Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

1. Ndio zinatumia bati chache
2. Ndio waweza tumia tofali za kuchoma
3. Gharama kwa boma 15m (normal standards )
Gharama kwa bati 5m
Gharama za finishing kuanzia 20m na kuendelea kulingana na uchaguzi wako wa materials
5m bati boss kama utanunua za gage 28 let say kwa 33000 10ft hizo ni bati 150 kwa uezekaji huo nahisi hilo litakua kanisa sio nyumba ya kuishi. NB nimetumia bati 120 kuezeka muezeko wa kawaida nyumba yenye vyumba 4 vya kulala na makolokolo mengine. HIZO SIO BATI CHACHE
 
Habari za muda Wakuu

Kuna nyumba nimetokea kuzipenda, nimeona Kama gharama ni ndogo
Ni nyumba ambazo zimejengwa bati kwa juu hazionekani

Kuna maswali najiuliza naomba majibu.

Je, kweli hizo nyumba zinatumia bati chache?

Je, naweza kutumia tofali za kuchoma?

Je, nikitaka kujenga nyumba ya vyumba vitatu (kwa staili ya hiyo nyumba) inaweza cost kiasi gani cha pesa?

Nawasalisha!

View attachment 1618253
 

Attachments

  • IMG-20200810-WA0001.jpg
    IMG-20200810-WA0001.jpg
    84.9 KB · Views: 9
Pamoja na kuwa utaezeka kwa gharama nafuu ila ujue utalipia huo unafuu kwenye kuidhibiti isivuje wakati wa mvua kwani zinaongoza kwa kuvuja ikiwa itaezekwa bila kufuata utaalamu elekezi,pia kwenye kupaka rangi ndani na nje utabidi upake rangi za gharama zenye kuzuia maji tofauti na kujenga nyumba zenye pia lenye kuonekana maana unaweza ikaskim na gypsum powder na siku zikaenda wakati unatafuta pesa za kununulia rangi ila kwa hizo nyumba haiwezekani,na mwisho utalipia huo unafuu kwenye madirisha,kwani haziihitaji madirisha ya nyavu zinataka uweke ya vioo(aluminium au pvc)kwani mvua ikinyesha inanyeshea direct chumbani bila kikwazo
Ha ha ha [emoji23]
 
5m bati boss kama utanunua za gage 28 let say kwa 33000 10ft hizo ni bati 150 kwa uezekaji huo nahisi hilo litakua kanisa sio nyumba ya kuishi. NB nimetumia bati 120 kuezeka muezeko wa kawaida nyumba yenye vyumba 4 vya kulala na makolokolo mengine. HIZO SIO BATI CHACHE

Hiyo ni gharama ya kazi yote ya bati , hapo weka mbao na bati, nadhani hukuelewa vizuri mkuu
 
Pamoja na kuwa utaezeka kwa gharama nafuu ila ujue utalipia huo unafuu kwenye kuidhibiti isivuje wakati wa mvua kwani zinaongoza kwa kuvuja ikiwa itaezekwa bila kufuata utaalamu elekezi,pia kwenye kupaka rangi ndani na nje utabidi upake rangi za gharama zenye kuzuia maji tofauti na kujenga nyumba zenye pia lenye kuonekana maana unaweza ikaskim na gypsum powder na siku zikaenda wakati unatafuta pesa za kununulia rangi ila kwa hizo nyumba haiwezekani, na mwisho utalipia huo unafuu kwenye madirisha,kwani haziihitaji madirisha ya nyavu zinataka uweke ya vioo(aluminium au pvc)kwani mvua ikinyesha inanyeshea direct chumbani bila kikwazo
Hi ni ndharia.....hata za paa mvua inaweza nyesha direct inategemea na jinsi mvua inavyonyesha na upepo
 
Tatizo la nyumba za contemporary ni zinategemea ujenzi bora wa fundi na finishing ya maana ndio zikufurahishe nafsi tofauti na hapo zinakuwa mbaya
Hizi za pitched roof zenyewe uzuri unaletwa na mitindo ya bati tuu mambo mengine hayana impacts sana
 
oh
ni kweli zina muonekano mzuri sana,siku hizi nyumba za bati zimepitwa na wakati
Hizo nyumba sio nafuu bali zinahitaji pesa nyingi ili zifanyiwe urembo na kipengele hicho ndio kinafidia pesa ya kwenye bati kwa hiyo inabskia kuwa ni option ya mtu kuchagua.

