run CMD
JF-Expert Member
- May 31, 2015
- 3,185
- 3,909
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeongea ukweli hizi nyumba shida yake kubwa kipindi cha mvua zinavuja kwa kuwa paa lake limelala sana na hupelekea maji kutuama kwenye ile gypsum board na kuleta shoti ya umeme kila mvua inaponyesha, gharama haina tofauti finishing ya nyumba iko palepalePamoja na kuwa utaezeka kwa gharama nafuu ila ujue utalipia huo unafuu kwenye kuidhibiti isivuje wakati wa mvua kwani zinaongoza kwa kuvuja ikiwa itaezekwa bila kufuata utaalamu elekezi,pia kwenye kupaka rangi ndani na nje utabidi upake rangi za gharama zenye kuzuia maji tofauti na kujenga nyumba zenye pia lenye kuonekana maana unaweza ikaskim na gypsum powder na siku zikaenda wakati unatafuta pesa za kununulia rangi ila kwa hizo nyumba haiwezekani, na mwisho utalipia huo unafuu kwenye madirisha,kwani haziihitaji madirisha ya nyavu zinataka uweke ya vioo(aluminium au pvc)kwani mvua ikinyesha inanyeshea direct chumbani bila kikwazo
Nikiona kuna jamaa alianza kikawaida hadi lenta kisha baadae akavutiwa na contemporary akaimodify vizuri tuInawezekan raman ya nyumba Ya kawaida ukabadlish mtindo wa upauaji (na ukapaua kwa mtindo Uo)
kuna jamaa niliwaona facebook hio tatizo wanali solve kwa kutengenezea kitu kufunikia nigumu kama lamiii sijui linaitwaje nila lazwa kwenye ukuta na bati so maji haya piti kabisaUmeongea ukweli hizi nyumba shida yake kubwa kipindi cha mvua zinavuja kwa kuwa paa lake limelala sana na hupelekea maji kutuama kwenye ile gypsum board na kuleta shoti ya umeme kila mvua inaponyesha, gharama haina tofauti finishing ya nyumba iko palepale
inawezekana mkuu ila itakubidi upate fundi makini na mzoefu na mwenye talent kidogo ya ubunifu(design) ..coz unaweza kuta nyumba unayotaka kuibadili channel za maji kufikia gutter ikawa mtihani kutokana na ilivyodizainiwa awali but all in all its possibleInawezekan raman ya nyumba Ya kawaida ukabadlish mtindo wa upauaji (na ukapaua kwa mtindo Uo)
Hivi kwenye mvua inakuwaje hizo nyumba? Mana ziko flati na mvua inapiga moja kwa moja kutani,madirishani