Naogopa kuwa mama

Dah,
Huyo mama ndo mfano wa mke mwema kwa mujibu wa 'Mithali 31', na ni mama bora kwenu.
Ila sasa inafaa apunguze kudekeza mabinti zake ili mpate kujua vizuri kazi za ndani - kupika, kufua, nk
Hatudeki na sio kama hatujui, ni vile hapendi kusaidiwa nawaza ikibidi nifate nyayo zake itakuaje
 
Mimi naona kabisa sitaweza aisee, naogopa😩😩
Mama yenu ni mchapakazi, lakini anakosea sehemu moja, kuwafanyia kazi na nyie. Hawa fundishi kuwajibika. Mtazoea kufanyiwa kazi, mtapata tabu kwenye nyumba zenu. Mama bora ni yule anayewafundisha watoto wake kufwajibika sio kuwafanyia. Mtoto lazima ujue kufua nguo zako, kufanya usafi na kupika
 
Tupate wapi tena mtu kama huyu, ambaye Mungu anakaa ndani yake ?
 
Hao anaoamka usiku mara 4 kuwaangalia wana umri gani?
 
Japo dhamira ilikuwa ni kuonyesha uoga wako na pengine kumpa sifa Bi. Mkubwa wako lakini kiuhalisia ulichoambulia hapa ni kuonyesha jinsi gani mama yako ana watoto wa ovyo kabisa ikiwemo wewe mwenyewe.

Usisubiri mpaka akuombeni msaada ndio mumsaidie. Eti mnaamka na kukuta kila kitu kilishafanywa tayari, hapa ni dhahiri mnaamka mida mibovu kwa kujua mama yupo.

Jaribuni kuamka kabla yake na mumsaidie kazi zake halafu muone kama akiamka na yeye atakasirika kusaidiwa.

Vitu vingine mjiongeze na nyie. Ni fedheha kwa mtoto wa kike kufuliwa na mama yake ama na mtu yeyote yule.

Nyie ndio mtakuja kuwapa ma housegal boxer za waume zenu wazifue.
 
Huyo mama yako atachoka sana akifikia uzeeni
Hao ndio wale wamama ambao kamwe hutasikia ana maumivu ya mgongo au miguu sijui inamuuma atazeeka na nguvU zake. Watoto wake watajua umuhimu wake siku wakibaki wenyewe. Na kila mmoja wao atasema hakika YULE ALIKUWA MTU NA NUSU
 
Madhali unauchezea ule ukuni na ukiwa na kizazi utakuwa tu mama.
Ila naamini hautakuwa bora walau nusu ya mama yako.

Umepata mama bora sana, muombee sana, ni moja kati ya wamama ambao mtoto unakuwa proud kote kote, ukiacha ile sifa ya uzazi ni ana sifa kede.
Wakati nakuwa mama yangu akiwa ana nguvu zake alikuwa kama mama yako, huwa nikimtiza na kukumbuka naishia kutabasamu na kumuombea dua.

Wamama bora kwa watoto wao mungu awaingize tu peponi moja kwa moja kwa kweli,


ISHIKE HII,
"UNAWEZA KUWA MAMA ILA NAAMINI HAUTOKUWA BORA KAMA MAMA YAKO"
 
Umesema vyema. Hata mimi wakati nakua nyumbani kulikua na wasaidizi wa kazi, kazi zote nafanyiwa mimi ni kuoga na kufua pichu tu. Majirani walikua wanasema nalelewa vibaya sana nitasumbua baadae. Nikaja kupata mtoto wa kwanza nikajikuta shughuli zote nafanya. Mpaka leo sijazoea kukaa na msichana wa kazi kwanza sipendi, kazi zangu nafanya mwenyewe. Kazi za nje tu ndio nina mtu
 
Watoto wa shangazi yangu waliishi maisha kama hayo uliyoelezea hapa. Siku haina jina wala taarifa mama yao (shangazi) aliugua ghafla akakimbizwa hospital kufika madaktari wakasema hamjaleta mgonjwa bali mmeleta mwili wa marehemu.

Hakuna rangi waliacha kuona wale binamu zangu kwa namna marehemu mama yao alivyokuwa kawadekeza aseeeeee, wanaishi maisha magumu mno!! Hao wakike wamezalishwa bila utaratibu, ni wavivu hakuna mtu anawakubali kuishi nao. Mmoja kaolewa ndoa tatu na zote zimemshinda sababu ya uvivu anaishia kuachika.

Maisha ni maamuzi yako ingawa malezi na makuzi ni muhimu sana hasa unapoanza maisha ya kujitegemea.
 
Hongera Kwa mama yako maana Mimi siwezi kuwa kama yeye hata robo,yaani mwanangu mkubwa wa kujitegemea alale aamke nimeshampikia chai,nguo zake nimemfulia,anachelewa kurudi pengine Hana sababu ya msingi Mimi nimsubirie nihakikisha amekula,bado usiku nikachungulie kama kashusha neti!! Yaani anawajibika Kwa mtoto wa 18+kama anahudumia wasiojiweza? Hivi haya ya kweli au unatania?
 
Huwezi kuwa kama mama yako ila anayoyafanya yawe funzo kwako.

Huenda mama yako hataki wasaidizi wa kazi kwa maana ya kutaka kuwafundisha mwenyewe nafasi ya mwanamke kwenye familia kwa vitendo.

Nimependa ulivyosema huwezi kuishi mwenyewe(unaogopa), changa karata zako vizuri hata ikitokea ukapata mwenza basi awe mwenye kuendana na wewe maana inaoekana unadeka sana pia.

Muhimu: Tengeneza mazingira ya kumsaidia majukumu wewe pamoja na hao ndugu zako ili nae apate kupumzika.
 
Hujawahi kufua wala kupika wala kufagia uwanja wala kuosha vyombo wala kudeki.

Mmemgeuza mama yenu punda? Kumsaidia kazi mnasubiri hadi awaambie?

Mitoto ya hovyo na mivivu! 😎

-Kaveli-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…