Nani mkali wa Pasi kati ya Kevin De Bruyne Vs Lionel Messi?

KDB akipiga pasi hesabu yake inaonekana wazi, namna alivyojipinda, nguvu anayoikadiria with accuracy, nk... Ukifanyia mazoezi unaupata uwezekano.

Messi haijulikani mpira unatokaje miguuni mwake na unafikiaje kwa mlengwa, ila tu unafika. Hata ufanyie mazoezi vipi, hutajua inawezekanaje. Ni kama anadanganya, ila ndio yanafanyika kweli.
Sahii kabisa,
miguu ya Messi iko sharp Sana,
Akishika mpira hatabiriki atafanya nn.

Unahisi Kama anapiga chenga akupite,kumbe anakusanya Kijiji muache nafas atoe pasi[emoji4]
 
Messi zama zake zilishapita, kwa sasa KDB ni top. Lakini hata kwa hizo zama zake Messi hakuwa Best. Xavi, Iniesta, Ozil
 
KDB pasi zake zinaitwa "chukua hiyooo". Anaepokea pasi anajikuta akisema, "jamaa anajua"

Messi pasi zake zinaitwa "ushindwe mwenyewe tu". Anaepokea pasi anajikuta akiwaza, "Oya huu mpira umenifikia vipi mazee?"

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Messi kwenye suala la pasi, anaweza kupambanishwa na wenzie aliopita nao La Masia.

  • Xavi Hernandez
  • Andres Iniesta
  • Thiago Alcantara
  • Cesc Fabregas
  • Sergio Busquets

Tofauti na La Masia, nadhani ni Mesut Ozil pekee ndio anaweza kubattle na Messi kwenye hiyo sekta!
 
Wasalaam,

Kevin De Bruyne na Lionel Messi ni wachezaji wawili wenye vipaji vya kipekee katika soka na wote wawili wanajulikana kwa ustadi wao wa kupiga pasi. Hata hivyo, wana mbinu tofauti za kucheza na kuandaa pasi.

Kevin De Bruyne, ambaye ni kiungo wa kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji, ana uwezo mkubwa wa kuona nafasi na kutoa pasi za kina. Ana udhibiti mzuri wa mpira na ufahamu wa hali ya wachezaji wenzake uwanjani. De Bruyne anajulikana kwa uwezo wake wa kutoa pasi za kuunganisha na pasi ndefu zinazovunja ngome ya timu pinzani. Yeye ni mtaalamu wa kubuni na kuandaa nafasi kwa wachezaji wenzake.

Lionel Messi, ambaye ni mshambuliaji na alikuwa akiichezea Barcelona, sasa PSG, na timu ya taifa ya Argentina, ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee. Yeye ni mtaalamu wa kupenyeza katika ngome ya timu pinzani na ana uwezo mkubwa wa kuunda nafasi za hatari. Messi ana udhibiti mzuri wa mpira na kasi ya ajabu, ambayo humruhusu kupenya katika safu ya ulinzi na kutoa pasi za kushtukiza ambazo mtu anamalizia kwa kuweka tu mguu.

Vivo hivo Messi ana uwezo mkubwa sana wa long ball na penetration passes kwahyo ameshacheza sana kama midfield deep kabisa.

Kati ya hao wawili nani ni Maestro akiikamia Midfield na anapiga pasi hatari??
Simpendi Messi ila mmemdhalilisha sana kumfananisha na upuuzi, KD hafikii hata kwa S. Fabregas.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Wasalaam,

Kevin De Bruyne na Lionel Messi ni wachezaji wawili wenye vipaji vya kipekee katika soka na wote wawili wanajulikana kwa ustadi wao wa kupiga pasi. Hata hivyo, wana mbinu tofauti za kucheza na kuandaa pasi.

Kevin De Bruyne, ambaye ni kiungo wa kati wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji, ana uwezo mkubwa wa kuona nafasi na kutoa pasi za kina. Ana udhibiti mzuri wa mpira na ufahamu wa hali ya wachezaji wenzake uwanjani. De Bruyne anajulikana kwa uwezo wake wa kutoa pasi za kuunganisha na pasi ndefu zinazovunja ngome ya timu pinzani. Yeye ni mtaalamu wa kubuni na kuandaa nafasi kwa wachezaji wenzake.

Lionel Messi, ambaye ni mshambuliaji na alikuwa akiichezea Barcelona, sasa PSG, na timu ya taifa ya Argentina, ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee. Yeye ni mtaalamu wa kupenyeza katika ngome ya timu pinzani na ana uwezo mkubwa wa kuunda nafasi za hatari. Messi ana udhibiti mzuri wa mpira na kasi ya ajabu, ambayo humruhusu kupenya katika safu ya ulinzi na kutoa pasi za kushtukiza ambazo mtu anamalizia kwa kuweka tu mguu.

Vivo hivo Messi ana uwezo mkubwa sana wa long ball na penetration passes kwahyo ameshacheza sana kama midfield deep kabisa.

Kati ya hao wawili nani ni Maestro akiikamia Midfield na anapiga pasi hatari??
Leo Messi ni complete package. Anakupa kila kitu kuanzia pasi, dribbling, mpaka kufunga
 
Back
Top Bottom