Munch wa annabelletz47
JF-Expert Member
- Aug 13, 2019
- 1,885
- 3,227
- Thread starter
- #321
Anzia
Anzia 10:1-16Matendo ya Mitume 10
9 Siku ya pili yake, walipokuwa wameukaribia mji, wakati wa adhuhuri, Petro alipanda juu ya nyumba kuomba. 10 Alipokuwa akiomba akahisi njaa, akatamani kupata chakula. Lakini wakati walikuwa wakiandaa chakula, akalala usingizi mzito sana. 11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. 12Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. 13Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”
14 Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”
15 Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”
16Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni.