bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Shetani utenda miujiza ikiwemo uponyaji pia kwa magonjwa ya kiroho Mungu utenda miujiza pia inategemea na huyo nabii upande aliopo sisi tunawatambua kupitia maandiko.As for me nakataa ila sikulazimishi uamini!
Hao unaoona wanakusanya watu kuna cha ziada wanachotumia siyo nguvu ya neno la Mungu,(japo neno la Mungu linatenda kwa wale wanaoihubiri kweli).
Manabii enzi za mababu wa imani walikuwa wanatumwa kuwakumbusha watu umuhimu wa kumrudia Mungu na kutenda mema ila hawa wa kisasa hawasemi hayo wao wanawaambia watu watafute hela haijalishi wataiba au wataloga na kwamba hakuna aliyezaliwa awe maskini,au kuwaahidi watu watamiliki magari nyumba nzuri etc vitu ambavyo haviwasaidii chochote kwenye ulimwengu wa kiroho.
Kila mtu amewekewa na Mungu uwezo wa kupambana kiimani na yanayomsibu kama umaskini mapepo etc siyo lazima kwenda kwa hao popoma,na mpaka watu waje kustuka kwamba jamaa ni wapigaji watakuwa wameng'atwa sana.
Utoaji Kama ni wa kiibada hakuna shida.
Ndo maana unaambiwa shika Iman kwa akili ukiyachunguza maandiko,Hawa mitume na manabii wa uongo hawali pesa yako.