TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Im sorry to say, mama yenu anawaharibu bila kujua.Kwakweli, nitalifanyia kazi
Katika maisha ni muhimu mtu kulelewa katika mazingira ya kujitegemea na kushiriki katika majukumu mbalimbali ya nyumbani. Inapotokea mtu mmoja (awe ni mama, baba, mfanyakazi nk) akawa yeye tu ndio anafanya kila kitu, hii inawafanya watu wengine hapo nyumbani kubweteka na kujikuta hawawezi kufanya chochote.
Mfano mimi mke wangu aliniambia yeye tangu azaliwe kazi zote za nyumbani anajua kufanya, isipokua KUPASI nguo ni baba yake amekua akimpasia! Matokeo yake nimemuoa hajui kabisa kupasi, na mwanzoni akawa anategemea eti MIMI ndio nichukue jukumu la kumsaidia kupasi nguo zake na zangu. Mwanzoni nilijitahidi ila nikaona huu ujinga, baada ya kumkomalia imemchukua muda mrefu sana kuja kujua kupasi.
Nina rafiki yangu mwingine wa kike, nae aliniambia nyumbani kwao baba yake ndio amekua akifanya kila kitu kuanzia kwenda sokoni, shopping anasema mpaka chupi, pads nk baba ndio anawanunulia! Kimbembe sasa dada alipokuja kuolewa akawa anategemea mumewe nae awe anafanya kama baba yake, yaani kila kitu afanye. Na asipofanya ni ugomvi humo ndani dada analalamika mume hayuko responsible.
Ushauri wangu nyie watoto hasa wa kike anzeni tabia ya kumlazimisha mama awaachie baadhi ya majukumu muwe mnafanya nyinyi. Mfano kama mpo wakike wawili au watatu mnachagua kila mtu kazi zake ambazo atakua anazifanya na muwe mnazifanya kweli. Kama ni kuosha vyombo, kufua, kufanya usafi nk muwe mnaamka mapema kufanya ili na mama nae apumzike.