Nani anatoa fedha za miradi, Rais au Serikali kutokana na bajeti yake?

Nani anatoa fedha za miradi, Rais au Serikali kutokana na bajeti yake?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Mara nyingi nimewasikia viongozi mba;i mbali mfano Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi Watendaji na wengine wengi wakisema tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutoa mabilioni kadhaa katika mradi fulani. Naomba mnielemishe.

Je, ni Mhe. Rais ndiye anayetoa fedha za miradi yote kutoka mfukoni mwake au fedha za miradi zinatokana na bajeti ya Serikali na mikopo mbalimbali.
 
Usipate tabu! ukisikia kutetea ugali ndio huko. Hii nchi unakuta mtu mzima na akili yake timamu lakini anajifanya hana akili!
Harafu hii lugha ya mama, kila kitu mama inakera.

Utaona mtu mzima mwanaume ana umri mkubwa kuliko huyo mama ,utasikia mama anatujari sana.
 
Nimeshukuru kwa mawazo yenu hasa NGOSWE2. Kumbe hela siyo za kwake ila kuna watu wanataka upendeleo wa vyeo.
Hela sio zake ila anauwezo wa kusema hizi msitoe hizi toeni. Means ni zake Shangaa apo sasa.
 
Umeorodhesha wateule(appointed) wa Rais hivyo wameteuliwa kwa lengo la kumsaidia na kuonesha(signal) uwepo wa rais hivyo si vibaya kupongeza au kumtaja rais kama mtoa hadhina pia jengne kuna sheria za bajeti/fedha ila rais anayomamlaka ya kuomb fedha zipelekwe mahala fulani kwa haraka..yey ndye kila kitu.
 
Rais ana mahela mengi sana mfukoni mwake hivyo akijisikia kutoa anachota anawapa mfanye ufisadi.
 
Ni Rahisi, yaani yeye akikataa hamuna kitu kinajiendea.
 
Back
Top Bottom