Nani yupo nyuma ya Uhuni huu kwa Sabaya?

Alitanua mno kwa kutumia vibaya madaraka yake, sasa ni muda wake muafaka wa kujutia yale yote aliyoyatenda akingali hai.
 
Jana tuliambiwa hukumu ya kesi iliahirishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi, Arusha.

kwa kile kilichodaiwa kuwa hakimu alikuwa anatimiza majukumu mengine ya kiofisi,mahali ambapo hatukutajiwa.

Leo asubuhi tunasikia taarifa ya Sabaya kuhamishiwa alfajiri,kutoka Gerezani Kisongo,na kupelekwa Mkoa mwingine kwenda kufunguliwa mashitaka mengine.

Anapelekwa Gereza lingine na Mkoa mwingine bila hata taarifa za Removal Order ya mahakama kutolewa.

Pia mshitakiwa huyu alieko chini ya ulinzi kama Mahabusu,huko Kisongo,anahamishiwa mkoa mwingine bila hata wakili wake kupewa taarifa.

Huyu mtu sio mfungwa kwa sasa bali Mahabusu.
Tena ambaye hukumu yake ni mwezi wa sita huu siku ya tarehe 10.

Halafu amehamishwa kwenda mkoa mwingine,na kusomewa mashitaka ambayo hata hajawaji kuhojiwa au kutakiwa kutoa maelezo yake na vyombo husika hapo awali.

Je!
Anachokihubiri Rais Samia na yale yanayoendelea kwa watendaji wake vinafanana?

Je!
Ni nani yuko nyuma ya hii Project Sabaya?

Katika kesi aliyoachiwa huru tulisikia tuhuma za kaimu DPP Kweka.
Ambaye alihusishwa na Familia ya Mbowe kama mkwe wake.
Akihamishia makazi kwa muda pale Arusha kwa kuisimamia kesi ile.

Sasa tunalazimika kuamini kwamba haya mambo yamerudi na yanashamiri kwa kasi.

Time will Tell!

Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni.

View attachment 2247466
Kama ilivyokuwa kwa Manji alivyomwambia Mtu kuwa haongei na Mbwa bali na mwenye Mbwa na Mbwa akwatwaa nchi ndivyo ilivyo pia kwa Sabaya ambapo mwaka Juzi alimuita Mtu 'yupo yupo' alipoenda Ziarani Kilimanjaro na bahati nzuri kwa tusiompenda na mbaya Kwake ni kwamba 'Yupo Yupo' yupo kweli sasa na anaupiga mwingi ile mbaya Kudadadeki.
 
Utavuna ulichopanda...hakuna uhuni hapo. Acha sheria zifate mkondo
sabaya ni muhuni aliyeamini kwamba mungu wake magufuli angeishi milele,
sabaya huyu aliyeua na kutesa watu leo anaonewa huruma bila kujali madhira aliyowasababishia watu wengine. ama kweli dunia shujaa.
sabaya huyu alipenyeza simu gerezani kisongo kwa kuwahonga maafisa magereza leo anaonewa huruma.
jana alimuomba raisi amsaidie kwakuwa ni mambo ya kisiasa?
sabaya anataka kutuambia kwamba siasa ni uhasama unaoweza kumpeleka mtu mahakamani? tujiulize wapo wakuu wa wilaya wangapi na mbona hawapelekwi mahakamani? sabaya ana nini cha mnoo?
tu kwakuwa alikuwa hai? siyo kweli lazima kuna mambo aliyafanya kinyume na utu.
acha akione
 
Uhalifu ambao mahakama imeshindwa kuuthibitisha.
imeshindwa kuuthibitisha mbona alifungwa? zile ni technicalities tu mkuu. hata babu seya ali lawiti watoto, kama kawaida yetu watanzania tukagawanyika na kusema ameonewa sijui kisa alitembea na nani na upuuzi mwingine wa kitoto kabisa
mtu awapigilie watu misumari miguuni na kuwakata masikio kisha atokee mpuuzi kama ASEME ANAONEWA INAKERA SANA
 
Hata Sabaya binafsi leo ameitamkia mahakamani kwamba hana imani na Kweka.
Sasa wewe ndie unaendekeza unyumbu bila facts.
Hana authority ya kuipangia ofisi ya dpp timu ya watenda kazi la msingi atulie Kama alivyokuwa anapanga mission zake za wizi!
 
Yaani kuna nguchiro zina tetea ule uovu ulio fanywa na uyo bwana 7ya?
 
Kama ilivyokuwa kwa Manji alivyomwambia Mtu kuwa haongei na Mbwa bali na mwenye Mbwa na Mbwa akwatwaa nchi ndivyo ilivyo pia kwa Sabaya ambapo mwaka Juzi alimuita Mtu 'yupo yupo' alipoenda Ziarani Kilimanjaro na bahati nzuri kwa tusiompenda na mbaya Kwake ni kwamba 'Yupo Yupo' yupo kweli sasa na anaupiga mwingi ile mbaya Kudadadeki.
Wengi wanaweza wasikuelewe GENTAMYCINE lakini umeandika jambo muhimu na lenye ukweli fulani hivi.

Sasa tunaweza kuelewa hata kiini cha upandishwaji cheo wa yule afisa wa Polisi kwenda kule Juu.

