Sioni sababu ya kwenda mahakamani. CHADEMA impelekee tu Spika barua kuwa CC imewavua uanachama hao wabunge wao.
Kama katiba inaruhusu mbunge kutokuwa na chama chochote kilichomdhamini, hilo ni la hawa walioufanya huu uchafu. Huu uchafu umeshirikisha Serikali nzima pamoja na mihimili ambayo imewekwa mfukoni mwa serikali.
CHADEMA isikpoteze muda na wala isithubutu kwenda mahakamani. Siku zote adui yako haweza kukuelekeza njia ya kupita salama. Huko mahakamani, kwa kuwa nao ni mhimili uliowekwa mfukoni mwa mtawala, watakuwa wamewaandaa watu wao. Mkienda tu huko, hawatataka mliongelee suala hilo kwa maelezo kuwa suala lipo mahakamani. Na pia mahakama hii iliyopo mfukoni mwa Serikali itatumika kumsafisha spika, NEC ha wote walioshiriki kwenye uchafu huu.
CHADEMA wakishapeleka barua kumtaarifu spika, wamemaliza. Akina Mdee wakiendelea kuwa wabunge, ni sawa tu. Watakuwa wabunge maalum wa Kongwa na Chattle.
Sent using
Jamii Forums mobile app