yake ya Instagram ameandika Ms Cyber security Sasa inakuwaje baba mchungaji adanganye
Kasema hiyo Masters ya Cyber Security kaisomea chuo gani na mwaka gani? Au ni "honorary" maana siku hizi kila kitu kinawezekana 😁

Kutoka BA in Rural Development SUA kwenda kwenye Masters ya Cyber Security....

99.99% this is kamba as usual.....
 
Bro embu elaborate hapo kwenye sexual predator anafanya mambo ya mzee Robert kelly
Ni mambo ya aibu mkuu hata kuyaelezea. Ni mambo ambayo kama ndiyo binti yako ametendewa unaweza ukachukua bunduki na kwenda kummiminia risasi za kichwa mhusika mpaka magazine yote iishe!

Ila misukule yake huiambii kitu. Sijui wana nguvu gani hawa jamaa aisee. Yaani ukiingia kwenye anga zao akili zote na lojiki vinakaa pembeni hata uwe una Ph.D.

Fikiria hawa "waliouliwa" na Mackenzie wa Kenya. Wengine ni wasomi kabisa lakini waliaminishwa kufunga mpaka kufa ili wakaonane na Bwana. Unajua njaa inavyouma? Ndiyo huli kwa makusudi tu mpaka internal organs zinaanza ku-shut down one by one lakini umekomaa tu. Imagine waliookolewa bado walikuwa wanakataa kula ili waumalize mwendo waende kwa Yesu.

Waogope sana hawa watu...na siku ukibahatika kuchomoka ndiyo unajiona jinsi ulivyokuwa mjinga wakati wenyewe walishahamia kusaka victims wengine.

Sema uzuri wengi wa watumishi wa aina hii mwisho wao huwa siyo mzuri pia maana Mungu naye huwa hadhihakiwi. Hushughulika nao hatimaye!
 
Huyo pastor Tony ni mwembamba sijui hali ,ana mwili mdogo kama yule tapeli Ontario aliyekusanya Kijiji humu jf akawapiga hela kwenye forex [emoji23][emoji23]..
Hahah umenikumbusha 2017 Ontario kipindi hicho wa moto sana humu aliwapiga umeme watu na elimu zao akawaachia maumivu makali.

Yule jamaa aliondoka na kijiji cha wasomi!
 
Tapeli sio tapeli, wenzetu wanapiga Ela kina zumarindi sio tuna wadis tu.
 

Halafu serikali ipo inamwangalia mtu kama huyu? Siku akiua watu ndiyo wanashtuka! Huyu ni mgonjwa wa akili na mahojiano yake na Millard Ayo wakati alipokwenda mbinguni ni uthibitisho tosha!

 
Back
Top Bottom