Nani atatusaidia kuondoa 'state capture' Tanzania?

Je alchofanya jamaa ni saw au la

Mass Uprising. Wananchi waanazishe maandamano nchi nzima kushinikiza kuoondka kwa state capture Tanzania. Hii kwa Tanzania itakuwa ngumu mpaka pale kila mmoja atakapoguswa
labda simba na yanga zibadilishwe kuwa vyama vya siasa, maana parade ya timu hizi mbili ndo parade pekee kwa tanzania zinazoongoza kukutanisha watu wengi zaidi na sirikali ikawa comfortable, na wakati mwingine inayatumia haya makutano kupenyeza agenda zake, otherwise tusubiri miaka mingine60.
 
1. Yatakiwa kuwe na nguvu ya pamoja ambayo italazimisha kubadili tabia ya kiongozi au viongozi ambao wamefanya state capture kwa njia ya maandamano. Kwa kuwa maandamano yameshindikana basi njia ingine ni ushawishi kwa umma kupitia mitandao ya kijamii. Hii ni ya kiufundi zaidi kwani kila kitu huwekwa kwenye tovuti ya Upinzani na wananchi wao kwenda humo kujifunza mengi.

Msanii wa muziki Ney kashindwa kufikisha ujumbe alokusudia wa wimbo wake wa Ntasema kwa sababu "gate keepers" wa "State Capture" wapo macho na wamei-alert BASATA hivyo hata njia ya muziki nayo ipo kwenye list ya maeneo ya kuyamulika.

2. Kuimarisha umoja ndani ya vyama vya upinzani khasa Chadema kwa kujitayaarisha na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuendelea kufanya semina na vyombo vya serikali ili kuelimishana kuhusu sheria, haki na wajibu wa kila mwananchi kuheshimu sheria na pia kwa vyombo ya dola kuheshimu utawala wa sheria. Ni jambo jema lilofanywa na TLS kwa kuweka kongamano ambalo lilihudhuriwa na polisi akiwemo kamishna Murilo.

Lakini hili latiwa dosari kwa Tundu Lissu kuachana na ajenda kama ya kuichachafya CCM na kuamua kushughulikia kesi yake na Tigo (yaeleweka) lakini ile momentum kwa upinzani inakuwa inakufa kwa kuzingatia pia kwamba hata Freeman Mbowe nae mpaka sasa amekuwa kimya. Itakuwa ni jembo linofaa endapo upinzani utaungana tena na kuweka kitu kama UKAWA ili kuwa na nguvu moja na sauti moja, kisha kutengeneza stratejia ya ushindi.

3. Vyombo kama TLS huu ndo wakati wake wa kuwabadilisha tabia (habits) wanasheria khasa majaji, mahakimu na mawakili wa pande zote kuhusu kuheshimu misingi ya sheria. Lazima sheria ibadilishwe watu wasitekwe na polisi basli wakamatwe na kuwekwa ndani kwa kufuata sheria ikiwemo kuomba kibali cha kumshikilia mtu zaidi ya masaa 24. TLS pia yatakiwa kuchochea kubadili kanuni za uteuzi ambapo wanasiasa hawawezi kuteuliwa katika nafasi za mahakama.

Kuna mengi lakini yote yahitaji vichwa visivurugwe kama anavyovurugwa mheshimiwa Mpina au Mbowe na Lissu.

Hadi sasa upinzani umekosa msemaji kwani Tundu Lissu yuko London na Mbowe hajulikani aliko, na walobakia wote ni CCM B.
 

Kweli mkuu unafiki unatusumbua
 

Umeongea ukweli mchungu mkuu.
 

Inaonekana hujui maana ya reforms. Tofautisha reforms na administrative action. Mikutano ya siasa na haki ya wakulima na wafanyabiashara zipo kikatiba ila administrative action ndio imepelekea kuvikataza na kuvirudisha. Reforms ni suala la Kikatiba kabisa mabadiliko ambayo yanatoka kwa wananchi na Sio matakwa ya Rais. Unaona Kenya IGP anaweza kuhukumiwa na Mahakama miezi SITA jela mpaka alipoomba msamaha. Huku Tanzania IGP ni Mungu Mtu.
 
Ni mtihani mkubwa ambao unalikabili Taifa leti kwa muda mrefu,changamoto nikwamba,niwangapi wanaelewa hilo? Watz wengi bado niwavivu wa kujifunza mambo na hii ndio inatupelekea kulipa gharama kubwa ya mateso.

Kweli kabisa mkuu, watanzania wengi hata hawapo informed.
 

Sawa mkuu
 

Kweli kabisa mkuu. Tukifanyia kazi ushauri wako tutafika mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…