Naomba kueleweshwa suala la ndege ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Tanzania Bara kupokelewa Zanzibar

Naomba kueleweshwa suala la ndege ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Tanzania Bara kupokelewa Zanzibar

Unaweza kukuta ndege tayari zimeingizwa kwenye mambo ya muungano, si sisi wenyewe ndo tumekalia usukani bhanaa.

Hata sUala la mzanzibari kuwa waziri wa uchukuzi halijakaa sawa maana hilo siyo jambo la muungano, na ukifuatilia unaweza kukuta hata ma-DED ambao ni wazanzibari....
Huyu mama hatufai kabisa kabisa.katiba haijui
 
isee kama ni amri yangu zanzibar ningefanya tu jiji then wizara zote zingekuwa sawa na ningeamisha watu wengi sana hasa walaimu na maness na askari wazanzibar wangekuja huku na wa huku wangeenda kule hii ingesaidia kuondoa ile hali ya sisi wazanzibar sijui nini nini...ingepotea kabisa..
Huu ndio muungano hasa wa kusubiri uchafuzi unaopewa jina la uchaguzi , tupigwe marisasi Na viboko Lengo ni kutulazimisha tuwe waTanganyika kwa jina la Tanzania
 
Unaweza kukuta ndege tayari zimeingizwa kwenye mambo ya muungano, si sisi wenyewe ndo tumekalia usukani bhanaa.

Hata sUala la mzanzibari kuwa waziri wa uchukuzi halijakaa sawa maana hilo siyo jambo la muungano, na ukifuatilia unaweza kukuta hata ma-DED ambao ni wazanzibari....
Ni kama tu magufuli alivokuwa anapendelea chato, naona na mama sasa kabeba ndege na kupeleka Zenji
 
Mleta mada huoni kwamba ulitakiwa ujiridhishe kwanza, kama Wizara ya ujenzi ambayo kweli si ya Muungano ndio mmiliki wa hizo ndege?!

Kama taasisi inayo miliki hizo ndege iko moja kwa moja chini ya ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano, vipi ndege ziwe ni za upande mmoja kivipi?!
Mkuu kwa ufupi, hizo ndege huwezi kusema ni bara peke yake na huo ndio ukweli! Na mimi ni M-bara.
 
Ndege si mali ya atcl ni mali ya ile taasis ambayo si ei jii hana mamlaka kikatiba ya kuikagua mahesabu yake wala mikataba ya manunuz wanayoingia
 
NAOMBA KUELEWESHWA SUALA LA NDEGE YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YA TANZANIA BARA KUPOKELEWA ZANZIBAR.

ZAA = Zanzibar
TAA = Tanzania BARA

Naomba kueleweshwa kwa Uhuru wa mawazo "the right to express my opinion under Article 18 of the Constitution of Tanzania of 1977" kuanzia zamani hakuna pa kuongelea hadi zama za G55 ,Mchungaji Mtikila na sasa kwenye social media utapata mengi kuhusu malalamiko ya watanzania bara.

Tafuta habari ya ndege kupokelewa Zanzibar kisha soma maoni au nenda kwenye Political platforms mbalimbali,

Hoja sio MATUMIZI
Bali swala la Ujenzi na uchukuzi sio la MUUNGANO
Kwanini swala sio la MUUNGANO likafanyike Zanzibar??
Lini swala lisilo la MUUNGANO la Zanzibar litafanyika Tanzania BARA??
Ukiondoa Waziri wa Ndani Ulinzi Nje hakuna Waziri mwingine yeyote anahusika na chochote kule Zanzibar.

Pia TGFA na ATCL hawahusiki lolote kule Zanzibar sababu wapo Chini ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi isiyo ya MUUNGANO
Hapa MAMLAKA za Viwanja vya ndege Zanzibar wanayo yao
Usajili wa vyombo VYA usafiri wao
Kila kitu cha Ujenzi na uchukuzi chao wao wenyewe pekee DAIMA DUMU,

Ni vizuri wajue kuwa hizo ndege ni za Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA huko Zanzibar ni MAPOKEZI tu
Wasije anza sema SMZ imenunua ndege hizo
Hahaha! Zenj inapeta Sana awamu hii!
 
