Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

Inapendeza ukifunika na zege ila kupaua kwa bati hazivutii ila kila mtu na mapenzi yake
Nalog off
Hazivutii kivipi wakati bati hazionekani? Kuezeka kwa zege ni gharama kubwa ukilinganisha na kutumia bati. Huyu amependa structure ya nyumba hizi lkn kwa bei nafuu.
 
Hii ya kwangu imenilia hela nyingi sana sana katika roofing!
25678901.jpg
 
Zege ni nzuri bt hawa mafundi wetu ni pasua kichwa maana akikosea tu ameshakuumiza na wakati mvua unyevu utatokea mpaka ndani mwisho wa siku hata amani ya kulala hiko chumba itapotea maana ni mwendo wa kuhis zege litaanguka usiku.
 
hyo migongo migongo juu kabsa kwenye paa ni bati au zege alafu maji ya mvua huwa yanashukia wapi au yanaingia moja kwa moja ndani mpaka kwenye mandoo?
Hizo nyumba huezekwa kwa bati na hapo unaloliona ni bati, maji yanatoka kupitia gutter. Kwenye gutter ndio kwenye utata, unatakiwa utumie gharama kubwa na fundi mzuri sana, la sivyo utakiona.
 
Hizo gata mbona hazionekan kwenye huo mchoro au zinafichwa ?
Hizo nyumba huezekwa kwa bati na hapo unaloliona ni bati, maji yanatoka kupitia gutter. Kwenye gutter ndio kwenye utata, unatakiwa utumie gharama kubwa na fundi mzuri sana, la sivyo utakiona.
 
Hizi nyumba inatakiwa kujengwa sehemu zenye hali ya jangwa kama huko Uarabuni ambako nadhani ndo asili yake, kule hawana mvua pia haziathiriwi na upepo mkali ulioko kule. Wabongo kwa kuiga nao wameanza kuzijenga bila kujua chimbuko lake, naweza sema ni ulimbukeni!!
 
Mimi Nimejenga Contemporary na ndio naishi humo hadi sasa...Nawapa facts....!

1. Nyumba ina Room 3 mbili kawaida moja master,plus sitting,dinning na public toilet,two verandah...bati zilicost 1.6m na mbao zilicost 1.1m

2.nilifanya waterproofing mwenyewe maana ni kitu nakifahamu ilinigharimu laki 540 mpaka ufundi

3.nyumba yangu ina muonekano wa kipekee mtaa mzima

4.wiki hii nafanya heat insulation itanigharimu laki 4 nyuma itakua na joto la chini kabisa


cha kuzingatia

1.Waterproofing
2.heat nsulation au uweke vent za kupitisha hewa kwenye paa
3. jitahidi kwenye madirisha ziba juu kwa polysulphide sealant inauzwa elf 25 moja inatosha ili kuzuia maji yasiingie ndani ya mvua,usizibe kwa silicone

4.inaweza kujengwa na tofali yoyote


nakaribisha maswalu
maishapopote hiyo heat insulation unamaanisha hizo vent ukishaweka alumninum vioo ni sawa pia au? Funguka kidogo mwana
 
Wala haiwezi kuvuna ila fanya vitu viwili;
1) Tafuta fundi bingwa wa kufanya "roofing", hapa ni pamoja na kujenga " gutter" zenye ubora wa hali ya juu sana.
2) Tafuta fundo mzuri wa rangi, na ingia gharama sana kwenye rangi ili kuepusha rangi kulowa na kubanduka
Hizi nyumba kama huna pesa ya kutosha achana nazo, ni gharama sana na sana sana kwenye roofing

Umeeleza yote...kama unataka kujenga nyumba yenye paa namna hii basi anza kuzoea kwa kucheza BIKO au anza kujifunza kufanya betting ya mipira ili upate mazoea ya kupata maumivu ya pesa yako
 
Kuna jamaa instagram wanahusika na hizo nyumba ila nimesahau majina yao
kwa nillivosikia zile nyumba hazina bati kabisa juu,ile ni concrete tu na nondo.wanadai zina gharama nafuu
zaidi ya hapo wasubiri wakuu
Bati zipo ila huwez kuziona jinsi walivyoziweka
 
Back
Top Bottom