Elections 2015 Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?!

Elections 2015 Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au shetani aliyegeuka malaika?!

mtu tangia azaliwe na tangia aanze utumishi wa uma au mtu kwa miaka zaidi ya arobaini hajawahi amini katika uadilifu yaani amekuwa jizi fulani tu halafu eti akishazeeka ndo abadilike awe muadilifu, subutuuuuuuu. mwizi ataendelea kuwa mwizi tu
 
wapi ulisikia shetani wa ukweli anakuwa malaika? ukiona hivyo huyo hakuwa shetani alikuwa msanii tu

Kila kitu kipo chini ya Mungu so sioni ajabu juu ya shetani kuwa malaika cuz vice-versa is true kama malaika alikuwa shetani.Jifunze kutafakari siyo kuropoka.
 
uzoefu wetu kwa maraisi waliopita ni kuwa tabia ya rais inabaki vilevile hata akiwa rais.

mzee mwinyi na uungwana wake ulibaki vilevile
mkapa alibaki vile vile japo mwishoni akaja kutibua tibua
kikwete wa tangia akiwa waziri alibaki yule yule hata aliposhika urais

kwahyo dr magufuli akiwa rais atabaki na uchapakazi wake pamoja na uadilifu wake

kwa upande mwingine lowasa akishika urais ataendeleza vitu vyake vile vile - bila kusahau kutengeneza turichmond, etc
 
Must watch: Nembo ya Magufuli, mgombea wa CCM yazua utata
Must watch: Nembo ya Magufuli, mgombea wa CCM yazua utata



  • Tazama hapa chini kwa umakini sana.... Kisha tafakari oktoba 25 tuchague kiongozi wa namna gani!...

    Hii ni kama alama ya freemason​

    paperclip.png
    Attached Thumbnails

 
Ukomavu wa kisiasa na uzalendo wa kweli katika nchi za wenzetu ni jambo la shani. ni njia inayoiwezesha nchi iweze kwenda mbele; lakini cha ajabu kwa nchi yetu kuna shida kubwa sana ya kufikiri kuwa mzalendo ni lazima uwe mwananchama wa chama cha mapinduzi; chama ambacho kimeshindwa kutimiza malengo ya wapigania uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. kitu kibaya zaidi ni kuwa mwalimu na hekima zake mnazitumia tofauti na dhamira ya yeye kujitolea kupigania uhuru kwa niaba ya watanzania; kwa hakika nchi hii mnaipeleka ndiko siko. mm naamni kuwa nchi yetu si maskini ila watu wake. nchi hii ina kila raslimali; kuanzia madini, mbuga za wanyama, kandA tofauti za ekolojia (zinazoiwezesha nchi yetu kuendesha kilimo cha mazao ya aina mbalimbali karibu yote yanayopatikana duniani), ukaribu wake na bandari, milima na mabonde mazuri, soko kubwa la nchi zinazoizunguka. ni kwanini tumekwama kwa miaka yote 54? jibu ni wazi kuwa viongozi wamepotoka na wametupeleka korongoni kusiko ama kwa sababu ya uwezo wao mdogo ama kwa makusudi. ni jambo la maana sana kama watawala watachukua maamuzi magumu ya sio kujisahihisha tena maana wamepewa miaka mingi sana kufanya jambo hilo lakini wameshindwa kiasi sasa wameshawishaka kufanya uhalifu kwa nchi yetu. Si kwamba mwalimu Nyerere hakujua kuwa nchi ina dhahabu nyingi na sikweli kuwa watu wa nje hawakumashawishi kuvuna hizo raslimali ambazo leo zinavunwa bila watanzania kufaidika nazo, LA HASHA. MWALIMU ALIKUWA MZALENDO WA KWELI ALIYEIPENDA NCHI YAKE NA WATU WAKE . NI MSOMI NA NABII WA NCHI YETU. MTU ASIYE WA TAMAA KAMA VIONGOZI WETU WA LEO. VIONGOZI MLIOKO MADARAKANI MUWE TAYARI KUIKABIDHI KWA ATAKAYESHINDA BADALA YA KUTOA KAULI KUWA MKO TAYARI KUFANYA VITU VYOTE LAKINI SI KUKABIDHI NCHI KWA YUELE AMBAYE WANANCHI WANAMTAKA, USHINDI KWA CCM NI LAZIMA, GOLI LA MKONO; MANENO KAMA HAYA NI CHUKIZO MBELE ZA MUNGU ALIYEIUMBA TANZANIA, KAMA KWELI MMEITENDEA MEMA NCHI YETU NI KWA NINI MTAFUTE KUJITWALIA MADARAKA KWA GOLI LA MKONO AU MKO TAYARI KUFANYIWA LOLOTE ISPOKUWA KUIKABIDHI NCHI KWA MSHINDI WA UMMA HAPO OKTOBA , 25, 2015? JE HAMUONI HILO NI CHUKIZO MBELE ZA MUNGU WETU NA KWA TAIFA LETU? WATAWALA WATAKWENDA LAKINI TAIFA LA TANZANIA LITADUMU KAMA MKIZINGATIA KUSHINDWA KWENU KUENDESHA NCHI YETU. MMESHINDWA MMESHINDWA ACHENI WENYE UWEZO WAIONGOZE MSIWAANGALIE KWA MACHO YENU YA HWILI FANYENI MAOMBI MFUNULIWE NA KUIKABIDHI NCHI KWA WALE AMBAO MUNGU AMEAMUA WAONGOZE. MSILAZIMISHE WATU WAMEWACHOKA. LET US HAVE A NEW BEGINNING FOR THE BETTER BRIGHT FUTURE
 