Dakika ya 10 ya mchezo, matokeo:

Wakojani 3 Sukuma Gang 0.

Bado dk.80
Haya maneno "Sukuma Gang" yatatuletea shida sana huko mbeleni kwa wale ambao watakuwepo hapa duniani..

Ukabila na Udini ni vitu viwili ambavyo vinagusa hisia za binadamu moja kwa moja...

Tuwe waangalifu kwa mstakabali wa vizazi vijavyo...

Ijumaa njema na mapokezi mema ya "ndege ZETU"...
 
Swali zuri.. Sikiliza kwa umakini na ili uelewe weka siasa pembeni.

TGFA ilishahama Wizara ya Uchukuzi tokea mwaka 2018, ilipitishwa na Bunge 2018, na GN ya serikali ilitoka 2018, iko chini ya State House, na TGFA ndio owner wa hizo ndege zote za ATCL kwa niaba ya Serikali.

Sasa, TGFA ndio inawabeba viongozi wote wa juu Serikalini, kuanzia Bara hadi Visiwani.. Kwa maana hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz, Rais wa Znz, Makamu wa Muungano na Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Zanzibar na Waziri Mkuu wa JM wa Tz, wote hawa wanapewa usafiri wa Anga na TGFA..

So ndege za TGFA, kupokelewa Znz, na baadae kukabidhiwa kwa mkataba ATCL ni sawa. Umeelewa?
Ndege ni za TGFA ipo chini ya IKULU kuanzia wakati wa Magufuli.
TGFA ni ya Tanzania BARA HAIHUSIKI Zanzibar kwa lolote
ATCL ipo chini ya WIZARA ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA
Hakuna sehemu yeyote ATCL wala TGFA inahusika na Zanzibar kwa lolote.
Zanzibar wana Taasisi zao wenyewe chini ya IKULU YA ZANZIBAR na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Zanzibar
Wana bajeti zao na kila kitu CHAO wenyewe Zanzibar PEKEE
 
NAOMBA KUELEWESHWA SUALA LA NDEGE YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YA TANZANIA BARA KUPOKELEWA ZANZIBAR.

ZAA = Zanzibar
TAA = Tanzania BARA

Naomba kueleweshwa kwa Uhuru wa mawazo "the right to express my opinion under Article 18 of the Constitution of Tanzania of 1977" kuanzia zamani hakuna pa kuongelea hadi zama za G55 ,Mchungaji Mtikila na sasa kwenye social media utapata mengi kuhusu malalamiko ya watanzania bara.

Tafuta habari ya ndege kupokelewa Zanzibar kisha soma maoni au nenda kwenye Political platforms mbalimbali,

Hoja sio MATUMIZI
Bali swala la Ujenzi na uchukuzi sio la MUUNGANO
Kwanini swala sio la MUUNGANO likafanyike Zanzibar??
Lini swala lisilo la MUUNGANO la Zanzibar litafanyika Tanzania BARA??
Ukiondoa Waziri wa Ndani Ulinzi Nje hakuna Waziri mwingine yeyote anahusika na chochote kule Zanzibar.

Pia TGFA na ATCL hawahusiki lolote kule Zanzibar sababu wapo Chini ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi isiyo ya MUUNGANO
Hapa MAMLAKA za Viwanja vya ndege Zanzibar wanayo yao
Usajili wa vyombo VYA usafiri wao
Kila kitu cha Ujenzi na uchukuzi chao wao wenyewe pekee DAIMA DUMU,

Ni vizuri wajue kuwa hizo ndege ni za Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA huko Zanzibar ni MAPOKEZI tu
Wasije anza sema SMZ imenunua ndege hizo
utawala ni kutoka hukooo,wa bara na visiwani
 
