Nani anaweza kutupa historia ya pesa?

Mugabe hata kama asingewekewa vikwazo angeprint pesa nyingi na kuziweka kwenye mzunguko matokeo yake ni yaleyale tu hyperinflation basi

Kimsingi yeye aliprint pesa nyingi zaidi ili kujikwamua toka kwenye vikwazo.

Umoja wa Ulaya leo hii mbali na Sarafu yao kutumika Ulimwenguni kote kama na wao watathubutu kuziprint pasina kuzingatia uhitaji wa sarafu yao sokoni hatma itakayowakuti ni kama ile ya Zimbabwe 'Hyperinflation'

Ndugu yangu, haijalishi nani anaongoza Uchumi wa dunia au nani kaungana na nani au nani anashirikiana na nani kiuchumi Athari ya kuprint pesa nyingi kuliko uhitaji ma kuziingiza kwenye mzunguko ni moja tu, Awe Ujerumani, awe Uchina, awe Kuwait au awe Marekani athari ni 'Hyperinflation'

Ndio maana wapo makini kuhakikisha wanadhibiti kiasi cha Inflation kwenye nchi zao

Ama kuhusu Sanctions (this is my fav subject[emoji23])
Tujaalie Afrika imeungana (AU) kama ilivyo Umoja wa Ulaya (EU), kisha ikatokea EU ikawa ndio mshirika mkubwa wa kiuchumi wa AU na wakapishana sera ikatokea EU wakawawekea vikwazo AU..... Hapa moja kwa moja AU itaathirika zaidi na vikwazo hivyo.

Kwa maneno mengine:
EU leo hii wakiwekewa Sanctions na Uchina wataathirika sana kwakuwa Uchina hivi sasa ndiye Patner mkubwa wa EU kwenye biashara mathalani kwa mwaka ulopita Uchina ilifanya biashara yenye thamani ya zaidi ya Euro Bilioni 586 ikifuatiwa na Marekani na mataifa mengine.

Hivyo basi hata EU wanaathirika na vikwazo, hakuna aliye salama.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
swali moja tu nakuuliza, hili swali huwa nikiuliza watu wanalikimbia, unasema hakuna nchi ambayo iko safe, kwamba nchi yoyote iki print Zaidi ya uhitaji inapata hyper inflation, lets say marekani pesa yao inatumika dunia nzima, kwa maana ya kwamba dolla ndio pesa pekee inayoweza ku back gold, na dollar ndo pesa pekee inayoweza kununua kitu chochote duniani, lets say, marekani kwa siri wame print pesa nyingi kuliko uhitaji, it means ile hela aliyo print sio lazima aiweke kwenye uchumi wake wa ndani, anaweza kutoka nje ya nchi na akanunua chochote anachotaka. hapo hakuna inflation kwa marekani, tatizo la marekani sio pesa bali vitu tangible, na tatizo la afrika ni pesa ila tuna kila kitu tangible, ok je kwa mtindo huu marekani ina weza kupata hyper inflation?

then lets say, marekani ni extension ya ulaya, na kila anacho gain marekani kupitia huo mfumo, na nchi za ulaya zina gain, so je ulaya wanaweza kupata hyper inflation?
 
Kama ndivyo ulivyomaanisha Mkuu,
Nadhani una Overestimate nguvu ya Marekani na EU na ni sawa kusema umechepuka kutoka kwenye uhalisia wa namna Ulimwengu unavyoenda,

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
how nifundishe, tuko hapa kuelimishana, ukitoa statement ya kupinga, pia toa na fact za kuitetea statement yako. umesema nimechepuka na uhalisia, unaweza kuelezea huo uhalisia
 
[emoji23][emoji23][emoji23] '....uhitaji...'
Yes Pesa ya Marekani inatumik Ulimwenguni na kwa sasa wanaizailisha kulingana na uhitaji wake ULIMWENGUNI KOTE.

Kama watizalisha kushinda uhitaji wake wa ndani na ziada wakaisukuma kwenye Mzunguko wa kidunia BILA KUZIDI mahitaji yake ya kidunia bila shaka hakutakuwa na hyperinflation Marekani wala Uchumi wa Dunia hautayumba.

Pia, kama watazalisha kupita uhitaji wake ndani ya Marekani na wakaisukumu kwenye mzunguko wa kidunia nako ikazidi UHITAJI WAKE KIDUNIA bila shaka Marekani itakumbwa na Hyperinflation huku Uchumi wa dunia ukitetereka. Hilo halina shaka.

Suala ni kwamba Marekani ana Advantage na huu mfumo wa fedha lakini haina maana anaweza fanya chochote bila ya kujiathiri, Uchumi wake uko kwenye hatari pia kama atashindwa kumaintain na kusatisfy mahitaji ya Uchumi wa Dunia.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
how nifundishe, tuko hapa kuelimishana, ukitoa statement ya kupinga, pia toa na fact za kuitetea statement yako. umesema nimechepuka na uhalisia, unaweza kuelezea huo uhalisia
Nadhani unaamini kwamba Marekani ni superpower na anaweza fanya chochote anachojisikia.
Na Katika Imani yako unaona kwamba hakuna kitakchoikwamisha aidha EU au US kuendelea kufanikiwa kiuchumi kama ulivyosema kwa EU 'hakuna kitu sunctions'
hii si sawa.
(Tell me if am wrong)

Uhalisia wa kiulimwengu ni kwamba kuna kanuni ambazo kila mmoja anapaswa kufuata ili kufanikiwa, Haijalishi Superpower au la.
Mfano wa kanuni hizo ni Msingi wa mada yetu ambayo ni Sarafu, nilieleza awali ya kwamba Thamani ya sarafu hutegemea Uhitaji wake ambao huenda sambamba na Bishara, Uwekezaji na Uzalishaji. Kanuni hii haina EXCEPTION yeyote atakaeikiuka atapatwa na athari hata kiwa EU au Marekani hata Zimbabwe ya bila vikwazo na hata Korea Kaskazini.

