Uchaguzi 2020 Nani mkweli kati ya hawa watu? Spika, NEC au CHADEMA?

Uchaguzi 2020 Nani mkweli kati ya hawa watu? Spika, NEC au CHADEMA?

Wao wanasema hawajapeleka. Sasa kwa nini NEC wasiwaumbue kwa kuweka wazi barua walioipata tarehe 19 lakini tarehe 20 walisahau kuwa wanayo.

Amandla...
Tuombe mahakama ifunue ukweli juu ya hii barua.
 
Siasa bongo kama ushabiki wa simb na yanga tu
 
Sioni sababu ya kwenda mahakamani. CHADEMA impelekee tu Spika barua kuwa CC imewavua uanachama hao wabunge wao.

Kama katiba inaruhusu mbunge kutokuwa na chama chochote kilichomdhamini, hilo ni la hawa walioufanya huu uchafu. Huu uchafu umeshirikisha Serikali nzima pamoja na mihimili ambayo imewekwa mfukoni mwa serikali.

CHADEMA isikpoteze muda na wala isithubutu kwenda mahakamani. Siku zote adui yako haweza kukuelekeza njia ya kupita salama. Huko mahakamani, kwa kuwa nao ni mhimili uliowekwa mfukoni mwa mtawala, watakuwa wamewaandaa watu wao. Mkienda tu huko, hawatataka mliongelee suala hilo kwa maelezo kuwa suala lipo mahakamani. Na pia mahakama hii iliyopo mfukoni mwa Serikali itatumika kumsafisha spika, NEC ha wote walioshiriki kwenye uchafu huu.

CHADEMA wakishapeleka barua kumtaarifu spika, wamemaliza. Akina Mdee wakiendelea kuwa wabunge, ni sawa tu. Watakuwa wabunge maalum wa Kongwa na Chattle.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nec inatakiwa ipewe barua kuwa sio wabunge,kisha Nec imtaarifu spika. Lakini all in all mtu akikosa sifa ya kuwa mwanachama wa chama kilichomdhamini anakosa ubunge. Japokuwa taratibu za kimaamdishi zinatakiwa kufuatwa.
 
Chadema wanasema hawakupeleka majina NEC,nani alipeleka?

NEC wanasema Mnyika kama katibu mkuu aliwapelekea majina tena yaliyopewa baraka na kamati kuu ya Chadema. Hii ni kweli au sio kweli?

Spika anadai hawezi kuvua ubunge wabunge ambao kwa mujibu wa katiba ya JMT sasa hivi hawana chama maana walishatimuliwa Chadema. Kisa tu NEC ya Wilson Mahera ilimpa majina. Ok kama NEC ilimpa majina bado wanasifa za kuwa wabunge kama ibara ya 67(b) na 71(e) inavyoweka wazi?

Au ndio kusema undavaundava tu hata kwenye mambo ya kuzingagia Katiba na sheria?

Chadema wanaweza kuupa ukweli umma wa watanzania ili tujue nani alipeleka majina? Nahisi kuna jinai inanukia, kama haipo kuna mtu mkubwa Cdm mpenda dili anahusika,Tanzania nzima inamfahamu.
Kwani chadema wamesha muandikia spika official latter kumjulisha kuwa wamefukuzwa uanachama? Au ni yale matamshi tu.
Kwa matamshi tu bado hawajafukuzwa kisheria kwa spika.
Hayo yatakuwa kama ya lipumba.
Kama wako serious kweli na huo ubunge wa hao wamama, wamwandikie spika barua ya kutowatambua,na nyingine wapeleke kwa msajiri na tume ya uchaguzi ndo tutajua hawakuwatuma.
 
Hivi unadhani kwamba CHADEMA hawajui wanachokifanya?

Sidhani kama wanaingia mtegoni ila ni mbinu ya kuhakikisha kwamba hili jambo linaisha kwa Baraka za Mahakama kwamba Wabunge ni halali au la, ila uwezekano upo mkubwa sana kwamba mahakama itasema ni halali, na hatimaye mjadala kufungwa ili kuepusha 'mihimili kugongana'😀
Haahaa 5 years kesi itadumu.chadema kujua Sana tatizo.
 
Kwani chadema wamesha muandikia spika official latter kumjulisha kuwa wamefukuzwa uanachama? Au ni yale matamshi tu.
Kwa matamshi tu bado hawajafukuzwa kisheria kwa spika.
Hayo yatakuwa kama ya lipumba.
Kama wako serious kweli na huo ubunge wa hao wamama, wamwandikie spika barua ya kutowatambua,na nyingine wapeleke kwa msajiri na tume ya uchaguzi ndo tutajua hawakuwatuma.
Ushauri mzuri.
 
Utakuwa umepoteza memory, katibu mkuu wa NEC alisema walipokea majina tar 19 Nov. Wewe una uhakika gani? Kuwa Mahera na Ndugai waongo. Ikithibitika kuna mtu wa Cdm alipeleka majina?
Ukumbuke kuwa Mtendaji Mkuu wa NEC, tarehe 23 alisema hawajapokea majina toka CHADEMA. Tarehe 23 ni kabla au baada ya tarehe 19?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli gani? Wakweli wenye wabunge wao chadema
Defence ya spika mpaka sasa ni kuwa Chadema walipeleka majina Nec,Nec wakampatia Spika. Hivyo bado anawatambua kuwa ni wabunge. Sasa nani alipeleka barua Nec?
 
ingekuwa hivyo wasingeogopa kwenda kamatimkuu; wangeenda na kukinukisha kwa Katibu mkuu, Na je nguvu iliyovunja milango ya gereza ni ya chadema?
Sijasema direct kwamba Mnyika, mbowe or Tundu ndo watakao kuwa wamepeka majina. Nachozungumza mimi majina yamepelekwa na CDM wenyeewe yaweza kuwa ni hata mdee mwenyewe, point ya msingi je signature ya KM wameipataje, may be hao hao waliopeleka majina wamefoji hadi signature ya mnyika
 
Sijasema direct kwamba Mnyika, mbowe or Tundu ndo watakao kuwa wamepeka majina. Nachozungumza mimi majina yamepelekwa na CDM wenyeewe yaweza kuwa ni hata mdee mwenyewe, point ya msingi je signature ya KM wameipataje, may be hao hao waliopeleka majina wamefoji hadi signature ya mnyika
Kuna mtu mmoja hapo Chadema mzee wa madili anahusika.
 
Back
Top Bottom