Naomba kueleweshwa suala la ndege ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Tanzania Bara kupokelewa Zanzibar

Masuala ya Muungano ni magumu na ukipata viongozi wasioweza kutathimini maadhara kuhusu maamuzi yao ni taabu Sana... thanks
 
Mimi ni mgeni humu hivi sukuma gang ni Wasukuma,kanda ya ziwa,au CCM.

Nakusikilizia counter hapa unijibu.
Wengine ni sukuma gangs na wao ni mdebwedo wanengua viu......n 😁😁😁😁
 
Wakati wasukuma wanateuliwa kila post na ikulu kuhamia chatle mlikua kimya.
Sasa macho yako pwani na visiwani watu roho juu.
Acha na siye tumulikwe.
 
kweli kabisa mkuu kwa hali tuliyofikia ni ngumu sana kujitenga nao hao watu ni vyema tukaboresha zaidi mazingira yetu tuwe kitu kimoja na wote tukawa na haki sawa hizi mambo sijui wazanzibar ukienda kule huna haki ya kupata kazi kwenye serikali yao kama huna kitambulisho cha uzanzibar mkaazi ila wao wakija huku wala hakuna anayejishughulisha tunawaona kama ndugu zetu na watanzania yoyote yule ila wao nitofauti kabisa hawatuchukulii kama ndugu zao kabisa..
 

Swali zuri.. Sikiliza kwa umakini na ili uelewe weka siasa pembeni.

TGFA ilishahama Wizara ya Uchukuzi tokea mwaka 2018, ilipitishwa na Bunge 2018, na GN ya serikali ilitoka 2018, iko chini ya State House, na TGFA ndio owner wa hizo ndege zote za ATCL kwa niaba ya Serikali.

Sasa, TGFA ndio inawabeba viongozi wote wa juu Serikalini, kuanzia Bara hadi Visiwani.. Kwa maana hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz, Rais wa Znz, Makamu wa Muungano na Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa JM wa Tz, wote hawa wanapewa usafiri wa Anga na TGFA..

So ndege za TGFA, kupokelewa Znz, na baadae kukabidhiwa kwa mkataba ATCL ni sawa. Umeelewa?
 
Hapo linatafutwa chaka la kutoa hotuba za kiccm Kwa wazanzibar sa lazma liandaliwe tukio hapo Leo makamu wa Kwanza WA rais atanangwa kwenye matv na redio mpaka akome vitukio kama hivi ni ajenda za maccm kufanya kampeni kama hujui SASA si unakumbuka mwendazake alichokula anakifanya kwenye matukio kama haya ndicho kinatafutwa SASA we tega sikio Tu.
 
Huyu Hangaya ana choko choko sana za chini kwa chini na makundi haya; 1. Bara 2. Wanaume 3. Kanda ya ziwa 4. Wanyonge ..acha tuendelee kumstahi kidogo
 
Sioni tatizo hata chembe, tena hii ni hatua nzuri kabisa. Kwa nini? sababu ni kwamba Zanzibar wanaserikali yao lakini wapo pia kwenye serikali ya muungano. Tanganyika ndio hawapo kwenye ramani. Ila sio shida as such. Ni wakati sasa wa kuleta umoja na ukaribu kwani hii ni nchi moja. Ndege zikipokelewa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Kumbuka Rais wa Zanzibar ni Waziri katika Serikali ya muungano. Taarifa ilisema Rais Samia amemtuma Rais wa Zanzibar kupokea Ndege hizo kwa niaba yake period. Shida ipo wapi?
 
Wakiambiwa iwe Serikali moja wanang'aka ila mambo wanayotenda ni ya Serikali moja. Sasa unakaa unajiuliza hawa watu wana Akili kweli. Wanatenda wasichokihubiri. Hivi Ndege hizo zinaenda Kupokelewa huko ili iweje? Zinaenda kupakwa Marashi ya Karafuu? Au ni sehemu ya Kampeini kuonekana chini ya utawala wake Ndege zilifikia pia sehemu nyingine ya Muungano?
 
Mimi ni mgeni humu hivi sukuma gang ni Wasukuma,kanda ya ziwa,au CCM.

Nakusikilizia counter hapa unijibu.
Wote ambao walikuwa wanamuona yule kichaa kama mungu wao, hii haijarishi una chama au huna.
 
Huyu Hangaya ana choko choko sana za chini kwa chini na makundi haya; 1. Bara 2. Wanaume 3. Kanda ya ziwa 4. Wanyonge ..acha tuendelee kumstahi kidogo
Mama anaupiga mwingi, wanaume kamili marijali tutamlinda kwa gharama yoyote dhidi ya wajane na mayatima aliowaacha mwendakuzimu.

Muacheni mama achape kazi, kutesa kwa zamu, sasa ni zamu yetu. [emoji817]
 

Hata ma Dc , Dc wa Iringa Mjini ni Mzanzibar.
 
Hii nchi kuielewa ngumu sana....

Ujenzi na Uchukuzi sio jambo la Muungano
Vipi kuhusu ATCL, ni shirika la Muungano au Tanganyika?
 
Mawazo hayo alikuwa nayo Nyerere yakamshinda akajiondokea zake seuze wewe mburumatari. Kua uyaone mambo
 
Kama ulivyosema yalimshinda Nyerere, wewe tulia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…