Binafsi kuliko nijenge hiyo bora ghorofa.
 
Zinaitwa kontemporary kaka angu ananishauri Sanaa nijenge stailo ya nyumba hzo ila was was wanting isje nyumba kuvuja wakat wa mvuaa maanke naona kbsa hkna kizuizi mvua inapiga directly Kama ilivyo na nyumba yote italowaa majiKama mti ukionyeshewa
 
Sinaitwa kontemporary kaka angu ananishauri Sanaa nijenge stailo ya nyumba hzo ila was was wanting isje nyumba kuvuja wakat wa mvuaa maanke naona kbsa hkna kizuizi mvua inapiga directly Kama ilivyo na nyumba yote italowaa majiKama mti ukionyeshewa
Wala haiwezi kuvuna ila fanya vitu viwili;
1) Tafuta fundi bingwa wa kufanya "roofing", hapa ni pamoja na kujenga " gutter" zenye ubora wa hali ya juu sana.
2) Tafuta fundo mzuri wa rangi, na ingia gharama sana kwenye rangi ili kuepusha rangi kulowa na kubanduka
Hizi nyumba kama huna pesa ya kutosha achana nazo, ni gharama sana na sana sana kwenye roofing
 
Mimi Nimejenga Contemporary na ndio naishi humo hadi sasa...Nawapa facts....!

1. Nyumba ina Room 3 mbili kawaida moja master,plus sitting,dinning na public toilet,two verandah...bati zilicost 1.6m na mbao zilicost 1.1m

2.nilifanya waterproofing mwenyewe maana ni kitu nakifahamu ilinigharimu laki 540 mpaka ufundi

3.nyumba yangu ina muonekano wa kipekee mtaa mzima

4.wiki hii nafanya heat insulation itanigharimu laki 4 nyuma itakua na joto la chini kabisa

cha kuzingatia

1.Waterproofing
2.heat nsulation au uweke vent za kupitisha hewa kwenye paa
3. jitahidi kwenye madirisha ziba juu kwa polysulphide sealant inauzwa elf 25 moja inatosha ili kuzuia maji yasiingie ndani ya mvua,usizibe kwa silicone

4.inaweza kujengwa na tofali yoyote

nakaribisha maswalu
 
Hii nadhalia ya kwamba hizi nyumba ni nafuu sio kweli, ukweli ni kwamba gharama za kupauwa zinapunguwa kwa kiwango kikubwa maana zinatumia mbao chache na bati chache lakini sehemu nyingine kama kusimamisha boma na kufanya finishing gharama zipo vilevile nimeongea na mafundi wengi wanatoa ushauri huo kinachobadilika ni mtindo tu wa ujezi......
Zile nyumba zina gharama kwenye finishing kwa sababu usipowekea bajeti nzuri kwenye finishing zinakuwa kama msikiti wenye uongozi wa mashehe wanaokula hela za michango ya ujenzi.
PIA sio kila fundi anaziwezea.
 
Kuna jamaa instagram wanahusika na hizo nyumba ila nimesahau majina yao
kwa nillivosikia zile nyumba hazina bati kabisa juu,ile ni concrete tu na nondo.wanadai zina gharama nafuu
zaidi ya hapo wasubiri wakuu
Kweli kenchi na bati ni utata usawa huu, ukizingatia mapaa marefu nikama yapo kwenye chati.
 
Hakika, utakachopunguza kidogo ni gharama za mabati na mbao pekee. Vitu vingine vinabaki vilevile
Unajua kusimamisha boma gharama yake inaweza kuwa mara moja na nusu ya gharama ya paa ya kupaua kwa bati na kenchi ndefu za siku hizi, hasa kwa mikoani!?
 
Back
Top Bottom