KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Nani anayeihujumu TTCL kwa kiwango hiki?
Kuna mmbo fulani yanaendelea kwenye TTCL kiasi kwamba tunaona kama ni hujuma kwa TTCL:
Kwanza, kipindi kirefu sasa ukitafuta laini za TTCL kwa mawakala wanakuambia hamna. Ni kweli shirika likose laini ambazo kimsingi ndio mteja na ndio zitachochea usambaaji wa huduma kwa watu wengi?
Pili, laini ya TTCL kupatikana kwake ni mpaka uinunue kwa gharama ya shilingi 5000 mpaka 7000 na hii ni gharama ya maeneo mengi ya Dar es Salaam sijajua upatikanaji na gharama zake mikoani na huku laini za mitandao mengine ni bure kabisa na hadi kifurushi Cha kuanzia unawekewa tena bure. Kwa nini zipatikane kwa gharama hivi?
Tunasikia kila siku TTCL kupata hasara lakini kama mambo yenyewe ndio yako hivi basi hasara ni lazima.
Mitandao mingine ikitumia kila mbinu za kibiashara kuhakikisha zinakuwa na wateja wengi kwa kusambaza laini kwa wingi TTCL wako nyuma kwenye ushindani. Kiuhalisia kabisa, watu wengi sio rahisi kununua laini kwa gharama hiyo. Kama ni kuuza, ingeuzwa hata shilingi 1000.
Mhe. Samia na Waziri Nape tazameni hujuma hizi zinzofanywa dhidi ya TTCL na ikiwezekana libinafishwe tu ili liendeshwe kibiashara zaidi.