Mimi hapo ndio maana huwa sizipiti Nyuzi zako humu bila kuzisoma kwa umakini.
Umemaliza kila kitu.
 
Yaani kuna nguchiro zina tetea ule uovu ulio fanywa na uyo bwana 7ya?
Mshitakiwa huwa haipangii mahakama bali anaweza wakataa baadhi ya watendaji kwa kutokuwa na Imani nao.

Kama MBOWE alivyokuwa akifanya kwenye kesi ya ugaidi wake.
 
imeshindwa kuuthibitisha mbona alifungwa? zile ni technicalities tu mkuu. hata babu seya ali lawiti watoto, kama kawaida yetu watanzania tukagawanyika na kusema ameonewa sijui kisa alitembea na nani na upuuzi mwingine wa kitoto kabisa
mtu awapigilie watu misumari miguuni na kuwakata masikio kisha atokee mpuuzi kama ASEME ANAONEWA INAKERA SANA
Babu Seya aliponzwa na mke wa aliekuja kuwa mke wa mkuu.
Wewe wala hujui kitu.

Hao waliopigiliwa misumari na kukatwa masikio.
Wewe binafsi ulikwishawaona au stori za BAVICHA pale Hai?
 
Babu Seya aliponzwa na aliekuja kuwa mke wa mkuu.
Wewe wala hujui kitu.

Hao waliopigiliwa misumari na kukatwa masikio.
Wewe binafsi ulikwishawaona au stori za BAVICHA pale Hai?
nilijua ungefika kwenye BAVICHA na kuacha facts nyingine zoote. Jiulize kwanza sabaya ni nani mpaka a
 
sabaya ni muhuni aliyeamini kwamba mungu wake magufuli angeishi milele,
sabaya huyu aliyeua na kutesa watu leo anaonewa huruma bila kujali madhira aliyowasababishia watu wengine. ama kweli dunia shujaa.
sabaya huyu alipenyeza simu gerezani kisongo kwa kuwahonga maafisa magereza leo anaonewa huruma.
jana alimuomba raisi amsaidie kwakuwa ni mambo ya kisiasa?
sabaya anataka kutuambia kwamba siasa ni uhasama unaoweza kumpeleka mtu mahakamani? tujiulize wapo wakuu wa wilaya wangapi na mbona hawapelekwi mahakamani? sabaya ana nini cha mnoo?
tu kwakuwa alikuwa hai? siyo kweli lazima kuna mambo aliyafanya kinyume na utu.
acha akione
Ni kweli Wakuu wa wilaya walikuwa wengi, Lakini hakuna aliyemsababishia MBOWE kupoteza kiti cha Enzi alichokwishakiona kama chake maisha yote Bungeni.
Zaidi ya SABAYA

Sabaya ni Mkuu wa wilaya pekee aliyethubutu kupambana na wezi na watengenezaji Pesa Bandia nyumbani kwao kabisa Jimboni Hai.
 
Sabaya ni mpuuzi km wapuuzi wanaomtetea,ameumiza na kuua wengi achanae achimbe kidogo mpumbav sana yule,he deserves a great neck mathet.
 
Hakuna sheria iliyofuatwa hapo.
Na hayo ndio makosa ambayo yalisababisha akaachiwa huru.
Na sasa yatajirudia tena.
Unayetetea muovi nawwe ni walewale tu. Ukitenda uovu majibu hapahapa ulimwenguni, na kinyume chake
 
Jana tuliambiwa hukumu ya kesi iliahirishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi, Arusha.

kwa kile kilichodaiwa kuwa hakimu alikuwa anatimiza majukumu mengine ya kiofisi,mahali ambapo hatukutajiwa.

Leo asubuhi tunasikia taarifa ya Sabaya kuhamishiwa alfajiri,kutoka Gerezani Kisongo,na kupelekwa Mkoa mwingine kwenda kufunguliwa mashitaka mengine.

Anapelekwa Gereza lingine na Mkoa mwingine bila hata taarifa za Removal Order ya mahakama kutolewa.

Pia mshitakiwa huyu alieko chini ya ulinzi kama Mahabusu,huko Kisongo,anahamishiwa mkoa mwingine bila hata wakili wake kupewa taarifa.

Huyu mtu sio mfungwa kwa sasa bali Mahabusu.
Tena ambaye hukumu yake ni mwezi wa sita huu siku ya tarehe 10.

Halafu amehamishwa kwenda mkoa mwingine,na kusomewa mashitaka ambayo hata hajawaji kuhojiwa au kutakiwa kutoa maelezo yake na vyombo husika hapo awali.

Je!
Anachokihubiri Rais Samia na yale yanayoendelea kwa watendaji wake vinafanana?

Je!
Ni nani yuko nyuma ya hii Project Sabaya?

Katika kesi aliyoachiwa huru tulisikia tuhuma za kaimu DPP Kweka.
Ambaye alihusishwa na Familia ya Mbowe kama mkwe wake.
Akihamishia makazi kwa muda pale Arusha kwa kuisimamia kesi ile.

Sasa tunalazimika kuamini kwamba haya mambo yamerudi na yanashamiri kwa kasi.

Time will Tell!

Mnyonge Mnyongeni Lakini Haki Yake Mpeni.

View attachment 2247466
7baya anastahili kufia gerezani

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom