Nani huyu anayepigwa hivi? Amekosa nini? Au ndio wasiojulikana?

Nani huyu anayepigwa hivi? Amekosa nini? Au ndio wasiojulikana?

Mheshimiwa Rais Samia, kama unapitia humu kusoma ni jambo jema. Lakini kama husomi na wasaidizi wako wana nia njema watakuletea hili swali.

Wewe kama Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania jee hawa wanao mtendea hivi Mtanzania mpiga kura wako na mlipa kodi ni askari wako?

Hii ni aibu kubwa sana kwa askari polisi wanaopaswa kulinda amani kufanya matendo ya aina hii kata kama huyo ni mhalifu.

Wao watakuwa na tofauti gani na vibaka na majambazi ya mjini? Kwani mbona wao wana access ya kumpeleka mahakamani mtuhumiwa kwa urahisi zaidi?

Tuliona maafisa wa uhamiaji wakichukuliwa hatua kwa matendo ya udhalilishaji hivyo tunategemea hawa wauaji wakichukuliwa hatua kali zaidi.

Hata IGP Sirro kama naye ataendelea kufumbia macho tabia hizi muwajibishe maana asikufikirie wewe ni kama yule aliyekuwa anahamasisha unyanyasaji

i
 
Ni nani huyu anaepigwa hivi? Amekosa nini? Kwanini wenye kumpiga wanasema "atatuharibia kazi" kazi gani? Na ame' post neno "kimeumanaaa" wapi? Ndiyo kosa lake? Anaefahamu kisa hiki atusaidie, tufahamu. Namba za gari ni T 777 BWS...
Ndio sababu chuki ya Raia kwa Polisi haitakuja kwisha.
 
Nyie mnaojidai sheria, natamani siku moja mkutane na hawa matapeli ndo mtaelewa...
Polisi ndio wanashauri hilo maana njia za kisheria hazifui dafu kwa watu wakorofi 😅 sheria inampa nguvu ya kurudi kitaa anapiga matukio sasa dawa yake ni kumgongelea msumari wa inch 6 utosini tu
 
Hapo mimi bora waniue vinginevyo itakua lawama lazima 1 pumbu ziwe halali yangu shenzi sana hata kama ni mhalifu bado anazo haki kama binadamu
 
Mbona video haifunguki?

Nikibonyeza tu najikuta Niko kwenye majukwaa tofauti tofauti..??
 
Hapo mimi bora waniue vinginevyo itakua lawama lazima 1 pumbu ziwe halali yangu shenzi sana hata kama ni mhalifu bado anazo haki kama binadamu
Lawama zipi mzee we pambana tu kiume ila ujue watakufirigisa vibaya mno kama huna skills za kupigana 😂😂😂 yani utarusha ngumi mbili 3 ila kinachofata wakikubana watakufirra
 
Nyie mnaojidai sheria, natamani siku moja mkutane na hawa matapeli ndo mtaelewa.
Hivi unafikiri wananchi hawaelewi kwamba kuna sheria? Unampeleka kwenye sheria baada ya siku mbili unamkuta street na anaendelea kutapeli kama kawaida. Ndo maana wananchi wamechoka wameamua kupiga tu.
Nikupe mfano, mtaani kwetu kuna kijana mwizi anaiba wizi wa kuvunja milango mchana, watu wamepeleka polisi anafungwa anatoka na akirudi uraiani anendeleza wizi. Sasa kuna mwezi Rais SSH aliwaachia jamaa kurudi kavunja geto la mtu. Polisi wametupa ruhusa sasa hivi mkimuona ueni Tuje tuchukue maiti
huyo jamaa anatapeli kwa mtindo gani?
 
Back
Top Bottom