Nani zaidi kati ya Toyota land cruiser vs Nissan patrol

Nissan zinapendwa uarabuni kwa sababu ya urahisi wa kufanya tunning mkuu. Japo ni magari yanayokaribiana kwa mambo mengi sana ila cruiser inafanya poa zaidi off road. Kuna video ya YouTube pale juu iangalie, ni comparison nzuri sana ya hayo magari mawili
 
Mfano patrol y60 na LC 80 series ipi matata zaidi?!
Merry Christmas Mkuu,
Nissan Patrol Y60 Kwanza sifa kuu iliyonayo ni stability iwapo kwenye barabara ya vumbi au lami kutokana na upana wake na ground clearance ya kawaida ukilinganisha na Land Cruiser series 80. Nissan bei ya vipuri ipo juu na zinataka matunzo zaidi.

Land Cruiser series 80, zinafahamika Kwa kuhimili njia mbovu na wepesi wake wa kufanyiwa service, vipuri kupatikana kirahisi kutokana na Toyota kuwa na sehemu nyingi za Ku assembly magari yake na dealership wa spare zake wapo maeneo mengi.Pia reliability ya hizi gari ni kubwa hata ikifanya kazi ngumu mfululizo.

Kiufupi kuna vitu Nissan Patrol anavyo na Land Cruiser Hana na kila mmoja kuwa na sifa yake ya kipekee.
Kila mmoja kwenye hizo gari alikuwa na injini Bora, Nissan ana Td42,Tb45,T48 na L/Cruiser ana 1HZ na 1Hdt.
 
Mkuu Nissan Patrol zinazofanya vizuri Uarabuni ni zile zote zenye injini za petrol ambazo ni TB45 na TB48 zipo kwenye Nissan Patrol Y60 na Y61. Zinafanyiwa tunning na zinafika hp kubwa sana, Kwa rekodi kuna injini ya TB48 walifikisha 2000hp.

Na kwenye Nissan Patrol Y62 ni mwendo wa V8 petrol injini hawana option ya diesel.
Kwenye mchanga waarabu hawataki gari yenye 4wd tu, wanapendelea gari yenye uwezo wa kukimbia na kutake off haraka.

Hiyo shughuli anayofanya Nissan Patrol akiwa na injini za Petrol, Land Cruiser iwe hardtop, pick up au series 200 ikiwa na injini ya 1VD-FTV inafanya vizuri. Kwa wao inabaki kuwa wachague Nissan au L/Cruiser.
 
Salamu sana ziwafikie wapendwa wana JF
Naomba kujuzwa japo kwa undani Kati ya haya magari mawili na sifa zake TOYOTA LAND CRUISER vs NISSAN PATROL
aksante.

Itakuwa inawahusu wale wenye Nissan nyeupe.
 
Howo, Yutong, Zhongton ni gari za muda mfupi. Hizo gari huwezi tumia miaka 10 ikakupa performance ileile.

Msweden unatumia mpaka mjukuu wako. Angalia gari za Kilimanjaro, zile Andare, zipo namba A ila mpya kabisa.

Tafuta michina ya miaka 5 nyuma.
 
Tukilinganisha Nissan Patrol Y60,Y61 zikiwa na injini ya Td42 na Land Cruiser series 70/80 zenye injini ya 1HZ.

Nissan Patrol zinatatizo la Clutch, na matoleo ya nyuma Gia kuingia zilikuwa tatizo.Bei ya spare hata kama ni toleo la zamani bei ipo juu.

Land Cruiser injini ya 1HZ ni jiwe haswa ndio iliyompa Toyota heshima popote duniani, hata ikifanya kazi kwenye high rpm haiwezi kusumbua, mfumo wake wa injection pump hata ukikutana na mafuta machafu haisumbui zaidi ya miss nazo zitakata.Kwenye Gia zile za mwanzo zilikuwa na ugumu Ila ziliboreshwa.Spea zake bei ni kulingana na eneo au genuine au used kila sehemu zipo. Ni gari ambayo sio Mayai fundi yoyote akifunga inatembea na haina teknolojia za kuleta utata.

Nissan Patrol kwenye Stability kamshinda Toyota Land Cruiser .Na Toyota kamshinda Nissan Patrol kwenye uimara wa injini.
 
Howo, Yutong, Zhongton ni gari za muda mfupi. Hizo gari huwezi tumia miaka 10 ikakupa performance ileile.

Msweden unatumia mpaka mjukuu wako. Angalia gari za Kilimanjaro, zile Andare, zipo namba A ila mpya kabisa.

Tafuta michina ya miaka 5 nyuma.
Nje ya Mada

Market Penetration vs durability/ reliable ni vitu tofaut kabisa
 
Duh! Mwenye basi hapo mbele yupo serious kweli kweli

Your browser is not able to display this video.
 
Warabu wanapenda sana Land Cruiser, wanazikubali kinoma yani. Ukiangalia desert clips utakuta ma 1HZ na ma 1VD-FTV ya kutosha ni mwendo wa 70 series na 200 Series tu.
 
Zote gari nzuri endapo ww sio mtu wa kuwaza pesa za kula na kuishi,

Ila tukianza sema gari hii mbovu au mbaya mbona wao wanatumia vizuri iweje sisi ambao hatujui hata kudesign clutch plate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…