Hii inanikumnbusha mbali sana..!!
Enzi hizo gheto kumetapakaa magazeti ya wasanii mbalimbali kama kina 2pac Shakur, Westlife na B.I.G hapa Bongo ndo kina Sugu, Dola Soul wanasumbua balaa, Ukienda gheto na mtoto akute room lilmepambwa namna hiyo we ndo mjanja wa mjini. Mitoko ilikuwa ni Mashati ya drafti na tisheti nyeupe chini ukivalia suruali yenye mifuko pembeni usawa wa magoti almaarufu kama Timbarland yaani we utaogopwa mtaa mzima. Siku ukitoka na Visuruali flani hivi vinaitwa vinyelamumo, almaarufu kama Bigmark, pembeni unakiredio chako cha mkononi almaarufu kama Walkman, Yaani we unasumbua mji balaaa..!!
Enzi hizo kina Prof J ndo wanachipukia na Hard brothers crew yao, Sugu anasumbua Nchi na kitu chake "Anamiaka chini ya kumi na nane," kila Barbershop utakayoingia ni Sugu Sugu Sugu enzi hizo akijiita Mr II. Kina LadyJd ndo wananusanusa, pembeni hivi kina King Creiz GK wanasogea kwa mbaaaaali daaah...!!! Kweli tunatoka mbali sana.
Mr II alikuwaga na mpaka kesho anakisauti flani hivi cha ki-hip hop haswa.. Anakitetemeshi flani hivi wakati wa kutema mashairi. Yaani enzi hizo mziki ulikuwa ni hizi tunazoita leo zilipendwa na hip-hop kwa pembeni wakisindikizwa na Taarab kidogo. Na hiphop ilikua ni hiphop haswa, siyo kama leo wasanii wa hip-hop wanavisha pua zao vidani na kutoga masikio huku wakisindikizia na kusuka nywele na full make up..!!! Huu mziki ulikuwa wa wagumu kweli kweli.. Akaja jamaa mmoja hivi ambaye alishawishiwa na hawahawa kina Sugu kurudi kufanya mziki Bongo na si kung'ang'ania USA, huyu jamaa alikuwa akiitwa Cool James mtoto wa Dandu (Rip) ndiye mwasisi wa hizi tuzo za KTMA alitoa wazo la kuanzishwa kwa tuzo hizo (siyo KTMA) sijui aliziitaje. Bahati mbaya kabla hazijaanza rasmi akafa kwa Ajali.
Kipindi hicho mziki wa kunakili miziki ya wakongwe ilikuwa ikitamba haswa na style hii ndiyo iliyomtoa Mr Paul, aliimba wimbo wa Zuwena wa Mariajan Rajab. Hivi wakuu
Matola,
Deo Carlione na
Ruttashobolwa mlikuwa wapi enzi hizo, Mnakumbuka nini?
Halafu kwa kumbukumbu zenu mnaweza kukumbuka mwanamziki wa kwanza kuanza mziki wa kuimbaimba (Siyo Kughani mashairi) almaarufu kama Bongofleva? Note, ninaposema Bongofleva R&B weka pembeni.. Tukumbushane wadau..
BACK TANGANYIKA