Naomba iwepo JF party kabla ya Septemba 30, 2024

Uongozi wa JF,

Tunaomba kabla ya Sept 30, 2024 tuwe na JF party sehemu tu ya kawaida tupeane mawaidha.

Kwa wale madada tutafurahi kuwaona badala ya kutiana moyo inbox.

Ahsante, nawasilisha.

JF Party zote za zamani (zilifanyika kama mara 2 plus matukio mengine kama ziara za kitalii na kuwaona wasiojiweza) zilikuwa zinaandaliwa na kuratibiwa na members kama wewe wenye nia zinazofanana...

JF ya sasa majority wana utoto mwingi bado kamasi zinawatiririka...

JF ya sasa mtu akiona picha tu selfika ya mtu mwingine, mbio kwenye maPM kusimangana na kuzushiana maneno, sembuse akiwaona watu live...shubamitiiii
 
Sijapenda leo ulivyoamka na hasira😂
 
Sawa sawa Mkuu hii ya siku hz ni utoto tu..ndio maana watu wanakutana ki legendary kimya kimya
 
Acheni uboya! Mbona enzi za Twitter, majamaa walizindua kitu kinaitwa T.O.T bonanza, yaani "Tanzanians On Twitter Bonanza rasmi mnamo mwaka 2020... na mwitikio ulikuwa mkubwa tena very positively?! na ikawa inafanyika kila mwaka... Sijui saiv maana sijafatilia kitambo baada ya kuzidi kubanwa na mambo.

Hakukuwa na aliyetekwa, kupelekwa polisi wala kupotea na kufa na wala kuzodolewa ingawa wasema hovyo/wananga serikali wapo tele! Machawa na wanaotetea upumbavu na ushetani, wauza miili, Wakujipendekeza, Wanafki rangi mbili... Na wengineo wote walikuwemo na ililika starehe sio poa! Tena ulinzi wa kutosha!

Sasa nyinyi mnaogopa nini?!

ZINGATIENI:- "Serikali ikiamua kuwapateni nyie maboya itawapata tu!"

Hebu tuandae "Tanzanians on JF Bonanza" Ebo!!!!!
 
Back
Top Bottom