Inawezekana lowasa si msafi lakini anabebwa Na vyama visafi na usafi wa vyama hivyo utamuongoza kutenda yaliyo mema tofauti na upande wa pili kuna mtu anaedaiwa kua ni safi lakini chama kilichompa dhamana si kisafi kiko ovyo kitu ambacho kitamfanya hata yeye ashindwe kuwatumikia raia kama kikwete
 
Kwanini usiseme tu sio msafi eti inawezakana alaf kumbuka kwa katiba ya jmt raisi hakiwa madarakani ashitakiwi ata chama chake kikimuwajibisha katiba ya nchi ita mlinda so usilete story zako za mtu mchafu chama kisafi au mtu msafi chama kichafu nakuomba tuchague mtu msafi
 
Kamwe! lowasa hatakuwa msafi ni fisadi, mwizi, mla rushwa mpaka anakufa. mikono yake ina hatia kubwa sana, ana dhambi nyingi mbele za mungu na mbele ya watanzania na adhabu yake soon ataipata maana malipo ni hapa hapa duniani. The time w'll tell
 
Wanabodi,

Leo tena naendelea na zile makala zangu za malaika na shetani.

Kwa wasomaji wapya katika kukumbushana tuu, hapo hapo mwanzo, shetani alikuwa malaika kabla hajawa shetani, tena ndio alikuwa malaika Mkuu! .

Kwenye himaya ya mashetani shetani hayuko peke yake, yuko na wale malaika wengine waliojiunga nae ambao sasa wote ni mashetani wengine walioamua kujiunga nae!.

Katika la jeshi la malaika wa mbinguni from time to kuna baadhi ya malaika huwa wana defect na kumfuata shetani na hivyo hugeuka mashetani.

Vivyo hivyo kwenye jeshi la shetani kuna mashetani huwa wanatubu na kumrudia Mungu hivyo hurejea na kuwa malaika. Hawa sasa ni harmless kwa sababu ushetani wao wote wanakuwa wameuacha kule ushetanini!.

Lakini inapotokea malaika akaamua kufanya kazi ya shetani huku amepose kama malaika!, huyu ni hatari kuliko hata shetani mwenyewe!, maana you can't tell!. Watu wa Mungu watamsikiliza wakidhani ni malaika kumbe nje na ngozi tuu ndio ya malaika lakini ndani ni ibilisi mwovu shetani wahedi! .

Swali ni jee?, nani ni hatari zaidi kati ya shetani aliyetubu na kugeuka malaika au malaika aliyegeuka shetani kwa kufanya kazi ya shetani huku akiendelea kupose as malaika?!.

Tafakari na chukua hatua.

Nawatakia Jumatano njema.

Pasco
Inaleta maana. Tahadhari nzuri.

But: Even a devil was an angel.

In that sense, an angel can change into a devil.

Then, the question is: if a devil was once an angel, can a devil become an angel again at some point...?
 
Wanabodi,

Leo tena naendelea na zile makala zangu za malaika na shetani.

Kwa wasomaji wapya katika kukumbushana tuu, hapo hapo mwanzo, shetani alikuwa malaika kabla hajawa shetani, tena ndio alikuwa malaika Mkuu! .

