Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

Kwa hoja yako wakuregenzi hawapaswi kuwa maofisa wa tume ya uchaguzi, polisi hawapaswi kutembea na ilani ya CCM,walinzi wa Rais wasivae nguo za CCM kama walivyokuwa wanafanya wakati wa JPM, wakuu wa miko na wilaya wasiongelee mambo ya chama katika shughuli za serikali, Bashiru asengeteuliwa katibu mkuu
Yaani kweli hata mie mara nyingi, najiuliza kwanini ziara za viongozi za shughuli za kiserikali,huwa inakuwa kama ya kichama zaidi, badala ya kuvutia wananchi wote bila kugubikwa na regalia za chama tawala ...sasa vyama vingine navyo vikitia timu na mavazi yao,

Si itakuwa fujo aiseee...ndo maana wananchi wengine huwa wanajisikia kukwazwa na kuishia kushindwa kuhudhuria shughuli au mikutano hiyo, manake mwisho wa siku wanajisikia kama vile si wahusika.

Nafikiri ingekuwa vyema zaidi, kama shughuli za mikutano ya kiserikali siku zote ziweke mazingira ya rafiki kwa wote badala ya kuonekana ni kama shughuli ya chama fulani......au nadanganya jamani... kazi iendelee.
 
Kuna watu walizoea sana maisha ya ujanja ujanja na wizi wizi...Yule jamaa aliwapiga pin sana lazima wamchukie tu....Watanzani mlitaka rais mkali na dictator mnaanza kulia kulia..

Hii nchi usipokuwa mgumu kama JPM mambo meeengi lazima yakugomee kuanzia kwenye uchumi, siasa, utamaduni na kila mahala..Lile Jamaa lilikuwa na maamuzi haijalishi mabaya au mazuri wakati wengine hiyo kuamua tu ni shida.

Dola lazima iogopwe na iheshiwe na watu wote, JPM aliipa dola heshima na michezo ya kipumbavu dhidi ya dola ikafa au kupungua....Watu kama Manji, Mo hawa waarabu na wahindi walikuwa wakiichezea hii nchi watakavyo na mpaka kuidharau dola wao na wajukuu zao..

JPM pamoja na mambo yake ambayo inaonekana wengine walikereka lakini alikuwa ni Rais aliyepaswa kuiongoza hii nchi kwa miaka zaidi ya 20....Kuteka, kuua ni moja pia ya kazi ya dola kwa wajinga wote wanaoweza kuhatarisha uhai na misingi ya nchi gizani huku mbele ya wananchi wanajiita wema...tutambue ni serikali pekee dunia inayoweza kujua mipango ya gizani ya kila raia wake..

RIP JPM.....tulitofautiana mitazamo kwenye mambo fulani lakini yapo mengi pia uliifanyia hii nchi na kufundisha watu hii nchi inataka kiongozi aina gani..
Wewe nawe utakuwa na file kule mahala,, si bure[emoji23]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Rostam Azizi alikaribishwa Magogoni.
Bashite alikuwa mtoto pendwa wakati akiwa na kashfa ya vyeti.
Kujenga Airport kijijini kwako nayo dili tu.
Katika hali ya halisi ukiambiwa umechafua hali ya hewa ina maana umejamba. Kisiasa itakua umeongea jambo la kuwaudhi watu wengi kwenye siasa.

Wenye kumbukumbu watakumbuka enzi ya awamu ya nne iliyokuwa na kashfa nyingi za ufisadi hadi rushwa kuonekana kama ndio njia sahihi kufanikisha kila jambo Anton Dialo alistaajabisha watu kwa tukio moja. Enzi za awamu ya nne ilisemekana alimshitaki waziri wa maliasili enzi hizo kwa JK kwa kutoweza kumpa kitalu cha uwindaji baada ya kumpa dola za kimarekani kiasi fulani. Kuonesha jinsi rushwa ilikua kitu cha kawaida kwa wakubwa kufuatana na Dialo JK alimuamuru waziri huyo kumrudishia Dialo hela zake. Hakuna ushahidi kama JK aliwachukulia hatua yoyote vigogo hao.

