Naogopa kuwa mama

Si mtamuua huyo mama? Aisee. Ana bahati mbaya mno mama Mtanganyika. Sasa MUNGU akiamua apumzike hizo kazi atafanya nani?
 
Hata mimi nimeshangaa bora nyumba ingekua na watoto wa kiume angalao inajulikana wanaume hawapatani na kazi za jikoni ila mpo wanawake tena watu wazima kazi kama kuosha vyombo nazo zinawashinda
 
Hata mimi nimeshangaa bora nyumba ingekua na watoto wa kiume angalao inajulikana wanaume hawapatani na kazi za jikoni ila mpo wanawake tena watu wazima kazi kama kuosha vyombo nazo zinawashinda
Malezi yako tofauti sana,yaani mama yangu atakuamsha na ngoma😂
 
Hivi kwanini wanawake wengi mnatamani sana mngekuwa wakiume? Hili nimeliobserve sana.

Jitahidi ufikie hata nusu ya alivyo mama yako, utakuwa mwanamke mzuri na mama bora kwa familia yako.

Baadhi ya kina mama ni mifano mizuri ya kuigwa, wanafanya mengi kwa maslahi ya familia na hutokaa uwasikie wakinung'unika lakini maisha yalivyo ni ya ajabu wengi wao huangukia kwenye ndoa na familia mzigo zinazowatesa.

Msaidie mama kazi hata kama hataki kusaidiwa, fanya hivyo hivyo sio kosa. Mimi nikiwa nyumbani huwa namsaidia mama mambo mengi sana na sipendi kuona anahangaika na nipo karibu na naweza kufanya kwa niaba yake. Mungu awajalie maisha marefu na afya njema wamama wote wanaozipambania familia zao kwa upendo, ni nguzo imara sana ambayo wengi huwa hawaoni umuhimu na thamani yake mpaka pale itakapodondoka.
 
Hapana mkuu, mimi sio mvivu
Sasa kama had umri huo unafuliwa nguo na kufanyiwa usafi, ni title gani upewe zaidi ya uvivu?
On a serious note na mama wa Kuwadekeza mmepata!! Mimi ni wa kiume lakini @14years nilikuwa napika chakula cha jioni cha Familia, kuosha vyombo, pamoja na kupiga pasi nguo za baba (rip).
 
Wewe ni mfifu sana, atakaye oa wewe shiiiii atateseka
 
Sijawahi kuogopa kuwa mama.Kila Jambo likifika wakati wake unajikuta Tu unaweza kuliishi.Binafsi nna watoto watatu wote bado wako primary.Katika hao watoto last born Tu ndo namwamsha.First born(girl) anaamka mwenyewe na kujiandaa, second ni mvulana std two anaamka mwenyewe anabandika maji ya kuoga,akiyatoa ananibandikia Mimi(hapa ndo nimekuja kugundua watoto wa kiume na mama zao wanavyowapenda)
Kuwa mama kwangu ni furaha Tu.Siku za j'pili mi napenda misa ya kwanza hivo huwa nawaacha wenyewe wanakuja misa ya pili.Na dada hawaamshi Ole wao nirudi kanisani nikute hawajaenda.

Nikutie moyo Tu.Wakati ukifika wala hutojuta.Katika kazi za nyumbani nnazopenda no.moja ni kupika.Hizo nyingine nazifanya Tu.
 
Asante kwa ushauri mzuri big ciccy 🌹🙏
 
Sio kama hatuwez kufanya mkuu, naweza na ninajua kila kitu ni vile hapendi kusaidiwa anapenda afanye mwenyewe kila kitu,. Ninachowaza ni kwamba na mimi itabidi niwe kama yeye
 
Sasa nimeelewa!
 
Dah,
Huyo mama ndo mfano wa mke mwema kwa mujibu wa 'Mithali 31', na ni mama bora kwenu.
Ila sasa inafaa apunguze kudekeza mabinti zake ili mpate kujua vizuri kazi za ndani - kupika, kufua, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…