Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

Wilbert255

Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
27
Reaction score
28
Habari za muda Wakuu,

Kuna nyumba nimetokea kuzipenda, nimeona Kama gharama ni ndogo. Ni nyumba ambazo zimejengwa bati kwa juu hazionekani.

Kuna maswali najiuliza naomba majibu:

Je, kweli hizo nyumba zinatumia bati chache?

Je, naweza kutumia tofali za kuchoma?

Je, nikitaka kujenga nyumba ya vyumba vitatu (kwa staili ya hiyo nyumba) inaweza cost kiasi gani cha pesa?

Nawasilisha!

Screenshot_20201102-220537~2.png
 
1. Ndio zinatumia bati chache
2. Ndio waweza tumia tofali za kuchoma
3. Gharama kwa boma 15m (normal standards )
Gharama kwa bati 5m
Gharama za finishing kuanzia 20m na kuendelea kulingana na uchaguzi wako wa materials
 
Hii nadhalia ya kwamba hizi nyumba ni nafuu sio kweli, ukweli ni kwamba gharama za kupauwa zinapunguwa kwa kiwango kikubwa maana zinatumia mbao chache na bati chache lakini sehemu nyingine kama kusimamisha boma na kufanya finishing gharama zipo vilevile nimeongea na mafundi wengi wanatoa ushauri huo kinachobadilika ni mtindo tu wa ujezi.
 
Pamoja na kuwa utaezeka kwa gharama nafuu ila ujue utalipia huo unafuu kwenye kuidhibiti isivuje wakati wa mvua kwani zinaongoza kwa kuvuja ikiwa itaezekwa bila kufuata utaalamu elekezi,pia kwenye kupaka rangi ndani na nje utabidi upake rangi za gharama zenye kuzuia maji tofauti na kujenga nyumba zenye pia lenye kuonekana maana unaweza ikaskim na gypsum powder na siku zikaenda wakati unatafuta pesa za kununulia rangi ila kwa hizo nyumba haiwezekani, na mwisho utalipia huo unafuu kwenye madirisha,kwani haziihitaji madirisha ya nyavu zinataka uweke ya vioo(aluminium au pvc)kwani mvua ikinyesha inanyeshea direct chumbani bila kikwazo.
 
Picha pls wengine hatukuelewi
Habari za muda Wakuu

Kuna nyumba nimetokea kuzipenda, nimeona Kama gharama ni ndogo
Ni nyumba ambazo zimejengwa bati kwa juu hazionekani

Kuna maswali najiuliza naomba majibu.

Je, kweli hizo nyumba zinatumia bati chache?

Je, naweza kutumia tofali za kuchoma?

Je, nikitaka kujenga nyumba ya vyumba vitatu (kwa staili ya hiyo nyumba) inaweza cost kiasi gani cha pesa?

Nawasalisha!

View attachment 1618253
Tunazo design tofauti tofauti mkuu ..kama unapendelea nyumba izo
 
Kuna jamaa instagram wanahusika na hizo nyumba ila nimesahau majina yao
kwa nillivosikia zile nyumba hazina bati kabisa juu,ile ni concrete tu na nondo.wanadai zina gharama nafuu
zaidi ya hapo wasubiri wakuu
Siyo lazima iwe ya zege mkuu ..kinachofanyika inatumia mbao chache but iyo roof inasetiwa katika pitch ndogo ndio husaidia hata kupunguza idadi ya mbao zitazotumika ..pia nyumba izi huleta muonekano mzuli wenye kuvutia
 
siyo lazima iwe ya zege mkuu ..kinachofanyika inatumia mbao chache but iyo roof inasetiwa katika pitch ndogo ndio husaidia hata kupunguza idadi ya mbao zitazotumika ..pia nyumba izi huleta muonekano mzuli wenye kuvutia

oh
ni kweli zina muonekano mzuri sana,siku hizi nyumba za bati zimepitwa na wakati
 
Hii nadhalia ya kwamba hizi nyumba ni nafuu sio kweli, ukweli ni kwamba gharama za kupauwa zinapunguwa kwa kiwango kikubwa maana zinatumia mbao chache na bati chache lakini sehemu nyingine kama kusimamisha boma na kufanya finishing gharama zipo vilevile nimeongea na mafundi wengi wanatoa ushauri huo kinachobadilika ni mtindo tu wa ujezi.
Gharama Zinapungua au hazipungui?
 
Gharama Zinapungua au hazipungui?
Kwa uhakika kabisa (bila shaka) gharama zinapungua kwenye kupaua kwa 50% au zaid.

Ila gharama kiujumla inategemea na namna jengo lilivyo sanifiwa, na hasa kwenye namna mitaro ya maji (gutters) ilivyowekwa. Maana kwenye nyumba za paa lisiloonekana ujenzi wa gutter huhitaji ratio kali ya mortar iliyochanganywa na waterproof materials, na kuna nondo pia, wakati kwenye paa la kuonekana hivo vitu hakuna kabisa. Hivyo kadri unavyoweka mitaro mingi ndivyo unavyoongeza gharama.

Tembelea ukurasa wa insta kama @ newblockcity_tz na wengine wengi utapata somo zaid huko

FFA5919B-B431-4A38-A3CA-515E667CE606.jpeg
 
Hii nadhalia ya kwamba hizi nyumba ni nafuu sio kweli, ukweli ni kwamba gharama za kupauwa zinapunguwa kwa kiwango kikubwa maana zinatumia mbao chache na bati chache lakini sehemu nyingine kama kusimamisha boma na kufanya finishing gharama zipo vilevile nimeongea na mafundi wengi wanatoa ushauri huo kinachobadilika ni mtindo tu wa ujezi......
Hakika, utakachopunguza kidogo ni gharama za mabati na mbao pekee. Vitu vingine vinabaki vilevile
 
Back
Top Bottom