Mshamba nn huyo Msami nan ambaye hamjui?
Usifuate mkumbo soma nilichoandika hapo kwanza ,nimekuambia mbele ya Mose iyobo ...Mose iyobo ni bingwa wa style na zinabamba kitaa Msami ni mzuri kwa kucopy hana style zinzobamba Mfano chukulia nyimbo ya "Nana" ya diamond kaangalie ile style bado kuna My number one hizo ni style katoa Mose iyobo .
Nipe style ya Msami hana lolote nanq asiyemjua ....Twende kweny tunzo sana!?
Mkuu Tunatatizo kubwa sana la kulinganisha ubora bila kuangalia era
Ubora wa mtu unapimwa kwenye era yake(yaani walikua wanatumia style gani na alikua bora kiasi gani kwenye hiyo hizo style)
Hadi leo Michel Jackson anaheshimika kama mwimbaji na dancer bora kabisa kuwahi kutokea duniani, lakini kwa kizazi cha sasa kuna watu wanacheza hadi unaogopa na kuona Mbona Jackson cha mtoto?
Ukirudisha wakina maradona na pele kwenye peak yao dunia ya leo watasugua benchi sana tu kwa matakwa ya makocha na mpira wa kileo, wanatakiwa wakina Haland game nzima ana touch 6 magoli mawili lakini wakina maradona wanapiga chenga uwanja mzima[emoji23]
Msumi enzi yake alifanya alichofanya Chino...... Ali dance sana na akaja kuwa muimbaji akavuma sana tu
Na enzi hizi mziki wetu ulikua mdogo sana mambo ya tuzo za dancer hayakuwepo kivile kama sasa
Sasa hivi Msumi amebaki kuwa mwalimu mzuri sana, video nyingi za muziki unazoziona za akina Nandy, Maua Sama na wasanii wengi waliopitia THT ni kazi ya Msumi kwenye dancing
Chino ni mzuri kwa era yake ya sasa lakini naamini hamfiki Iyobo sema ni vile uimbaji umemtoa zaidi na kumfanya maarufu zaidi
Ila kwenye kucheza tu iyobo ni balaa kwenye era yao
Kwenye huu ulimwengu wa ku TREND ukipigisha kura lazima Chino atashinda tu, kuna watu watampenda tu hata hawajawahi kuona akicheza ila trend ya nyimbo zake na ile signature yake kwenye nyimbo zake “Chinowanaman” inavutia sana aiseee