Kwakweli huu mradi kila nikiuangalia na complications zake huwa nakuna kichwa sana na kujiuliza kina nani walipendekeza mradi wa aina hii?
Pamoja na usanifu wake kujikita kwenye gharama za juu bado sijawahi kuona faida ya mradi huu na sijui kama utakuja kukamilika. Mbaya zaidi umeshatushinda kuuendeleza kwa wakati.
Kiukweli nchi yetu ni masikini sana na hakukuwa na tija yoyote kubuni mradi ambao utakula zaidi ya trilioni 7 Tshs fedha za awali huku ukiwa hauna maana kwa nchi.
Hivi ni mizigo kiasi gani itakayo kuwa inapita kwenye hiyo reli hadi tuigharamie hivyo?
Bomba la mafuta limefeli na sasa Uganda ameamua kuegemea Kenya zaidi, serikali yetu bado haijatueleza ni kwanini? Huu mradi utakuwa unatumiwa na watu wa kanda ya ziwa kusafirisha matikiti maji?
Yani Rais Magufuli kwakuwa ana nguvu ya kutumia fedha za nchi basi amekuwa akizitumia kwa utaratibu mbovu kweli.
Sioni pia tija kwenye daraja la coco beach baada ya serikali kuhamia Dodoma, sioni tija yoyote kwenye daraja la huko sijui busisi kanda ya ziwa dah yani watanzania wengi wanataabika ili kugharamia miradi isiyo na tija yoyote ile.
Haya ni mawazo ya G Sam? Siamini!
Inaelekea ujenzi wa mradi wowote kwako ni hasara, maanake umeorodhesha baadhi ya miradi hiyo. Tanzania itabaki kama alivyoiacha mkoloni tukifuata mawazo kama haya.
Ndio, inawezekana ikawa ngumu sana kuukamilisha huo mradi wa reli kwa wakati uliopangwa lakini hiyo isiwe sababu ya kutoujenga.
Umefanya uchambuzi upi uliofanya uone mizigo haipo na haitakuwepo miaka yote ijayo? Maana yako ni kwamba hapatakuwepo na maendeleo daima ndani ya nchi hii?
Uduni wa maoni ndani ya mada ni huu:
- Maadam serikali imehamia Dodoma, basi hakuna sababu za kuiendeleza Dar?
- Ushahidi wa bomba la mafuta kuhamia Kenya upo wapi?
- Tsh 7Trillion kwako ni mwisho wa Tanzania kuwepo?
- Huonyeshi takwimu zozote kuhusu mizigo iliyopo leo na itakayokuwepo kesho na keshokutwa, wewe unaangalia sasa tu!
- kwa maana hiyo hiyo, hata bandari hazistahili kupanuliwa na nyingine kujengwa?
Kiufupi, hii ni mada mbovu ya kuanzia mwaka 2020 hapa JF; na sidhani kwamba G Sam anahusika katika kuiandaa.