Nani yupo nyuma ya utekaji na mauaji haya Tanzania? Kauli moja nini kifanyike?

Nani yupo nyuma ya utekaji na mauaji haya Tanzania? Kauli moja nini kifanyike?

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
8,406
Reaction score
9,619
Wakuu habari,

Sio wote JF wenda wanaguswa na yanayoendelea ndani ya nchi hii (zingatia wapo machawa wa ccm)

Taifa sasa linajaa laana za watu kutwekwa, kuuawa (machozi ya damu).

Nani yupo nyuma ya upumbavu huu? Nani anaratibu kwa faida ya nani?

Kama ni kwa faida ya Taifa nakataa, kama ni kwa faida la genge dogo ndani ya nchi nakubali.

Nini kifanyike sasa, maoni yako ni muhim sana, machawa wa CCM kaa mbali na andiko hili.

Natanguliza pole kwa ndugu na jamaa kwa kipindi ichi kigumu. Tutavuka kwa dam na jasho hakuna atakae ishi milele. Ila hili halivumiliki.

Pia soma:
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Tungoje taarifa rasmi kutoka vyombo vya Usalama
 
aisee tuache kusifia sifia uninga watanzania damu ya mtu haiendi bure utawarudia kuanzia aliepanga tukio mpka walofanya na tukiwajua chuma yao nchi imeanza kulia machozi ya damu
Nani yupo nyuma ya ujinga huu na kwa faida ya nani? Malengo yao ni yapi, nini kifanyike?
 
Nani yupo nyuma ya ujinga huu na kwa faida ya nani? Malengo yao ni yapi, nini kifanyike ,
chakufanya ni raia wenyewe kulindana na kujilinda tumeshndwa kupata bunduk bas tutbee na visu basii maana hakuna tamko kutoka kwenye mamlaka yyte tangu mambo haya yameanza kutokea
 
Polisi ndiyo wakujibu swali lako.

1. Bahati mbaya hilo halitatokea zaidi ya dharau, uwongo, kubadili mambo, kusingizia, na kutuhumu wakosoaji wa serikali.

2. Si kila anayepotea polisi au wanaojiita wanausalama wanahusika. Lazima tuwaze kwa werevu bila mihemuko. Tz ina watu zaidi ya milioni 60, inawezekana wengine wanapotea new mambo mengine tu.

3. Baadhi ya matukio kama kutekwa na KUUWAWA kwa Ali Kibao, Sativa na wengine ni dhahiri wanaojiita wanausalama wanahusika. Labda kama wewe unatembea umefumba macho huoni, na masiko umetia pamba husikii wala huelewi.
 
uchunguzi uanzie kwenye chanzo cha Taarifa za utekaji ni muhimu zaidi 🐒
Utekaji upi wazungumza maana yapo matukio mengi ya utekaji achana na wa aliekua msaidizi wa Mnyika.

alafu nimetaadhalisha machawa wakae mbali na andiko hili.

Wakati tunaendelea kutaka jua nini kifanyike napendekeza ,serikali ya tz kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa period (ICC) ushahidi upo
 
20240908_151114.jpg
 
Back
Top Bottom