Ubena Zomozi
JF-Expert Member
- Jun 19, 2022
- 1,608
- 1,286
Huna loloteKumuomba Mungu afanye miujiza tuondokane na hii laana ya state capture.
Hili
.https://www.jamiiforums.com/threads/nusura-ya-tanganyika-ni-anguko-la-ccm.2264411/
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huna loloteKumuomba Mungu afanye miujiza tuondokane na hii laana ya state capture.
Hili
.https://www.jamiiforums.com/threads/nusura-ya-tanganyika-ni-anguko-la-ccm.2264411/
ikiwa vyama vya siasa hususani upinzan vitaacha ushirikina, ramli chonganishi, kutoana kafara na unganga wa kienyeji ili kupata uongozi ndani ya vyama vyenyewe,
na wakaanza kutumia hoja, sera, mipango mikakati mahususi ya kushawishi wananchi kuwaunga mkono, nadhani manung'uniko na mapendekezo dhaifu yasiyo na tija kama haya yasingekuepo kabisa humu jukwaani,
Zaidi sana,
upinzan ukiepuka kukurupuka na kujipa umuhimu wasio shahili kupindukia mbele ya jamii, na wakacha mihemko na ghadhabu za kinyumbu pale wanapokosolewa kwenye masuala mepesi kabisa, inafanya jamii nzima iwaone wapinzani kama watu waliokua confused tu...
Lakin pia kuporomosha matusi mazito mazito na kutukana wenye watu mawazo na mitazamo tofauti dhidi maoni yao, hii imefanya watu wengi sana wenye hekima na busara zao, kujitenga na kupuuzia mawazo yanayoibuliwa na wapinzani ambao wanaenekana kabisa ni watukanaji tu..
Wapinzani wanalalamika sana mpaka wanasahau nini wanadai au wanatetea. wamepoteza uelekeo kabisa. mathalani, check hata mtoa hoja hii anaehoji na kuomba kuungwa mkono na wadau humu JF. Matokeo yake ataungwa mkono na wenye mihemko, waporomosha matusi tu na watukanaji tu ambao siku zote ni waoga kichizi field. Hawatokagi kwenye maandamano, hawajitokezagi kupiga kura...
kiujumla Tanzania hakuna state capture. Na CCM itaendelea kuongoza nchi na kuwaletea wanainchi maendeleo endelevu kadiri uwezavyo...
hakuna umuhimu wa katiba mpya kwa sasa, hakutawahi kutokea mass uprising, wala muujiza wowote wa kishirikiana...
liberations zifanywe ndani ya vyama vya siasa vilivyogawanyika na vyenye uhasama na uadui mbaya sana baina ya viongozi waandamizi wake, mathalani chadema, nccr mageuzi n.k🐒
Njia ya tatu ni Nzuri na bora sana. Kwa ufupi njia nne ulizopendekeza ni bora zaidiKwa Sasa Tanzania ipo kwenye Hali ya state capture, baada ya serikali, vyombo vya Dola , mahakama na bunge kuwa kitu kimoja na kuondoa uwajibikaji. Leo bunge limeacha kazi yake ya kuisimamia serikali baadala yake limekuwa rubber stamp ya maamuzi ya serikali. Kwa mfano bunge la Tanzania limetumika kupokea wabunge wasiokuwa na chama au waliofukuzwa kwenye chama chao.
Ila kwa sababu ya state capture bunge linafanya maovu na hakuna wa kuligusa. Bunge kupitia Spika wake wameona suala la wananchi kutekwa sio la msingi kujadiliwa bungeni ila kumpongeza Rais Kwa hotuba yake ndio la muhimu zaidi.
Swali ni je, nani atasaidia tuondokkane na bunge la mchongo lililojaa machawa wa serikali wasiojua majukumu yao?.
Mahakama ndio imeoza kupindukia. Kuna kipindi Jaji Mkuu Ibrahim Juma alisema hadharani ya kwamba majaji watoe hukumu kwa kuangalia falsafa ya serikali.
Yani baadala ya mahakama kuwa huru na kufanya maamuzi stahiki, Jaji Mkuu anashauri majaji waangalie muelekeo wa serikali ni upi.
Jaji Mkuu mwenyewe alitakiwa kustaafu kwa mujibu wa Katiba ila kutokana na state capture aliongezewa muda kinyemela. Ndio maana Rostam Aziz alidai ya kwamba mahakama zetu zinapigiwa simu tu na kutoa maamuzi.
Swali ni nani atawasaidia wananchi waondokane na mahakama mbovu ya Tanzania?
Vyombo vya Dola navyo vinajiendesha under state capture.
Ndio maana mpaka Leo tunajikanyaga kuhusu nani anateka watu na kuwapoteza. Polisi hawajui, TISS hawajui na hata JWTZ hawajui. Sasa nani atawalinda wananchi dhidi ya utekaji . Leo Kuna wananchi jumla ya 89 wamepotezwa mpaka Leo ila kila mtu hajui wapi wapi. Yani raia anaondolewa kwenye basi na kuuawa na hakuna anayewajibika.
Inasikitisha sana. Kutokana na state capture wananchi watazidi kupotezwa na hata kuuawa bila ya msaada. Nani atawasaidia wananchi na huu ukatili?
Serikali imejaa dharau na kebehi. Waziri wa Fedha alifikia sehemu ya kusema asiyeridhika na tozo ya miamala ya simu ahamie Burundi. Kauli za dharau na kiburi maana hakuna wa kumwajibisha. Rais Samia akatoa Lugha ya dharau kwamba wanaotekwa wanajiteka wenyewe.
