Nani atakuja kutufidia sisi kama nchi kutokana na mradi usio na tija wa SGR?

Nchi pekee na Burundi wanapelekewa reli ya gharama kiasi hicho. Sisi kama nchi hatuna akili kwakweli.
 
Bila shaka huoni tija pia ya kujenga Ofisi Kuu za Chadema ndio maana mmeishia kupanga mabanda pale Ufipa! Ahahahahahaha!
Tatizo lenu uvccm hamna hoja za kujibu bali kila jambo mnaingiza siasa. leta hoja za kutetea huu mradi then uanzishe hoja yako juu ya ofisi za chadema nje ya mada hii
 
Huwezi kunifundisha kitu kuhusu haya mambo. Pia huwezi kuelewa nilicholalamikia na naelewa nyie wapiga makofi wa awamu hii kila kitu anachotoa Magufuli nyie kazi yenu ni kupokea bila kuhoji.
Mkuu mbona kama nyie pia mnapinga kila kitu anachokifanya Magufuli. Sio kwamba anaesifia kila kitu na anaeponda kila kitu wote ni sawa tu?
 
Umewahi kwenda nchi zilizoendelea? Umeshawahi kuona nchi isiyo na usafiri wa treni? Usafiri wa treni una kawaida hii: kujenga ni gharama lakini manufaa yake ni makubwa!
Reli ndio uchumi wa nchi. Wajifunze kwa nchi kama Us na SA
 
G Sam,
Mshamba wa Koromije anadhani watu tunahitaji kushangaa madaraja na mabugando kama yeye
 
G Sam,
Afadhali SGR Kiongozi. Ule wa umeme ndiyo kimeo squared.
Maji hayo hutoka Mtera na Kidatu. Huko mitambo inafungwa kwa ukame, Stieglers Gorge nayo itakauka tu kipindi fulani.
Tumeacha umeme wa gesi. Bado kuna ardhini (thermal).
Tatizo ni kupata percent miradi mipya
 
Mkuu, nakuhakikishia kama kuna kimeo ambacho Magufuli amekivaa basi ni aina ya huu mradi wa SGR. Yani hauna tija kabisa na hela ya mradi hitokaa irudi
 
Mni mpumbavu asiyeona faida ya mradi huu.

Labda ungeuliza uendeshaji wake, lakini ni mradi mzuri sana na wenye faida kubwa ya muda mrefu ikiwa tu tutaweza kuuendesha wenyewe bila kutegemea mataifa ya nje.
Tatizo la maoni mengi ni kudhani kwamba maisha ya duniani yanaisha baada ya mtu kufariki.

Ni mawazo ya kibinafsi ambayo yanawazia leo na kesho wakati kuna Tanzania ya miaka 50 ijayo.
 
So huyu dogo ni mpumbavu


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama anaamini hauna tija, atakuwa ni mpumbavu tu.

Mashaka yangu ni katika kuuendesha tu huu mradi si kwengine.

Nasubiri kuona mbinu ipi itatumika kuuendesha huu mradi ambayo itakuwa na tija kuliko ya reli zetu zingine mbili tulizonazo hivi sasa.

Kusema kweli tuna mtihani mkubwa sana mbele yetu na nikifikiria wafaulu wetu walipotufikisha hivi sasa, napata kigugumizi cha vipi niusifu.
 
Nmekusoma michango yako kwenye huu uzi wako..
Nihitimishe tu kwa kusema kwamba wewe ni mpumbavu na mbumbumbu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasomi wa Tanzania wamesoma kufaulu mitihani na kupata vyeti kwa njia ya kukariri ila kiukweli kichwani hamna kitu. Kwa hiyo ukiona vitu haviendi sawa katika uendeshaji ujue ni uwezo mdogo wa waendeshaji.

Kuna tatizo katika elimu ya Tanzania inabidi litatuliwe.
 
Mama, huu mradi hauna tija. Mwaga facts nijibu facts kuhusu huu mradi na mbaya zaidi naelewa nchi nyingi zenye SGR physically!
 
Mkuu naomba nikuweke sawa. Ukiona kwenye uendeshaji wa mradi mtu unakwama ujue basi kwenye investment cost hukuwa sahihi.
 
Mkuu naomba nikuweke sawa. Ukiona kwenye uendeshaji wa mradi mtu unakwama ujue basi kwenye investment cost hukuwa sahihi.

Mradi unaweza kukwama kwa matatizo mbalimbali ila uendeshaji mbovu huchangia asilimia kubwa kukwama kwa mradi wowote.

Ila hata hiyo "investment cost" pia inapangwa na watu na hao watu ndio haohao wenye elimu ya vyeti na kukariri kwa hiyo wakikosea usishangae.
Ndio maana naona tatizo ni elimu yetu ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…