Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Nani anamuelewa Pastor Tony Kapola?

Nani anamfahamu vizuri pastor Tony kapola.

Kanisa lake liko wapi ?
Nilisikia liko morogoro kutwa yupo Dar,dodoma

Kwanini waumini wake na mke wanavaa nguo za ovyo ?

Inakuaje ameungana na hawa manabii wa uongo matapeli wa zimbabwe ?
Weka picha
 
Ulisomea wapi kupima uwezo wangu? Ungekuwa una akili usingeleta ukosoaji wako wa kipuuzi kwa jambo ambalo halihitaji ubishi. Kwa mfano nikikuona wewe Joanah umechoka nikakuuliza ukanipa sababu zako haitakiwi nikuamini? Hizo akili zako kawashauri serikali na wapinzani kuhusu bandari wasiendelee kulumbana.
Sipendi kabisa ligi na poor brain kama wewe,...Sikiliza we subiri kofia na t-shirt za CCM ukabishane majukwaani.
Nipishe mie
 
Ni kijana mpya katika huduma ya uinjilishaji, ila amekosa adabu na nidhamu katika kuvaa yeye na waumini wake wamekosa hekima ya kujisitiri ili kulinda ushuhuda wao
Exactly nimeliongelea hili Ila naona watu wananiambia nifuate neno lake mavazi hayanihusu.

Ina maana kadada kako uchi wa mnyama Sana,,,na kamstari kachupi kanaonekana halfu we umekomalia kusema nisiangalie Mavazi niangalie neno.
 
Hapana siamini katika hili mchunga kondoo hawezi kuwa hivyo matapeli tu hao sawa na dalali. Ila ukitaka mpata mhasibu, hata mwanafunzi primary wampata na mafunzo maalumu ndo maana mtoto darasa kwanza na chekechea hawafananani ila kwenye dini ambayo ni jambo kubwa watu twalinganisha kupitia idadi ya followers nadhani tuanzie hapo
Unamtetea kwa kigezo kipi mkuu.
 
Ni mambo ya aibu mkuu hata kuyaelezea. Ni mambo ambayo kama ndiyo binti yako ametendewa unaweza ukachukua bunduki na kwenda kummiminia risasi za kichwa mhusika mpaka magazine yote iishe!

Ila misukule yake huiambii kitu. Sijui wana nguvu gani hawa jamaa aisee. Yaani ukiingia kwenye anga zao akili zote na lojiki vinakaa pembeni hata uwe una Ph.D.

Fikiria hawa "waliouliwa" na Mackenzie wa Kenya. Wengine ni wasomi kabisa lakini waliaminishwa kufunga mpaka kufa ili wakaonane na Bwana. Unajua njaa inavyouma? Ndiyo huli kwa makusudi tu mpaka internal organs zinaanza ku-shut down one by one lakini umekomaa tu. Imagine waliookolewa bado walikuwa wanakataa kula ili waumalize mwendo waende kwa Yesu.

Waogope sana hawa watu...na siku ukibahatika kuchomoka ndiyo unajiona jinsi ulivyokuwa mjinga wakati wenyewe walishahamia kusaka victims wengine.

Sema uzuri wengi wa watumishi wa aina hii mwisho wao huwa siyo mzuri pia maana Mungu naye huwa hadhihakiwi. Hushughulika nao hatimaye!
Watu.wachache watakuelewa kaka
 
Eti " kwanini hahubiri mavazi"?....
Na we hapo unaona umeuliza swali la msingiiiiii baada ya kutafakari sanaaa??😀
Kama husikii Mungu akisema kupitia yeye,si ajabu yeye Sie aliekusudiwa uisikie sauti ya Mungu kupitia yeye.
So nenda na zingatia kule unakoisikia sauti ya Mungu na kuielewa.
Unaongea upumbavu
 
Soma vizuri matendo 5:1-16
Ile Sadaka ilikuwa akabidhiwe mtume Petro,wao wakacheat,wakatoa nyingine wakaibana,kilichofuatia ulikuwa ni msiba...
Sasa endelea kuficha Sadaka[emoji851]
Sio mtume Petro, Kanisa liliamua kuishi kiushirika! Narudia tena ni Kanisa sio amri ya Petro ingawa ndio alikuwa mkuu wa Kanisa.

Vyote vilivyopatikana walivitumia kwa ushirika sio Mitume kujinufaisha kwa ufahari! Siku hizi injili inatumika kama fursa kiuchumi! Wanatumia mistari kuhalalisha hilo. Wanasema imeandikwa watumishi watakula madhabahuni lakini wao wanasaza madhabahuni.

Tunafikiri ni kama waajiriwa wa Mungu na tunastahili mapato hasa utajiri! Kibali cha kumtumikia Mungu ni neema ya kutetemekea! Hatuna mastahili hata ya kulitamka jina lake. Tutumie hizo huduma kuvuta watu kwa Kristo sio kuwavuta kwenye Makanisa yetu tuvune sadaka!

Ipo siku ambayo kila mmoja wetu itamjia ghafla na tutajibu mbele ya kiti cha hukumu. Ni bora ufanye mambo yako mengine kuliko kutumia injili kuvuna wakati tumepewa vipawa bure! Tunadai mishahara kwenye professional zetu sababu tulilipia gharama kujua! Vipawa tunapewa bure, tuvitumie bure!
 
Anaitwa Antony Kapola
Ana Masters ya Cyber security

Mkewe ana PhD.

Ana kanisa lake Morogoro ndiyo. Ila ana semina karibia Mikoa mingi. Kote huko ulipopataja. Halazimiki kubaki hapo Morogoro

Kanisa lake lipo chini ya Ministry ya Eubert Angel, huyo nabii anaiyemuita baba.

Unaweza kumtafsiri Eubert kama tapeli, ila taifa lake linamuona wa maana. Anasaidia kupooza makali ya vikwazo vya kiuchumi.
Eubert Angel ni baba wa Major one, bushir hapo tayari jibu unalo ni watu wa namna Gani hawa
 
Back
Top Bottom