Na hakuishia hapo akaendelea kudai hata waliouawa kwenye matukio ya utekaji Vifo vyao ni vya kawaida. Yani kwake uhai wa raia ni kawaida tu. Anaongea hivyo maana state capture inamsaidia na hakuna uwajibikaji na hakuna atakalofanywa. Ni nani atatusaidia tuondokkane na Rais mwenye kiburi na dharau Kama huyu?
Leo Tanzania Tume ya Uchaguzi inaweza kuamua kuwapa CCM majimbo yote na hakuna atayeiwajibisha.
Leo watu wanaweza kuamka asubuhi na kwenda kuapishwa bungeni bila kuwa na chama na Wakaaapishwa.
Mimi nadhani Kuna njia nne za kuondokana na huu ufirauni wa state capture nchini Tanzania.
1. Katiba Mpya itakayoweka structures na uwajibikaji. Yani mtu akitekwa hadharani mchana akaenda kuuawa , RPC wa eneo lililotokea utekwaji anawajibika mwenyewe kwa kutochukua hatua. Juzi hapo Kenya IGP Msaidizi alihukumiwa miezi SITA jela kwa kudharau mahakama baada ya raia kupotea bila sababu. Pona yake wale raia wawili waliopotea walipatikana siku hiyo na yeye kuomba msamaha mahakama na kusamehewa.
2. Mass Uprising. Wananchi waanazishe maandamano nchi nzima kushinikiza kuoondka kwa state capture Tanzania. Hii kwa Tanzania itakuwa ngumu mpaka pale kila mmoja atakapoguswa .
3. Second Liberization movement. Hapa ni kuanzisha kikundi Cha uasi kuondoka state capture na kurudisha mamlaka kwa wananchi. Hii njia sio nzuri maana itapelekea vita na mauaji na mambo mengi kurudi nyuma.
4. Kumuomba Mungu afanye miujiza tuondokane na hii laana ya state capture.
Hakika Tanzania inahitaji kuokolewa. Ni kama Mwanaume aliyelishwa limbwata na hawara akatelekeza familia. Kuna kikundi cha watu wachache kimeikamata Nchi hawataki kuachia. Wako tayari kuua ili mradi waendelee kutawala
Hawataki Katiba mpya wala Tume Huru kabisa ya uchaguzi. Mkaza Mwana ndio anasimamia uchaguzi na wanasema anayetangaza matokeo ndio anaamua mshindi. Hakika wananchi wa Tanzania wanahitajika kufanya maamuzi magumu uchaguzi wa 2024 na 2025.
Tutaendelea kumlaumu Nyerere hadi lini kwani sisi ni misukule yake?Tangu lini mihimili ya serikali ya Tanzania ya kawa huru wa kulaumu ni Nyerere ndo chanzo cha siasa za state supremancy.
Nyerere unamlaumu bure. He did what he could do during his watch.
You are (as we all are) also charged to do what you can do during your watch!
Kwa kweli suala lililobaki ni kumuomba sana Mungu bila kuchoka ili aonyeshe njia ya namna ya kuondokana na utawala huu dhalimu, uliojikita katika kuwapoteza raia na mauaji holela ya wananchi
Ni kweli lakini usisahau kipindi cha Nyerere wapo waliowajibishwa na wengine kuwajibika wenyewe pale yalipotokea ya kutokea !
Hayati Mzee Mwinyi kwa mfano mmoja tu ,
So Nyerere mumuache apumzike !
Baba kama hakujenga nyumba mpaka mwisho wa uhai wake nami nifanye vivyo hivyo hata kama uwezo ninao ?????!!!! 😳🙄🙏
UMENGOJA NINI MUDA WOTE HUO??HADI ALIESABABISHA HIYO SITUATION KAFA NDIYO UJE KUSEMA LEO??
HATA KUPONGEZA REFORMS ALIZOZIFANYA THE CURRENT PRESIDENT HAUTAKI.
UMENGOJA NINI MUDA WOTE HUO??HADI ALIESABABISHA HIYO SITUATION KAFA NDIYO UJE KUSEMA LEO??
HATA KUPONGEZA REFORMS ALIZOZIFANYA THE CURRENT PRESIDENT HAUTAKI.
UMENGOJA NINI MUDA WOTE HUO??HADI ALIESABABISHA HIYO SITUATION KAFA NDIYO UJE KUSEMA LEO??
HATA KUPONGEZA REFORMS ALIZOZIFANYA THE CURRENT PRESIDENT HAUTAKI.
Kwani kuna mtu kanyimwa mshahara au kuna wananchi wanazuiwa wasifanye kazi zao za kila siku kama hakuna kilichokwama basi acha tupige kazi.
Kwa kweli hali inasikitisha sana.
Nakumbuka Rais Samia, baada ya kifo Cha Ali Kibao, ali-post Kwenye ukurasa wake wa Twitter, kuwa amesikitishwa mno na kifo Cha Ali Kibao, hatataka matukio ya aina hiyo yajitokeze nchini kwetu, Kwa kuwa nchi hii ni ya kidemokrasia na Kila mtu ana HAKI ya KUISHI
Siku chache zilizofuata, Rais kageuka na kusema kuwa eti hicho kifo ni drama tu na kifo ni kifo tuu!😳
Hivi sasa ni mwezi kamili tokea kifo Cha Ali Kibao, hakuna uchunguzi wowote unaoendelea kuhusu kifo hicho Cha Ali Kibao na yeye Rais Samia amegoma kuunda Tume huru ya Kijaji kuchunguza kifo hicho!😳
Dawa iliyobaki ni Moja tu Ili kuondoa hiyo State Capture ni Kwa wananchi wote kujitoa Kwa kile tunachoita People's Power na kuwalazimisha hawa watawala wetu wakatili ili wasalimu amri na kuirejesha nchi yetu Kwenye Demokrasia kamili