Kwanza hakuna wakati ambapo NEC walisema kuwa walipokea majina toka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA baada ya kupitishwa na Kamati Kuu. Hili umelisema wewe.
Ninachokumbuka ni kuwa NEC wametoa kauli 2 zinazotofautiana. Kwanza walisema kuwa hawajapokea jina lolote toka CHADEMA. Nadhani kauli hiyo aliitoa mkurugenzi wa NEC tarehe 23 Novemba.
Spika anasema alipokea majina toka NEC tarehe 20 Novemba. Mpaka hapo, au Spika au Mkurugenzi wa NEC, mmojawapo ni mwongo, au wote ni waongo.
Tatu mpaka sasa, NEC wanasema walipokea majina toka CHADEMA, lakini hawataji mtu aliyewapelekea, na hawasemi ilikuwaje tarehe 23 Novemba NEC iwe haijapokea majina halafu Spika awe amepelekewa majina na NEC tarehe 20 Novemba!!
Kwa mwenye akili timamu, hahitaji kujiuliza ni nani mwongo. Waongo na hawa wawili, Mahera na Ndugai.
Sent using
Jamii Forums mobile app