Nani kasema Nguruwe halali? Sio Ukristo au Uislamu kote wamemkana.

Anzia
Anzia 10:1-16
 
Ila huyo limdudu libaya limekaa vibaya sana nilikuwa narafiki yangu msabato tukiendaga mnadani huwa wanachinjwa anamchukia vibaya. Mambo mengine ni uroho tuu wa nafsi kula vitu vya ovyooo[emoji23][emoji3][emoji3]
 
Hata muuza bangi naye huwa mkali linapoharibiwa soko la bangi yake, lakini bangi itabaki kuwa haramu tu jinsi kitimoto kilivyokuwa haramu na najisi.


Wasabato ni Waisilamu au Wakristo???
Nimekuuliza hivi Wasabato ni watu?
 
Ifike muda tu ukubaliane na ukweli kwamba pilipili za shamba wewe zisikuwashe hata kidogo.

Huyu mnyama mnapenda sana kumzushia kashfa na kila aina ya majungu ila penzi analotupa na utamu wake katika tasnia ya msosi halikwepeki na ni ngumu sana kututenganisha nae.

Hebu acheni kumsema my wetu.
 
Mhu! Yesu alifundisha kwamba "hakuna kimwingiacho mtu kutoka nje kinaweza kumfanya awe najisi. Bali kitokacho ndani mwake kama vile mawazo mabaya, maneno mabaya nk. Na kwa kusema hivyo alihalalalisha vyakula ambavyo watu waliamini wakivila vinawafanya wawe najisi.
 

Nitamla tu
 
16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

18 Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;

19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.

20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,

21 Msishike, msionje, msiguse;

22 (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?

23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…