Kwenye himaya ya mashetani shetani hayuko peke yake, yuko na wale malaika wengine waliojiunga nae ambao sasa wote ni mashetani wengine walioamua kujiunga nae!.

Katika la jeshi la malaika wa mbinguni from time to kuna baadhi ya malaika huwa wana defect na kumfuata shetani na hivyo hugeuka mashetani.

Vivyo hivyo kwenye jeshi la shetani kuna mashetani huwa wanatubu na kumrudia Mungu hivyo hurejea na kuwa malaika. Hawa sasa ni harmless kwa sababu ushetani wao wote wanakuwa wameuacha kule ushetanini!.

Lakini inapotokea malaika akaamua kufanya kazi ya shetani huku amepose kama malaika!, huyu ni hatari kuliko hata shetani mwenyewe!, maana you can't tell!. Watu wa Mungu watamsikiliza wakidhani ni malaika kumbe nje na ngozi tuu ndio ya malaika lakini ndani ni ibilisi mwovu shetani wahedi! .

Swali ni jee?, nani ni hatari zaidi kati ya shetani aliyetubu na kugeuka malaika au malaika aliyegeuka shetani kwa kufanya kazi ya shetani huku akiendelea kupose as malaika?!.

Tafakari na chukua hatua.

Nawatakia Jumatano njema.

Pascal
Hili swali japo ni la zamani lakini bado liko very valid.

Baada ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam kusema kazi ya U RC amepewa na Mungu, naungana naye ni kweli na hakuna yoyote wa kumtoa.
Vitendo vyovyote viovu huwa inspired na shetani, hata wizi ni kazi ya shetani, udanyanyifu ni kazi ya shetani, ukiweza kuiba cheti cha mtu, ukaiba jina la mtu, ukawasilisha vyeti hivyo bandia vya wizi kujipatia elimu ya juu, ulipohitimu ukapata kazi nzuri, ukateuliwa ukawa mkuu fulani, kisha sasa ukaachana na shetani na mambo yake yote, ukaanza kutenda matendo mema ya kusaidia watu, japo ulifanya mambo ya kisheni kufika hapo ulipo, hivyo bado ni Mungu alikupitisha mapito ya shetani ili baadea akupe deliverance na kumtumikia Mungu, wewe sasa unakuwa umezaliwa upya na kubatizwa upya, mtu yoyote akikuuliza yale ya shetani usimjibu kitu.

Mfano enzi za kumtumikia shetani uliitwa Daudi Albert Bashite, ulipozaliwa ukapewa jina la Daudi Bashite, ukasoma shule ya nsingi kama Daudi Bashite, ukasoma shule ya sekondari kama Daudi Bashite, ukapata Zero kama Daudi Bashite, shetani akamtumia Daudi Bashite kuiba cheti chá mmtu mwingine, ukiitwa Daudi Bashite, na sasa ukajibadili jina na kumtumia jina la cheti ulichoiba na kugeuka kuwa Paul Makonda, ukajiunga na chuo kama Paul Makonda, ni Mungu ndio aliokufanya ujiunge chuo, ni Mungu ndio aliokufa ukahitimu kama Paul Makonda, ni Mungu ndio aliokufanya ukateuliwa RC kama Paul Makonda, na sasa unafanya kazi ya Mungu kama Paul Makonda, mtu yoyote akikuuliza kuhusu Daudi Bashite usimjibu na ukiambiwa uonyeshe vyeti, onyesha vyeti vya Paul Makonda tuu! .

Hata Paulo mwanzo alikuwa Saulo, na hata Yesu alijaribiwa na shetani, hivyo Daudi Bashite alitumika tuu na shetani kumtengeneza malaika Paul Makonda.

Tumkatae shetani na mambo yake yote tuyakatae. Japo kumtumikia shetani ili kuja kuwa malaika ruksa.

Paskali.
 
Mkuu hii mada yako inachanganya. Malaika kugeuka Shetani ni hatari kwani hakuna asiyejua habari za Shetani na mambo yake. Tatizo ni hilo la pili la Shetani kugeuka Malaika; hili ni gumu kulijadili kwa sababu hatuna japo mfano mmoja. Malaika alishawahi kugeuka Shetani ndio maana leo tunazungumzia habari za Lusifa na mashetani wenzake.

