Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

"Msinichezee mimi nina faili milembe.." Spika Job Ndugai
 
Binadamu unapoongea lazima uwe na kiasi. Lazima upime hicho unachoongea kitakusaidia nini katika hustle zako ama kitakughalimu nini katika mahusiano yako na watu wengine.

Dialo kateleza, matamshi yake yaweza kuwa na negative impacts kwake hasa mahusiano yake na chama chake. Sidhani kama atapata uenyeki wa chama pindi muhula wake ukiisha. Kaanzisha mgogoro usiokuwa na faida yoyote kwake.
Mark my words.
Nimemsikia jana nikamshangaa, yule atamalizana na CCM mwakani,
 
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Je, ni TAL wa Chadema?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Labda huyu hapa?

 
Imani moja kuu ya mwana CCM aliyeiva kisiasa ni kusema kweli daima, na fitina kuwa mwiko.

Interview ya Mwenyekiti wa CCM na StarTv iko mitandsoni.
CCM ina wajibu wa kuitafakari, hasa juu ya utendaji wa Awamu ya Tano.

Kiufupi......

Mahojiano kati ya Mhe Anthony Diallo Mwenyejiti wa CCM Mkoa wa Mwanza na Mtozi Alloyce Nyanda

Mjadala umeleta hisia na ushahidi mpya kuhusu utawala wa JPM
1.Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Biashara yetu ya Star Tv ,RFA iliharibika -Diallo

2.Sie hatukulipwa na CCM , waliolipwa ni Crew iliyokuwa inatembea na vifaa kama majukwaa , walipewa hela ya kula na kubeba vifaa , ukitazama katiba vitabu vyetu kuna hela chama hadi leo haijakipa-Diallo Mwenyekiti wa CCM

3.Mgombea wetu wa wakati ule alisema atatusaidia na alisema hadharani tena mara mbili pale Kirumba na furahisha lakini tuliambulia misukosuko

4.Awamu ya 5 iliharibu sana protocal ya Chama , viongozi wa chama walikuwa wanawekwa mstari wa nyuma kabisa gari zinakuwa mwisho hata kama ukifika unakuta mtu amekata utepe-Anthony Diallo mwenyekiti wa CCm

5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigiwa kiwako akadondondoka ,awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCm


6. Kuna siku nimemwambia waziri mkuu , hivi unajisikia raha gani kuzungukwa na mabunduki maana umezungukwa na mabunduki kama ishiri sie tumekuchagua ila unatuogopa ki vipi? -Antony Diallo

7. Swala hapa siyo katiba swala ni kuchagua watu makini ,unawezaje kuchagua kiongozi katika nafasi kubwa ya uongozi huku ana rekodi ya mirembe? Tuwe makini kuchagua viongozi-Anthony Diallo

8. Kama nchi tumepitia katika kiza kifupi ,tumepitishwa katika Black spot apo Nyuma , Sasa angalau watu wanaraha furaha imerejea-Dkt Anthony Diallo

9. Hata mimi Nimeshgulikiwa kidogo wakaniacha ila nimepata msukosuko-Anthony Diallo


10. katiba siyi ya Vyama ni ya wananchi kosa tulilofanya ni kugeuza katiba kuwa vyama na kuacha wananchi hata katika lile
bunge walitawala wananchi-Dk Anthony Diallo

11. Katiba siyo Tatizo , tatizo lipo kwa watu mnachagua Rais ambae hataki kufata katiba mtanfanya nini? Kwani katiba ya sasa ilikuwa inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila utaratibu? Lakini yamefanyika-Anthony Mwandu Diallo

12. Rais Samia nimefanya nae kazi ni Rais makini na jasiri ni muumini wa utawala wa bora-Anthony Diallo

13. CCM tulijua haitashinda mwaka 2015 na wananchi wamegeuka wiki mbili tu baada ya kuamua hata kuunda makundi ya vijana kwenye maeneo mbali mbali waweke Star Tv ilibidi itumike nguvu

15. Kuna mambo hatukuweza kuyasema kwa sababu mfumi uliharibika kabisa. Tuliamua kunyamaza tuliamua ku play safe mode ili kesho uendelee kuishi na watoto wako.

Diallo kashangaza kawa mkweli na muwazi
 
5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigiwa kiwako akadondondoka ,awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCm
Safi sana..., asingepigwa ila angeambiwa aondoke na kusimama na wengine huko....., Haya mambo ya kugeuza shughuli za nchi kama vikao vya chama hawa jamaa wapigwe tu..., hakuna namna, ili huu ushamba uishe.... (Eti Viongozi wa CCM)
 
Hebu tunaomba video moja ya Dialo akiongea mbele ya Mwendazake au hata mazungumzo yake siku ya msiba
 
Ngosha Diallo ni chuma
Siungi mkono alichofanyiwa ila si mtu safi kihivyo nadhani pia awe amejifunza kuwa mwema kwani aliwafanyia watu wengi mabaya na waliumia kama yeye na walikuwa na watoto kama yeye ila hawakuwa na kituo cha Tv kuongelea alivyowaumiza na hata kupelekea wengine kufa kwa sonona
 
Huwa najiuliza, Hayati Mpendwa wetu angeweza kukaa kimya akishuhudia Watu wakimsagia kunguni baada ya kustaafu?

Kama angestaafu wangemgeuka na kuanza kumsema sana kama walivyomsema Nyerere na Mkapa

Mara nyingi Viongozi walioruhusu kusemwa na kuandamwa wakiwa madarakani wakistaafu watu huwa wanaachana nae kwa kuwa hakuna Dongo jipya, ila wale walioogopw sana wakiwa Mamlakani hupata shida sana wakistaafu
 
Back
Top Bottom