Huyo Dialo enzi hiyo ya awamu ya nne alijilimbikizia vyeti feki hadi vya Phd huku kuna shaka ya yeye kufika japo kidato cha nne. Kuna mwandishi mmoja aliandika kitabu kuwaorodhesha watu mashuhuri wenye vyeti feki ambapo Anton Dialo ni mmoja wapo.

Kutokana na hila na kujilimbikizia sifa za uongo Anton Dialo ambaye pia ni mfanya biashara mkubwa akaweza kufikia kua naibu waziri.
Kwa ukweli kauli zake za kinafiki dhidi ya magufuli zimewaudhi wengi. Huyu ni mmojawapo ya watu wamekua wanasitiriwa ndani ya ccm kwa sababu ni mmoja ya wale waliyoigeuza ccm kama kampuni yao binafsi enzi za awamu wa nne.
 
Kuna watu walizoea sana maisha ya ujanja ujanja na wizi wizi...Yule jamaa aliwapiga pin sana lazima wamchukie tu....Watanzani mlitaka rais mkali na dictator mnaanza kulia kulia..

Hii nchi usipokuwa mgumu kama JPM mambo meeengi lazima yakugomee kuanzia kwenye uchumi, siasa, utamaduni na kila mahala..Lile Jamaa lilikuwa na maamuzi haijalishi mabaya au mazuri wakati wengine hiyo kuamua tu ni shida.

Dola lazima iogopwe na iheshiwe na watu wote, JPM aliipa dola heshima na michezo ya kipumbavu dhidi ya dola ikafa au kupungua....Watu kama Manji, Mo hawa waarabu na wahindi walikuwa wakiichezea hii nchi watakavyo na mpaka kuidharau dola wao na wajukuu zao..

JPM pamoja na mambo yake ambayo inaonekana wengine walikereka lakini alikuwa ni Rais aliyepaswa kuiongoza hii nchi kwa miaka zaidi ya 20....Kuteka, kuua ni moja pia ya kazi ya dola kwa wajinga wote wanaoweza kuhatarisha uhai na misingi ya nchi gizani huku mbele ya wananchi wanajiita wema...tutambue ni serikali pekee dunia inayoweza kujua mipango ya gizani ya kila raia wake..

RIP JPM.....tulitofautiana mitazamo kwenye mambo fulani lakini yapo mengi pia uliifanyia hii nchi na kufundisha watu hii nchi inataka kiongozi aina gani..
Safi sana! Na kwa taarifa, huyu mwamba kawaamsha wengi akili muda utasema tu!
 
Huyo Diallo hiyo analysis ya kushindwa uchaguzi alitumia factors zipi maana kama maoni hata mimi, wewe na yule ana yake..

JPM 2015 ndiye alikuwa game changer wa CCM, CCM walikuwa hawana namna zaidi ya kumsimamisha JPM ambaye wananchi tuliowengi wakati ule tulikuwa na imani naye na tuliamini ni mwaminifu, mchapakazi, na sio mpigaji kama hao akina Diallo wanao lialia..
2015 CCM walishinda kihalali kabisa na hii ilisababishwa na mtazamo mpya tuliokuwa nao dhidi ya Magafuri...CDM kumsimamisha EL nao lilikuwa kaa la moto kwao na advantage kwa CCM...
Unakosoa nini halafu unaandika nini?
Au nawe file lako limepita maeneo?[emoji2]
 
Huyo Diallo hiyo analysis ya kushindwa uchaguzi alitumia factors zipi maana kama maoni hata mimi, wewe na yule ana yake..

JPM 2015 ndiye alikuwa game changer wa CCM, CCM walikuwa hawana namna zaidi ya kumsimamisha JPM ambaye wananchi tulio wengi wakati ule tulikuwa na imani naye na tuliamini ni mwaminifu, mchapakazi na sio mpigaji kama hao akina Diallo wanao lialia..

