Kama Reli ya kati haitengenezi faida, TAZARA haitengenezi faida, hakuna muujiza wa kuifanya SGR kutengeneza faida. Kama kungekuwa na msongamano wa mizigo ambayo reli ya sasa ya kati inashindwa kuhudumia, hakika kupata treni ya kasi ingesaidia kuisafirisha mizigo yote. Mpaka sasa, reli ya kati inafanya kuokoteza mizigo. Hata siku moja haijawahi kutosheleza uwezo wa treni kubeba, sasa hiyo ya kasi zaidi itabeba mizigo gani? Na hakuna reli duniani inayopata faida kwa kusafirisha watu.
Reli ilikuwa ni muhimu lakini ilitakiwa ujenzi wake utegemee zaidi sababu za kiuchumi kuliko matakwa ya moyo.