Kwa upande mwingine, haijawahi kusikika au kuandikwa popote Shetani kugeuka Malaika - haipo. Hivyo, sina budi kusema kwamba mfono wako ni irrelevant na Shetani ataendelea kubaki Shetani milele yote.
Mkuu Dudus, natafakari tuu japo ni kweli haijawahi kuandikwa shetani kugeuka malaika, mtu yoyote aliyetenda mambo ya kishetani kama kuiba jina, kufoji vyeti!, kughushi halafu akafanikiwa na sasa kumrudia Mungu na kutenda mema ni sawa na shetani kugeuka malaika.

Paskali
 
Hii hadithi tu....Shetani na Malaika zake walishahukumiwa na hawana nafasi tena ya kutubu.....tafuta mfano unaokwenda na ukweli ....
Mkuu Mtazamo mfano uko valid kwa matendo mabayavya Daudi Bashite na mema ya Paul Makonda.

Paskali
 
Pasco,hata Mtakatifu Paulo alikuwa muuaji wa wakristu akiitwa SAULI,hivyo vyote vya wezekana kwa Mungu.Ila badala ya hii ya Shetani na Malaika.bora ungeiweka hii ya SAULI kuwa PAULI.

Pole Mungu ndiye ahukumuye kwa HAKI.

Kwa sasa nikipiga akili MASWALI ni mengi kuliko majibu.
Tetty hapo kwenye Sauli weka Daudi.
P.
 
Absolutely! This is relevant example. Binadamu hutubu na kugeuka sio Shetani. By the way, sijui kwa mfano wa Pasco Shetani ni nani na Malaika ni nani? Binadamu ni binadamu sio Shetani wala Malaika. Upotoshaji wowote ni lazima ukemewe kwa nguvu zote na kwa wakati.
Shetani ni bimadamu anayemtumikia shetani na Malaika ni bimadamu anayemtumikia Mungu.

Paskali
 
Mfano wa Shetan kujeuka Malaika,tunaipata kwenye kisa cha Sauli kwenye Biblia alie kuwa akiwaua watu wa Mungu,lkn cku 1 akiwa anaenda Dameski kutekeleza mauaji ya wakristo,ghafla njian alikutana na Mwanga mkali na Yesu akamwambia "Sauli Sauli Sauli Mbona waniudhi?
Kuanzia wakati huo Sauli alibadilika na akaacha ushetani wake na kuwa mcha Mungu akiwa anajilikana kwa jina la Paul, kiasi cha kifanya kazi ya Mungu kwa kiasi kikubwa kuliko hata mitume walio ishi na Yesu.
Vivyo ndivyo ilivyo kwa Daudi na Paulo.
P.
 
Eti umesema kuna mashetani wanatubu kwa Mungu alafu wanakua malaika tena???? Heheheh haitakaa ikatokea milele
ni kweli ila watu wa shetani ndio wanatubu na kuwa watu wa Mungu.
P.
 
Shetani akigeuka Malaika hakuwahi kuwa shetani huyo na malaika akigeuka kuwa shetani naye hakuwahi kuwa malaika! Malaika hawezi kuwa shetani na kinyume chake ni kweli vile vile. MMM
Hii ni kweli ila watu wao ndio wanatubu na kumrudia Mungu kwa kutenda mema.

P.
 
Mkuu Mtazamo mfano uko valid kwa matendo mabayavya Daudi Bashite na mema ya Paul Makonda.
Paskali
Ndugu yangu Pasikali (kwa sauti ya Mheshimiwa Raisi), Sasa unataka kuhalalisha UZURI wa shetani aliyebadilika kuwa malaika? Sawa.Tuseme tumekubaliana na hoja yako. Swali: Kwa mantiki hiyo unadhani zoezi la KUHAKIKI vyeti ni halali? Maana, chukulia kwa mfano, Rebeka Mafumu (jina la bandia- kama yupo wa kweli sikukusudia kumtaja kama mfano), alifeli kidato cha Nne. Akachukua cheti cha Kabula Kumalija (jina la bandia tena), akawa Nesi. Je, anakuwa Malaika (aliyetoka ushetanini) ndani ya Jina jipya? Je, uhakiki unaoendelea (ambao wengi tunausifu na kuushangilia) uachwe kisa Mashetani WAMEBADILIKA kuwa MALAIKA ndani ya majina mapya (ya kununua)? Hoja yangu ni hiyo ndugu yangu na rafiki yangu Pasikali....
 
Back
Top Bottom