Ndege ni za TGFA ipo chini ya IKULU kuanzia wakati wa Magufuli.
TGFA ni ya Tanzania BARA HAIHUSIKI Zanzibar kwa lolote
ATCL ipo chini ya WIZARA ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA
Hakuna sehemu yeyote ATCL wala TGFA inahusika na Zanzibar kwa lolote.
Zanzibar wana Taasisi zao wenyewe chini ya IKULU YA ZANZIBAR na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Zanzibar
Wana bajeti zao na kila kitu CHAO wenyewe Zanzibar PEKEE
Ifike wakati mkubari kuwa sisi ni nchi moja, hizo ndege Ni Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukishasema hivyo tu wazanzibar wamo,sio TGFA Wala ATCL hao wasimamizi tu lakini ukweli upo palepale JMT ndio mmiliki.
Hizi ndege zinaporuka kwenye anga la Zanzibar utasema ziko nje ya nchi? Acheni utoto basi,.
 
Tuukuze utanzania zaidi kuliko kukuza mgawanyiko.Mimi kwangu sioni tatizo.Ndege zetu zinaruka katika anga la Tanzania ikiwemo Zanzibar.

Ndege hizi zinamilikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi.Pia Rais wa Zanzibar ni mumbe wa baraza la mawaziri kataika serikali ya jamuhuri ya Muungano.
😍👍
 
Ifike wakati mkubari kuwa sisi ni nchi moja, hizo ndege Ni Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukishasema hivyo tu wazanzibar wamo,sio TGFA Wala ATCL hao wasimamizi tu lakini ukweli upo palepale JMT ndio mmiliki.
Hizi ndege zinaporuka kwenye anga la Zanzibar utasema ziko nje ya nchi? Acheni utoto basi,.
😍
 
Ndege zote tulizonunua kama Taifa ni Mali ya Wakala wa Serikali wa Usafiri wa Anga (Tanzania Government Flight Agency) na huu wakala ni mali ya Muungano. Hivyo, sheria iliyoanzisha TGFA hizo ndege siyo ATCL bali mali ya TGFA. Pia tusisahau kuna TAA na ZAA. Hizi ni mamlaka za viwanja vya ndege. TAA na ZAA siyo wamiliki wa ndege, bali wamiliki wa viwanja vya ndege.

Kwa Tafsiri nyingine ATCL ni mali ya muungano kama ambavyo TGFA ni mali ya muungano.
 
Ndege ni za TGFA ipo chini ya IKULU kuanzia wakati wa Magufuli.
TGFA ni ya Tanzania BARA HAIHUSIKI Zanzibar kwa lolote
ATCL ipo chini ya WIZARA ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA
Hakuna sehemu yeyote ATCL wala TGFA inahusika na Zanzibar kwa lolote.
Zanzibar wana Taasisi zao wenyewe chini ya IKULU YA ZANZIBAR na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Zanzibar
Wana bajeti zao na kila kitu CHAO wenyewe Zanzibar PEKEE
Ikulu ya Tanzania ni ya Muungano.

Tanzania Government Flight Agency (TGFA)
is one of the executive agencies of Tanzania. It provides VIP flight services to government officials.[1][2] The Tanzania Government Flight Agency supports and manages all Tanzanian government aircraft, which it leases to Air Tanzania Company Limited (ATCL).[3]
 
Zile tisa zilipokelewa Bara hizi mbili kuna dhambi gani zikapokelewa huko Visiwani?. Ndio maana ya Muungano ni kuvumiliana na kuishi pamoja ni sawa na ndoa kila mmoja anaweka pembeni yale majivuno na ukubwa wake ili lengo la pamoja liweze kutimizwa.
 
Usikute wanatatua kero ya muungano. Inawezekana kabisa ATCL au Wakala wa Ndege za Serikali ikawa tayari imeorodheshwa kuwa kero ya muungano na sasa ndege hizo mpya kupokelewa kwake Zanzibar ni njia ya kutatua kero hiyo! Usicheke.....
 
Back
Top Bottom