Sijui umenipata vyema?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Na kwa lengo la kielimu tu waweza tuambia Marekani ina Uhitaji na vitu gani Tangiable ambavyo haina? na nchi za kiafrika ina shida na pesa gani ambazo hazina?


Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Usisahau ulaya ndio baba mlezi wa marekani. Ulaya ina control marekani. Unajua wazungu wajanja sana. Wanathamini utaifa kuliko nchi. Ndo story alitaka kuwaletwa na trump. Trump alikua anapigania nchi ya marekani ambayo ina race zote. Ila biden anapigania taifa la wazungu. So when it comes to state issue. Wala jamaa hawana masihara. Ndo maana unaona mzungu yoyote katika kona yoyote ya dunia analindwa. There is no way wazungu wa south afrika watatolewa pale. Wanaback up ya ulaya na marekani combined.
Wanaishi kama state sio nchi. Ndo maana blacks na latino wataendelea kua watumwa ndani ya marekani. Sababu wao wanahisi nchi yao inawapenda. Lakini marekani inaongozwa na wanaotumikia state sio country.
 
Sawa Mkuu,
unasema Ulaya inaidhibiti Marekani, waweza fafanua ni kwa namna gani?

Na pia unaelezeaje suala la Trump Kuongeza Ushuru kwa Chuma na Aluminium vinavyoingia Marekani ikijumuishwa na vile vinavyotoka Ulaya? (ilhali walikua na makubalino ya kuondoa ushuru ili kusisimua biashara miongoni mwao)

Unalizungumziaje suala la Trump kukataa kuiweka EU katika orodha ya ambao hawalipi kodi katika miamala ya kibiashara (exemption from Tariffs)?

Unalizungumzuaje suala la Trump kuongeza Ushuru kwa zao la Zaituni toka Uhispania (EU) mwaka 2018?

Unalizungumziaje suala la Marekani kutofautiana na 'Walezi' wake (kama unavyowaita) EU katika suala la JCPOA?

Unauzungumziaje Mtafaruku uliozuka ndani ya NATO hasa wakati wa Trump akilalamika ya kuwa US ananyonywa kwa kutumia pesa nyingi zaidi ndani ya NATO kuliko wengine?

Vipi kuhusu US kutishia kutoza Ushuru Magari yanayoingizwa Marekani toka Ulaya?

Vipi kuhusu suala ya US kujitoa kwenye Makubaliano ya Paris (wakati wa Trump) huku ikitofautiana sana na 'Walezi' wake EU?

Vipi kuhusu US kugomea mapendekezo ya EU katika maboresho ndani ya WTO katika kurahisisha Usuluhishi baina ya wanachama?

Tafadhali tupe Mwangaza...

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Hapo zamani mfumo uliokua ukitumika zaidi katika biashara Ulikua ni wa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa. Lakini kutokana na mapungufu ya mfumo huo ndipo ulipoibuka mfumo wa pesa (commodity money) ambapo bidhaa moja ilitumika.

Katika mfumo huu kila jamii ilitumia pesa ya aina tofauti kulingana na mazingira yao au level ya maendeleo iliyofikiwa na jamii hiyo, kuna waliotumia chumvi,sea shells,silver, gold n.k

Jamii zilizotumia Silver na Gold zilitangulia kuja na mfumo wa Coins. Zilitawala maeneo makubwa na hvyo kueneza mfumo huu wa kutumia coins. Na jamii nyingne zlizofanya biashara na jamii hizi ziliupokea mfumo huu.

Pesa za karatasi (noti) zilianza kama risiti, mtu alipoenda kuhifadhi vipande vya silver au Gold alipokea risiti kutoka kwa wahifadhi(benk). Hizi risiti zikawa zikitumika pamoja na Coins.

Mfumo wa pesa bado unaendelea kupiga hatua kama tunavyojua leo hii kuna pesa nyingi inayozunguka kielectronic kuliko coins na noti.
 
Nani ana control mfumo?
Hutaonekana kwenye hili swali, na kama ukionekana naomba jibu lako liwe honest
 

Sawa
 
Hii ni kweli kabisa. Inasemwa kuwa wanaexport inflation. Wanaprint mahela halafu yanaenda kuumiza vinchi vingine kabisa.
 
Waweza tueleza inafanyaje kazi Mkuu?
Yaani kivipi?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Ili kuelewa kinachozungumziwa jielimishe kwanza vitu vifuatavyo.
1. Jua uchumi ni nn
2. Ijue inflation ni nn
3. Jua basic history ya biashara
4. Fanya tafiti pesa imetoka vipi kuwa dhahabu mpaka kua dollar

Ukimaliza kuvielewa hivo. Ndo tunaweza kuwa kwenye page moja ya mazungumzo. Otherwise hutaelewa kinachozungumziwa.
 
Nafikiri ni Busara kwa wewe kujibu swali na si kuzua swali baada ya kuulizwa swali,

Ningelikua ni wewe ningejitahidi kujibu swali ningeeleza namna inavyofanya kazi kama mwenyewe ulipozungumza kuwa 'tupo hapa kuelimishana'

Tafadhali tueleze inafanyaje kazi?

Au swali ni gumu kiasi haiwezekani kuelezeka kuwa wanawezaje ku export inflation?
[emoji23][emoji23][emoji23]
Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…