Nani wa kumfungia kiongozi wetu Speed Governor? Nchi itapigwa mnada hii

Nani wa kumfungia kiongozi wetu Speed Governor? Nchi itapigwa mnada hii

Umejitahidi sana kuwaelewesha Watz waliojipa Cheo Cha " Chawa", ingawa Nina HAKIKA, hayupo atakayekuelewa..
Mara nyingi watu wanafikiri tuna chuki na serikali na ni chama fulani. Kuna wengine hata sio wanachama wa chama chochote. Tunahitaji kuona nchi inafanikiwa. Tumepewa amri ya kuumbea mji amani maana katika amani yake na sisi tutapata amani. Hii ni pamoja na mafanikio yetu. Yamefungwa pamoja tuwe wenye chama na tusio na chama.
 
USA ya Biden ni taifa moja kubwa sana mipango yao ni tofauti na ya nchi za kiafrika.

Unapomkejeli SSH kumbuka wamekwenda Korea marais wengi tu wa afrika.
Nani kasema kuna shida ya kwenda Korea?.
Katika dunia hii hakuna kitu kinachoitwa Mkopo wa Masharti nafuu.
Neno Masharti nafuu ni kauli ya kisiasa hio.
 
Kwa huyu bi Mkubwa ni suala la muda tu keep my comment.
Mimi sihadithiwi wewe nyumbu.Serikali isiyo na hela haiwezi tangaza maelfu ya Ajira Mpya Kila mwaka.

Huo ujinga nenda Kwa wajinga wenzako.Bajeti ya Nchi tuu imetoka wastani wa Trilioni 35 Leo hii tuko Trilioni 50 unaongea upuuzi.

TRA imetoka kukusanya Trilioni 18 mwaka 2021 Leo hii 2024/24 tuko Trilioni 27.

Kwenye Suala la maendeleo Samia halinganishwi na kima yeyote hapa Tanzania
 
Nani kasema kuna shida ya kwenda Korea?.
Katika dunia hii hakuna kitu kinachoitwa Mkopo wa Masharti nafuu.
Neno Masharti nafuu ni kauli ya kisiasa hio.
Ndio umeshatolewa tena huo mkopo ni haki yako kuyaamini maelezo ya Waziri au kutoyaamini.
 
Hatua za haraka zichukuliwe kuokoa jahazi kuzama.
 
Salaam, Shalom!!

Nchi yetu ni maskini, na Umaskini wetu ni WA matumizi ya akili katika kuzitumia vizuri raslimali na kuzibadili raslimali kuwa utajiri.

Niliwahi kuhoji kuwa, dhamana ya mikopo anayokopa kiongozi wetu ni nini Hasa?

Speed katika kukopa ni kubwa sana, ni Kweli tunahitaji pesa Kwa ajili ya kumalizia miradi iliyoanzishwa na Hayati Magu lakini tunahitaji kufanya Utafiti mikopo iliyokopwa tulinganishe na KAZI mikopo hiyo imefanya tupate balance!

Ikiwa tunakopa na wizi unafanyika, pesa zinaibwa na hazitimizi kusudi Kisha tunarudi tena kukopa, hii Hali ni Hadi lini?

Nani wa kumfunga kiongozi wetu Speed Governor kuhusu mikopo?

Iweje Nchi ikope vijipesa kiduchu vya mboga Kwa kubadilishana na Raslimali zenye thamani mara elfu zaidi ya mikopo hiyo?

Ikiwa Bunge limeshindwa kumdhibiti Kiongozi wetu kutukopea bila kutuuliza, ni nani atazuia au kumshauri vizuri kuhusu mikopo yenye TIJA?

Mh Ndugai akiwa Spika wa bunge, alishindwa kumfunga kiongozi huyu speed governor, Nani ataweza?

Hivi Trillion 2 ni pesa ya Kugawa migodi yetu?

Trillion Moja ni pesa ya kuwapa wageni kufanya UVUVI deep sea? Kwanini tusiwadhamini wavuvi kupitia kampuni za wazawa wanunue Meli kubwa kufanya UVUVI huko deep sea tuexport nje Samaki🤔???

Swali: Njia Gani wananchi tuzitumie kumzuia kiongozi wetu kukopa pesa kiduchu Kwa Kugawa Ardhi, misitu, Bandari na Bahari, raslimali ambazo ni thamani yake ni kubwa kuliko vipesa anavyokopa Kisha vinaishia kuibwa?

Karibuni🙏

Pia soma Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea
Mama Samia sio visionary leader ndio maana amezungukwa na small minds kama kina january makamba na nappe ndio anawasikiliza. Nchi za kibeberu wana wenye akili sana kuhakikisha nchi zetu zinabaki hapo zilipo kimaendeleo kwa faida yao. Na wamesema hivyo halafu utakuta kiongozi anaenda kukopa ovyoovyo na kupokea mipango yao kama ndio mipango yetu. Hebu fikiri mtu anamtoa mtu kama pofesa aidan mwaluko mtu mweledi wa wa sheria na mahusiano ya kimataifa na yule Phd holder Kalimani aliyekua waziri wa nishati unaweka wababaishaji uwaziri. Yaani tukifanya makosa mwakani nchi itauzwa yote dubai nawaambieni. Mama atakua ameitendea nchi jambo ikiwa badala ya kung'ang'ania asaidie wanaccm kupata mtu aina ya magufuli. Hapo tutamkumbuka kabisa mama.
 
Mama Samia sio visionary leader ndio maana amezungukwa na small minds kama kina january makamba na nappe ndio anawasikiliza. Nchi za kibeberu wana wenye akili sana kuhakikisha nchi zetu zinabaki hapo zilipo kimaendeleo kwa faida yao. Na wamesema hivyo halafu utakuta kiongozi anaenda kukopa ovyoovyo na kupokea mipango yao kama ndio mipango yetu. Hebu fikiri mtu anamtoa mtu kama pofesa aidan mwaluko mtu mweledi wa wa sheria na mahusiano ya kimataifa na yule Phd holder aliyekua waziri wa nishati unaweka wababaishaji uwaziri. Yaani tukifanya makosa mwakani nchi itauzwa yote dubai nawaambieni. Mama atakua ameitendea nchi jambo ikiwa badala ya kung'ang'ania asaidie wanaccm kupata mtu aina ya magufuli. Hapo tutamkumbuka kabisa mama.
Hana uwezo kutuletea kiongozi tumtakaye,

Yeye apumzike,

Wananchi tunamjua tumtakaye 2025.
 
Kila Mhe. Mbunge anapoanza kuzungumza ni slogan ni ile ile. Mhe. Rais kaleta pesa nyingi na miradi inaendelea. Pesa karibu zote zinazotekeleza miradi nchi hii ni fedha za mikopo toka nje. Kwa nini tutambe na fedha za mikopo inayotekeleza miradi kutoka nje. Lini tutajisimamia sisi wenyewe na kutamba kuwa fedha zetu za ndani ndo zinatekeleza miradi?. Tusitambe kwa sababu hiyo miradi inayotekelezwa fedha zake ni madeni na tutakuja kulipa. Tutafute njia ya sisi kujisimamamia wenyewe.
 
Back
Top Bottom