2015 CCM walishinda kihalali kabisa na hii ilisababishwa na mtazamo mpya tuliokuwa nao dhidi ya Magafuli... CHADEMA kumsimamisha EL nao lilikuwa kaa la moto kwao na advantage kwa CCM...
Dialo alikuwa jikoni we ulikuwa mtaani
 
Mama samia na kamati kuu ya ccm wasimfumbie macho huyu Diallo.
Leo atamtukana kiongozi aliyepita kwa matusi km haya ila kesho napo atamtukana mama atakapostaafu.
Watu km hawa hawafai kuwa wenyeviti wa vitongoji.
Eti mwenyekiti wa ccm mkooa
Nani hajui uchafu wake??


Huku nikujipendekeza kishamba.
 
Mahojiano kati ya Mhe Anthony Diallo Mwenyejiti wa CCM Mkoa wa Mwanza na Mtozi Alloyce Nyanda*

Mjadala umeleta hisia na ushahidi mpya kuhusu utawala wa JPM
1. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Biashara yetu ya Star Tv ,RFA iliharibika -Diallo

2. Sie hatukulipwa na CCM , waliolipwa ni Crew iliyokuwa inatembea na vifaa kama majukwaa , walipewa hela ya kula na kubeba vifaa , ukitazama katiba vitabu vyetu kuna hela chama hadi leo haijakipa-Diallo Mwenyekiti wa CCM

3. Mgombea wetu wa wakati ule alisema atatusaidia na alisema hadharani tena mara mbili pale
Kirumba na furahisha lakini tuliambulia misukosuko

4. Awamu ya 5 iliharibu sana protocal ya Chama , viongozi wa chama walikuwa wanawekwa mstari wa nyuma kabisa gari zinakuwa mwisho hata kama ukifika unakuta mtu amekata utepe-Anthony Diallo mwenyekiti wa CCm

5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigiwa kiwako akadondondoka ,awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCm

6. Kuna siku nimemwambia waziri mkuu , hivi unajisikia raha gani kuzungukwa na mabunduki maana umezungukwa na mabunduki kama ishiri sie tumekuchagua ila unatuogopa ki vipi? -Antony Diallo

7. Swala hapa siyo katiba swala ni kuchagua watu makini ,unawezaje kuchagua kiongozi katika nafasi kubwa ya uongozi huku ana rekodi ya mirembe? Tuwe makini kuchagua viongozi-Anthony Diallo

8. Kama nchi tumepitia katika kiza kifupi ,tumepitishwa katika Black spot apo Nyuma , Sasa angalau watu wanaraha furaha imerejea-Dkt Anthony Diallo

9. Hata mimi Nimeshgulikiwa kidogo wakaniacha ila nimepata
Msukosuko-Anthony Diallo

10. katiba siyi ya Vyama ni ya wananchi kosa tulilofanya ni kugeuza katiba kuwa vyama na kuacha wananchi hata katika lile
bunge walitawala wananchi-Dk Anthony Diallo

11. Katiba siyo Tatizo , tatizo lipo
Kwa watu mnachagua Rais ambae hataki kufata katiba mtanfanya nini? Kwani katiba ya sasa ilikuwa inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila utaratibu? Lakini yamefanyika-Anthony Mwandu Diallo

12. Rais samia nimefanya nae kazi ni Rais makini na jasiri ni muumini wa utawala wa bora-Anthony Diallo

13. CCM tulijua haitashinda mwaka 2015 na wananchi wamegeuka wiki mbili tu baada ya kuamua hata kuunda makundi ya vijana kwenye maeneo mbali mbali waweke Star Tv ilibidi itumike nguvu

15. Kuna mambo hatukuweza kuyasema kwa sababu mfumo uliharibika kabisa. Tuliamua kunyamaza tuliamua ku place safe mode ili kesho uendelee kuishi na watoto wako.
 
Kikwete....kuna kipindi bangi ilimchanganyaga, akaacha ila nasikia karudia tena ila si kivile.
 
Back
Top Bottom