Naomba kueleweshwa haya kuhusu nyumba hizi ambazo bati zake hazionekani

1. Ndio zinatumia bati chache
2. Ndio waweza tumia tofali za kuchoma
3. Gharama kwa boma 15m (normal standards )
Gharama kwa bati 5m
Gharama za finishing kuanzia 20m na kuendelea kulingana na uchaguzi wako wa materials
5m bati boss kama utanunua za gage 28 let say kwa 33000 10ft hizo ni bati 150 kwa uezekaji huo nahisi hilo litakua kanisa sio nyumba ya kuishi. NB nimetumia bati 120 kuezeka muezeko wa kawaida nyumba yenye vyumba 4 vya kulala na makolokolo mengine. HIZO SIO BATI CHACHE
 
 

Attachments

  • IMG-20200810-WA0001.jpg
    84.9 KB · Views: 9
Ha ha ha [emoji23]
 

Hiyo ni gharama ya kazi yote ya bati , hapo weka mbao na bati, nadhani hukuelewa vizuri mkuu
 
Hi ni ndharia.....hata za paa mvua inaweza nyesha direct inategemea na jinsi mvua inavyonyesha na upepo
 
Tatizo la nyumba za contemporary ni zinategemea ujenzi bora wa fundi na finishing ya maana ndio zikufurahishe nafsi tofauti na hapo zinakuwa mbaya
Hizi za pitched roof zenyewe uzuri unaletwa na mitindo ya bati tuu mambo mengine hayana impacts sana
 
oh
ni kweli zina muonekano mzuri sana,siku hizi nyumba za bati zimepitwa na wakati
Hizo nyumba sio nafuu bali zinahitaji pesa nyingi ili zifanyiwe urembo na kipengele hicho ndio kinafidia pesa ya kwenye bati kwa hiyo inabskia kuwa ni option ya mtu kuchagua.

Binafsi kuliko nijenge hiyo bora ghorofa.
 
Zinaitwa kontemporary kaka angu ananishauri Sanaa nijenge stailo ya nyumba hzo ila was was wanting isje nyumba kuvuja wakat wa mvuaa maanke naona kbsa hkna kizuizi mvua inapiga directly Kama ilivyo na nyumba yote italowaa majiKama mti ukionyeshewa
 
Sinaitwa kontemporary kaka angu ananishauri Sanaa nijenge stailo ya nyumba hzo ila was was wanting isje nyumba kuvuja wakat wa mvuaa maanke naona kbsa hkna kizuizi mvua inapiga directly Kama ilivyo na nyumba yote italowaa majiKama mti ukionyeshewa
Wala haiwezi kuvuna ila fanya vitu viwili;
1) Tafuta fundi bingwa wa kufanya "roofing", hapa ni pamoja na kujenga " gutter" zenye ubora wa hali ya juu sana.
2) Tafuta fundo mzuri wa rangi, na ingia gharama sana kwenye rangi ili kuepusha rangi kulowa na kubanduka
Hizi nyumba kama huna pesa ya kutosha achana nazo, ni gharama sana na sana sana kwenye roofing
 
Mimi Nimejenga Contemporary na ndio naishi humo hadi sasa...Nawapa facts....!

1. Nyumba ina Room 3 mbili kawaida moja master,plus sitting,dinning na public toilet,two verandah...bati zilicost 1.6m na mbao zilicost 1.1m

2.nilifanya waterproofing mwenyewe maana ni kitu nakifahamu ilinigharimu laki 540 mpaka ufundi

3.nyumba yangu ina muonekano wa kipekee mtaa mzima

4.wiki hii nafanya heat insulation itanigharimu laki 4 nyuma itakua na joto la chini kabisa

cha kuzingatia

1.Waterproofing
2.heat nsulation au uweke vent za kupitisha hewa kwenye paa
3. jitahidi kwenye madirisha ziba juu kwa polysulphide sealant inauzwa elf 25 moja inatosha ili kuzuia maji yasiingie ndani ya mvua,usizibe kwa silicone

4.inaweza kujengwa na tofali yoyote

nakaribisha maswalu
 
Zile nyumba zina gharama kwenye finishing kwa sababu usipowekea bajeti nzuri kwenye finishing zinakuwa kama msikiti wenye uongozi wa mashehe wanaokula hela za michango ya ujenzi.
PIA sio kila fundi anaziwezea.
 
Kuna jamaa instagram wanahusika na hizo nyumba ila nimesahau majina yao
kwa nillivosikia zile nyumba hazina bati kabisa juu,ile ni concrete tu na nondo.wanadai zina gharama nafuu
zaidi ya hapo wasubiri wakuu
Kweli kenchi na bati ni utata usawa huu, ukizingatia mapaa marefu nikama yapo kwenye chati.
 
Hakika, utakachopunguza kidogo ni gharama za mabati na mbao pekee. Vitu vingine vinabaki vilevile
Unajua kusimamisha boma gharama yake inaweza kuwa mara moja na nusu ya gharama ya paa ya kupaua kwa bati na kenchi ndefu za siku hizi, hasa kwa mikoani!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…